Hakuna nchi yenye starehe Kama Tanzania na Burundi kidogo

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Nimetembea nchi zote hizi zinazotuzunguka hamna nchi Tamu Kama Tanzania hii nchi laini sana just imagine unazaliwa kwenye familia ya kimaskini ila probability ya kutoboa inakuwepo.

Nenda Kenya kaone hata ardhi kuipata ni ngumu kama kwenu masikini. Nchi nyingine ndo zinachekesha kabisa just imagine unaenda nyumbani kwa Mwanamke unamkuta baba yake na hakwambii kitu kisa umebeba karanga, mahindi na mazaga zaga.
 
Tanzania nchi nyepesi sana kuishi.. posta city centre machinga wanaweka genge ama mzigo wa milion hata 100, na hakuna cha TRA kuwagusa wala nani.. machinga anamuogopesha afisa wa TRA hata kumsogelea... ukimgusa tu kiongozi wa machinga akampigia simu namba moja, hiyo ajira ya TRA inaisha siku hiyo hiyo
 
We ungeenda Brazil aka kwa pele ndiyo ungeona balaaa

Ova
 

mawazo ya wasiotembea
 
Kipimo kimojawapo ni wasio raia wa TZ, wakikaa TZ kwa muda fulani, huhitajika winji kurejea walikotoka, hata ikiwa ni zile nji za 'mamtoni'. Aghalabu, wengi wao hurejea TZ kupitia NGO, makampuni au bendera nyingine mradi tu waendeleze uhalali wa kukaa kwao TZ. Wanarejea kwao tu kula Thanksgiving / Kiri-si-Maasi.
 

kichwa cha habari ni starehe sio kupanga mizigo posta
 
Mfano balozi Donald Wright aliwahi ishi bongo mwaka jana karudi tena kama balozi
 
Mfano balozi Donald Wright aliwahi ishi bongo mwaka jana karudi tena kama balozi

Huyo Mheshimiwa Balozi atakuwa anaionjoi sana. Waafrika fulani walipata ajira kwenye NGO iko based Marekani. Duty post Afrika chini ya Jangwa la Sahara. Yaani wanapata salary ya Kimarekani, kwa maisha ya Kiafrika. You cannot beat that combination!

Pana kampuni inayorhyme na "Bongo siondoki", nasikia ilianzishwa na Bazungu. Kila nikiona matangazo yao, yananipa wivu. Kama Bazungu benyewe banasema "Tutabanana hapahapa", kulikoni kina siye kutaka kuzamia kwenda kwao "majuu"? Wao wanaona nini hapa kwetu ambacho wazawa hatukioni?
 
Burundi kuna starehe gani ndugu? Bora ungetaja Kampala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…