Von G
JF-Expert Member
- Jan 21, 2015
- 243
- 246
Busquet, Carrick, Xabi Alonso wanafana kila kitu.Nashangaa Mourinho anavyohangaika kumsajili Nemanja Matic au Eric Dier kama viungo wa ulinzi yaani namba 6.
Kwanini asimsajili Sergio Busqet, kiungo matata katika nafasi ya Defensive Midfielder. Kusema kweli Sergio Busqet ni kiungo mkabaji pengine wa muda wote sema hapewi sifa zake na wadau wa soka.
Najua mtashangaa, kwakuwa wengi mmekariri kuona namba sita akiwa na sifa ya kupiga makwanja (tackling) lakini kwa Sergio habari ni tofauti yeye anajua sana kukaba nafasi na kufanya interception huku akiwa na jicho la ziada la kuanzisha mashambulizi yenye akili. Kwakifupi huyu ndio muhimili wa Barca na Timu ya taifa ya Spain.
Ifikie muda tuanze kutambua mchango mkubwa wa Sergio hasa wakati huu ambao akina Messi na Neymar wakiongezewa mikataba minono kuliko Busqet.
Ningefurahi kama siku moja Mou au Guardiola wakimleta EPL Sergio Busquet, mmoja kati ya wachezaji wasiopewa heshima na sifa zake!
Huwa tunawaita Invisible midfielder