Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kichwa cha Habari Chajieleza , Uongozi wowote wa Umma Duniani kote ni dhamana ya muda mfupi sana , tena ni dhamana ya kusaidia kuboresha maisha ya jamii husika (BOTTOM UP) , ni fursa kwa aliyechaguliwa kuongoza kuonyesha Uwezo wake wa kuisaidia jamii yake .
Maana yake ni kwamba viongozi wa Umma kazi yao kuu ni kuhakikisha wanainua Jamii yao kutoka chini na kuipeleka juu kiuchumi , na baada ya hapo tutaona maendeleo binafsi ya mwananchi mmoja mmoja na hatimaye Jamii nzima .
Jambo hili ni tofauti kidogo kwa Nchi ya Tanzania , huku kwenyewe Viongozi wanateuliwa ili kuwezesha Chama chao kushinda Uchaguzi Ujao , kwa njia zozote zile ikiwemo Mauaji , Wizi wa kura , uonevu na ubambikaji kesi , Ushahidi wa Jambo hili ni idadi kubwa ya Mawaziri ambao uchaguzi uliopita Walipita bila kupingwa , Akiwemo Waziri Mkuu , hawa wote walipita hivyo baada ya washindani wao kupotezwa , kuteswa , kupigwa ama kudhulumiwa .
Nchi yenye viongozi wenye akili kama hizi haiwezi kuendelea milele , hata kama itauza Bandari , mbuga , misitu pamoja na Raia wake .
Naona Aibu sana kuwa miongoni mwa Raia wa Tanzania wa Kuzaliwa , Kiukweli Najuta