Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,600
- 35,158
Wiki kadhaa niliposti uzi wa kulishauri jeshi (JWTZ) kuwekeza kwenye technolojia bahati nzuri kila mtu alitoa mawazo yake kuna walio kosoa kuna walio unga mkono nk nk!!
Lakini leo acha niongelee hili kidogo! na nitapenda kuongea na hawa wavaa miwani myeusi (TISS) maana naamini kwenye nchi yeyote hawa jamaa ndio moyo kama sio uti wa mgongo wa nchi! na wakichemka tu nchi imeenda na maji!!
Niseme wazi kabisa HAKUNA NCHI DUNIANI IMEENDELEA BILA KUWEKEZA KWENYE ELIMU NA TEKNOLOJIA! Hakuna na wala haito kuwepo!
Lakini nashangaa sana hii nchi yetu mambo ni tofauti kabisa! maana hakuna mtu anayechukulia elimu kwa uzito wake!
Mpaka leo kuna shule hazina vyoo alafu nguvu tumezipeleka kwenye reli inayojengwa kwa mkopo badala ya kuboresha mfumo wa elimu! Leo hii DED ananunua gari la 400mil wakati kwenye halmashauri yake kuna shule hazina madarasa nayie ndugu zetu wavaa miwani ya tinted mpo tu mnaangalia kama hamuoni!
Ukiwa na ELIMU MBOVU kamwe usitarajie uwe na TEKNOLOJIA maana TEKNOLOJIA ni matokeo ya uwekezaji kwenye elimu!
Mfano hizi siku mbili tatu tumekuwa na tatizo la LUKU ambalo limepelekea baadhi ya watendaji wa TANESCO watumbuliwe lakini kabla ya kuendelea embu tujiulize...
JE huu mfumo wa LUKU aliye utengeneza ni mtanzania au watu wa nje? kama umetengenezwa na watu wa nje ina maana Tz nzima hakuna mtu aliye kuwa na uwezo wa kutengeneza mfumo kama huu? ni kweli nyie TISS mlishindwa kabisa kushauri apatikane mtu wa kutengeneza mfumo kama huu hapa Tz? ina maana mlishindwa hata kushauri tenda wapewe maprofesa wetu huko vyuoni?
Kama hujui, kwenye coding/programming mtu anayetengeneza software ana uwezo wa kuacha malango wa nyuma (back door) kwa ajili ya kuingia kwenye mfumo muda wowote atakao! je kama mifumo mingi serikalini inaundwa na makampuni ya nje je unadhani wanashindwa kutengeza hii backdoor ili waweze kuingilia mfumo muda wowote wanao taka? na kama wanaweza usalama wetu ukoje?
Infact mifumo mingi ya technolojia nchini (ikiwemo LUKU) kuna uwezekano mkubwa imetengenezwa wa watu wa nje na hii ni moja kati ya matokeo ya kuwekeza kwenye siasa badala ya kuwekeza kwenye elimu na technolojia!
Yani ni aibu mwanafunzi wa computer engineering (baadhi yao) wanaanza chuo mwaka wa kwanza alafu hajui hata kuwasha laptop (leave alone kuitengeneza) na mbaya zaidi hawa hawa wana-IT na wahandisi wa kompyuta wanao anza chuo wakiwa hawajui hata kuwasha laptop ndio tunao watengemea watuendeshee mifumo ya LUKU!
Je kwa mtindo huu LUKU itaacha kusumbua kweli? Je huyu mwanafunzi wa computer engineering anayetoka pale UDSM ambaye hajui hata kutengeneza kawebsite ataweza kutengeneza mfumo kama wa LUKU? Je hata kama hawezi kutengeneza ataweza kuusimamia kweli?
Kumtumbua kiongozi wa TANESCO sio suluhisho, kama kweli tunataka kuikomboa hii nchi JAMBO LA KWANZA NI KUUFUMUA MFUMO WA ELIMU then TUWEKEZE KWENYE TEKNOLOJIA! Leo utamtumbua mtu wa TANESCO alafu una muweka mwingine ambaye nae ni zao la mfumo mbovu wa elimu je tatizo likirudia utamtumbua tena?
Sasa tatizo la LUKU ni muendelezo wa uwekezaji mbovu kwenye elimu na technolojia kiasi kwamba kama nchi tunaishia kutegemea watu wa nje watutengenezee mifumo nyeti ya nchi kitu ambacho kiusalama ni hatari sana!
Narudia tena HAKUNA NCHI HAPA DUNIANI ILIWEZA KUENDELEA BILA KUWEKEZA KWENYE ELIMU BORA NA TEKNOLOJIA!
Magufuli, Samia, Majaliwa hawa wote ni wana siasa na wataondoka na kuiacha nchi yetu, lakini nyie ndugu zetu wavaa miwani ya tinted kama nilivyo sema hapo awali nyie ndio moyo wa taifa na mngekua makini zaidi basi mlitakiwa hata hili la LUKU mlione na hata kama hamkuliona mapema basi sasa ndio wakati wa kujipanga lisirudie tena!!
Anzeni kuwalazimisha hawa wanasiasa waanze kuwekeza nguvu kwenye elimu ili tupate vijana wenye IQ kubwa na wenye uelewa wa maswala ya IT na sio taifa linakuwa na wahitimu wa computer ambao ukiwaambia watengeneze website hawajui mwishoe tunaishia tunategemea watu wa nje watutengenezee mifumo yetu!
Kwa kifupi aibu tupu!