Hakuna sababu ya kumchukia Waitara, ameonesha uzalendo wa hali ya juu

October nyimbo itakuwa ni buriani chadema,buriani chadema.
Manyumbu yalikupenda sana ila bwana amekupenda zaidi.
 
Chadema ina nguvu sana nchi nzima hadi chattle.
 
Ningemwelewa tu kama angejilipua na kuupa umma wa watanzania maovu ynayotendwa na ccm na serikali yake.
Kujilipua sio njia pekee ya kuweka wazi malalamiko ambayo unahakika yapo ya yanatakiwa kupata majawabu. Na kitu kingine ambacho tunaweza kukiona kibaya leo kumbe uchunguzi huu unaweza ukakitengeneza chama.

Ni malalamiko haya kuhusu matumizi mabaya ya pesa ya chama ndiyo hufanya kukichafua chama hasa wale ambao wanataka kuwa wanachama lakini wapata woga.
Mhe Mbowe ni kiongozi mzuri lakini ana kura moja tuu. Lazima tutengeneze uwanja ambao watu wengi watakuja tuendeleze chama na kuweza kuchukua dola.
 
Hakuna aliyetumwa pale. Ifike mahali tukubaliane kwamba si sawa kudhani kwamba kila anachofanya au anachosema kiongozi ni sahihi na kila asiyekubaliana nacho ametumwa au amenunuliwa

Haya ni mawazo mgando. Ni sawa na kukwepa ngumi kwa kufumba macho
Kwa hiyo unakubali kuwa si kila analofanya ama kusema Mwenyekiti wa Chadema ni sahihi na wanaompinga hawajanunuliwa??? 🔨
 
Maovu gani? Kuimarisha sekta ya afya? Kuimarisha miundo mbinu? Kudhibiti mafisadi na wabadhirifu?

Waliotaka kumpatia kipondo, je walikuwa wanapinga kuimarishwa kwa secta hizo?

Unaweza danganya watu fulani kwa wakati fulani, lakini huwezi kuwadanganya watu wato kwa wakati wote.
 
Mara mia mbowe kuliko jiwe, sidhani kama hata kibila lake unalijua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhuru wa maoni siku hizi hauko neutral tena; uko biased against maoni yako hayapendezi upinzani. Nimeona hapa watu hawajadili hoja kwa uhakika bali wanatumia hisia zaidi. Kuna hoja moja iliyoko mpaka sasa kuhusu Corona na lockdown; kwa wale jamaa wengine eleweni kuwa sina maana ya kitu hii


Pande zote mbili zina ukweli fulani: (a) Corona husambaa kwa watu wengie kukutana, (b) Watu wengi watakufa wasipopata njia za kujipatia kipato chao cha kila siku. Badala ya watu kujadili jinsi pande mbili hizo za shilingi zinawezaje kuunganishwa ili kuwa na jibu mbadala wa tatizo letu, imekuwa ni kama mashindano ya ama lockfown au hatutaelewa, na upende mwingie ukiwa tutafuangua au hatuatelewa. Hiyo ni jamii ya hatari sana kuwamo. Hata rangi kwenye picha zetu za digital huanzia 0 hadi 255 siyo 0 na 1 tu. Sasa hivi watanzania tumekuwa kama vile tuko kwenye binary life ambapo picha inakuwa pixelated sana badala realistic fuzzy life ambapo picha inakuwa smooth.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…