Uchaguzi 2020 Hakuna pingamizi atawekewa mgombea wa CHADEMA

Uchaguzi 2020 Hakuna pingamizi atawekewa mgombea wa CHADEMA

Zile saa nane ama yale masaa manane jana ya tar 25. August. 2020 ya kumsubirisha mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA kuanzia saa sita mchana mpaka jioni ya saa moja na dk 40 yalikuwa ni faida tupu kwakwe.

Trust me wale wagombea wengine waliopewa kipaumbele na kuharibu ratiba wakaingia fasta wakapokelewa na kupitishwa haraka wamefanya makosa mengi ya kisheria na hili litawagharimu pakubwa.

Mgombea wa CHADEMA ndie pekee kazunguka mikoa 16 katika uhalisia wake kutafuta wadhamini...hii imempa credit kubwa sana..ni awali njema..awali iliyokosa mawaa wananchi katika uhalisia wao na kwa furaha bila shuruti wakamdhamini kwa mikono yao na vidole vyao wenyewe..hii kiroho ni hali chanya yenye uhai.

Wagombea wengine wamepata wadhamini kupitia daftari la kupigia kura(pengine kupitia tume ya uchaguzi) yamenyofolewa majina wakajaziwa...akidi ikatimia tume ikapitisha kwa mtazamo wa haraka unaweza kudhani hakuna shida...! Lakini kiroho kuna shida kubwa sana.

Udhamini wa hawa wagombea wengine ni mfu hauna uhai kwakuwa mgombea hajakutana ana kwa ana na hao anaotaka wamdhamini. Udhamini wa hawa hauna msingi chanya kwakuwa baadhi ya hayo majina kuna marehemu ndani yake. kuna wengine hawampendi tena mgombea..kuna wengine wameshahama vyama nknk. Nina hakika hata wengine number zao za simu hazipatikani tena ama wao wenyewe hawajulikana walipo. Kwahiyo hapa tunaona wazi kabisa hakuna muunganiko wa kiroho na hata kimwili kati ya mdhamini na mdhaminiwa

Ukiachana na hayo upangaji wa mipango na ratiba ya kuomba udhamini kwa CHADEMA vilikuwa vizuri na vya viwango vinavyotakikana na tume ya uchaguzi na kwa sheria za uchaguzi..namna watu walivyojikusanya na kukusanyika..vibe chanya waliyokuwa nayo..zoezi zima la udhamini lilivyoenda nknk..ukiachana na delayments zisizozuilika zoezi zima la kutafuta wadhamini lilikuwa perfect..Hili limekishape chama na kukiongezea credit kubwa!

Uwezo na matumizi ya fedha...kwenye hili tena CHADEMA wamepiga bao lingine la haja..Jamani inahitajika mipango kabambe na fungu la kutosha kuweza kuzunguka mikoa 16 na mfasara wa watu wasiopungua 20 na wote hao wapate chakula malazi nk na magari yapate mafuta nk

Udhamini wa kimyakimya ni udhamini wa kificho na uliojaa makandokando mengi hata kijamii pia ukiachana na kisheria..hauleti tumaini na hisia za umoja na kuwa wamoja kati ya mdhamini na mdhaminiwa.

Tuna masaa chini ya 15 kwa ajili ya kuwekeana mapingamizi ni masaa machache lakini yaliyobeba simulizi nyingi...wewe wakati uko kitandani mwako umelala kuna watu hawajalala wala kupumzika wako busy kuhakikisha wanaruka na kukwepa vizingiti na hila zote za pingamizi.
Wakati mnaendelea kujipamba mtandaoni, CCM inaendelea kujikusanyia wabunge majimboni.
 
