Hakuna sababu ya kumchukia Waitara, ameonesha uzalendo wa hali ya juu

Hakuna sababu ya kumchukia Waitara, ameonesha uzalendo wa hali ya juu

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Inashangaza sana kwa watu wenye akili timamu kumchukia mtu ambae amejitolea kulisaidia taifa kuibua ubadhirifu au ufisadi.
Mwita Waitara alijilipua ili kuupa umma wa watanzania ukweli juu ya unadhirifu unaofanyika ndani ya Chadema.

Mwita aitara amefanya jambo hili kwa kutumia haki yake ya kikatiba kama ibara ya 18(d) ya katiba ya JMT inayotoa haki ya kupashana habari juu ya mambo muhimu ya jamii ya Tanzania.

Mfano ni nani alikuwa anafahamu kuwa mwenyekiti wa Chadema alikuwa anaikopesha Chadema bila maandishi na sasa analipwa mil 50 kila mwezi?.

Hivyo sioni sababu ya watu kumchukia mpiga mbiu huyu ambae amelisaidia taifa kufahamu mengi yaliyokuwa yamejificha.

Jana kuna watu walimfanyia vurugu wakati anafanya shughuli za kiserikali. Inashangaza sana wanachama na wafuasi wa Chadema kufurahia kuwa alitaka kupigwa kama mwizi. Wakati ukweli ni kuwa aliondoka baada ya watu waliotumwa kumletea vurugu.

Hivyo kama mtu anasema ukweli hakuna haja ya kumchukia bila sababu. Maana ameisaidia jamii yetu kupata ukweli.
 
Hakuna aliyetumwa pale. Ifike mahali tukubaliane kwamba si sawa kudhani kwamba kila anachofanya au anachosema kiongozi ni sahihi na kila asiyekubaliana nacho ametumwa au amenunuliwa

Haya ni mawazo mgando. Ni sawa na kukwepa ngumi kwa kufumba macho
 
Una uhakika na hayo unayoyasema, mbona unaingilia uchunguzi wa Takukuru je ukiitwa ukathibitishe haya uliyoyasema upo tayari. Nyie ndo mnaompa wakati mgumu Maxence Melo anaingia gharama za mawakili kutetea. Hebu tulia vyombo vinafanya uchunguzi wake
 
Hakuna aliyetumwa pale. Ifike mahali tukubaliane kwamba si sawa kudhani kwamba kila anachofanya au anachosema kiongozi ni sahihi na kila asiyekubaliana nacho ametumwa au amenunuliwa

Haya ni mawazo mgando. Ni sawa na kukwepa ngumi kwa kufumba macho
Ok kwahy hata Viongozi wa Chadema wanaohama hawanunuliwi eti ee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna aliyetumwa pale. Ifike mahali tukubaliane kwamba si sawa kudhani kwamba kila anachofanya au anachosema kiongozi ni sahihi na kila asiyekubaliana nacho ametumwa au amenunuliwa

Haya ni mawazo mgando. Ni sawa na kukwepa ngumi kwa kufumba macho
Kwa hiyo Waitara alifanya kosa gani? Kusema suala lipo mahakamani? Kusoma barua ya mkuu wa wilaya? Na hao waliozomea na kuleta vurugu walijileta?
 
Waitara Mwita ni Bonge moja la MNAFIKI. Huyu jamaa alikuwa CHADEMA hivo ni SEHEMU YA UFISADI HUO ...!!Lakini leo anajifanya malaika baada ya kuhamia CCM. Huyu jamaa Wakurya wanawaita " MURISYA"!
 
Back
Top Bottom