Hakuna record label ninayoweza kukubali inisainishe, watanipa nini ambacho sijafanya! – Diamond

kasema anataka kitu special toka hzo record labels,maoni yake ni kwamba bado hawajamshawishi,kasema kila kitu anaweza kukipata kupitia mgt yake.kama kuna kizur cha ziada kinachofanywa na hzo record labels labda angekubali mikataba yao.
 
huyu kijana anatudhihirishia kushuka sana, na kwenye mziko hakuna anachokifahamu, sasa asubiri hao madogo wake wampge chini ndo atajua

Inawezekana ni kweli Diamond kwenye Muziki hafahamu kitu, je wewe level yako ya kufahamu Muziki inaishia wapi? Kutunga, kuimba, Kukosoa, kuponda au?

Kwa kigupi alichokiongea Diamond kina maana sana kwa Bongo na Africa kwa Ujumla, Mambo ya Filam na Muziki wa Kiafrica bado uko local na unaweza kushine Africa nzima bila kuwa na Lebel yoyote, unaweza kuniambia Koffi Olomide yupo Lebel gani?, mbona Muziki wake Ekotite umechezwa Africa nzima?

Kwa Africa unahitaji uwe na watu kama Babu Tale,Mkubwa Fella na aina kama hiyo, kwa kifupi hao jamaa wanaujua muziki wa Tanzania na East Africa vizuri sana, Wakina Nature walikuwa wanaimba hovyohovyo tu lakini jamaa waliwavuta na kuwatengenezea TMK ambayo ilitingisha nchi nzima, haohao ndio waliowatengeneza Yamoto Band, haohao ndio wanamsimamia Diamond na sasa Wameshawaibua Ray na Harmo

Kwa taarifa yako tu lebel kama Sony isingeweza kuwainua watu kama Harmo, Ray au Yamoto , sasa kama wakina Fella wamekuinua na umepata sifa Africa na unapata show kubwa, unaweza record kwa Godfather na video na nyimbo zako zinakubalika Africa nzima unaenda kwa lebel kubwa kama Sony kufanya nini?

Kiba kapote kwenda Sony
 
Ngoja TCRA wafungie hivyo vimeo ujinga upungue humu ndani
 
Kambona andika vizuri basi uandishi gani huu wa Facebook?
 
Nilichogundua Watanzania wengi hatujiamini katika maamuzi na tunaamini kutoka mpaka usimamiwe.

Swali

Diamond akisainiwa atafanyiwa kipi cha ziada ambacho yeye hawezi kukifanya Collaboration,Kushoot video mzuri,Show za Afrika na Ughaibuni au Matangazo?

Maana hayo yote kashayafanya yeye kama yeye na management yake tu sasa hizo label zitamfanyia kipi cha ziada? Jamani mbona jambo dogo tu hilo tutumie ubongo kufikiri.
 
Kama label hazina maana yeye anataka kuanzisha ya nini? au anayo ya nini?!!!
Anyway anaonyesha kipaji cha ujinga na kukipromote
 
Domo atawaua na presha!! Tangazo tu anafanya kama mziki (tangazo la cocacola)
Kama hauna tongotongo au mgandamizo wa hisia alichosema yupo sahihi na tayari ana label yake, sasa wewe shupalia "aje" yako mpaka mapovu yakutoke kwenye matundu.

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Watu wa uswahilini hawahitaji Sony au Warner kusikiliza hizi Bongo fleva.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…