CDM walijua kwani sio mara ya kwanza kusimamisha mgombea. Unafikiri wangepona kama walikwenda kinyume. Hiyo ingekuwa zawadi kubwa kwa JPM na wange waengua mapema kabisa bila huruma. (I stand to be corrected).
Kusema kweli haya mambo mengine ni ukiritimba tu (wa CCM na serikali zao), after all wanaochagua ni wananchi kwa kura zao.
Sawa kabisa, nakubaliana na wwe. Wangelipata sababu nzuri sana! Ni uabtili, waachie wananchi wachague, hakuna sababu ya Mkurugenzi na tume kumpitisha mtu, wacha wanachi wawapitishe kwa kura!
 
Majimbo aliyozunguka Lisu kutafuta wadhamini Ni 20 CCM tayari imeshachukua majimbo 22 ambayo wabunge wa CCM wanepita bila kupingwa

Hapo unaweza kuona kuwa ziara zake Ni hopeless sababu Hadi Sasa Hana mbunge kote alikozunguka

Wewe nae Ni shida
 
Lakini katika katiba ya Tanzania ibara ya 66 imetaja makundi ya wabunge sijaliona hilo kundi la wabunge wanaopitishwa bila kupingwa katika katiba inatambua a) wabunge wa kuchaguliwa b) wabunge wa kuteuliwa na Rais na c) wabunge wanawake wanaochaguliwa kutoka katika vyama vyenye wabunge. Sasa hawa wanaopitishwa na tume kabla ya uchaguzi wao kundi lao ni lipi na bungeni watakuwa wanamuwakilisha nani hiyo tume iliyowapitisha au na kwa kutumia katiba ipi.maana katiba iliyopo haitambui hili kundi lao.
Naona watakuwa wanawakilisha Wajumbe
 
Majimbo aliyozunguka Lisu kutafuta wadhamini Ni 20 CCM tayari imeshachukua majimbo 22 ambayo wabunge wa CCM wanepita bila kupingwa

Hapo unaweza kuona kuwa ziara zake Ni hopeless sababu Hadi Sasa Hana mbunge kote alikozunguka

Upuuzi pitishenu watu wagombee mnaogopa nin achen hoja za kitoto
 
Kimsingi kuna wagombea fake wamepandikizwa uchaguzi huu, sikuamini hata yule Mbobezi wa TISS anasema walisaka wadhamini kimya kimya, kuna jambo hapo la kuchukua.
Hao wengie akina mapumba na shibudi tunawajua kitambo, hakuna haja kuwajadili.
 
Je kukubalika kwa Lissu ni kwa sababu
A; Lissu anapendwa kuliko Jiwe au
B: Watu wanamchukia Jiwe?
 
Majimbo aliyozunguka Lisu kutafuta wadhamini Ni 20 CCM tayari imeshachukua majimbo 22 ambayo wabunge wa CCM wanepita bila kupingwa

Hapo unaweza kuona kuwa ziara zake Ni hopeless sababu Hadi Sasa Hana mbunge kote alikozunguka
Hopeless anapoandika hopeless inakuwa Ni HOPELESS+
 
Zile saa nane ama yale masaa manane jana ya tar 25. August. 2020 ya kumsubirisha mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA kuanzia saa sita mchana mpaka jioni ya saa moja na dk 40 yalikuwa ni faida tupu kwakwe.

Trust me wale wagombea wengine waliopewa kipaumbele na kuharibu ratiba wakaingia fasta wakapokelewa na kupitishwa haraka wamefanya makosa mengi ya kisheria na hili litawagharimu pakubwa
 
Nasubiri kuona namna Lisu atakavyoweza kupata asilimia 7,ya kura! Asilimia saba
 
Majimbo aliyozunguka Lisu kutafuta wadhamini Ni 20 CCM tayari imeshachukua majimbo 22 ambayo wabunge wa CCM wanepita bila kupingwa

Hapo unaweza kuona kuwa ziara zake Ni hopeless sababu Hadi Sasa Hana mbunge kote alikozunguka
Aisee lakini muda bado sana lolote kisheria linawezekana kuhusu hao walipita bila kupingwa na nn tafasiri ya neno hill kisheria bado kazi ipo.
 
Back
Top Bottom