Hakuna Shahidi Anayeweza Kutoa Ushahidi Kwa Kificho Halafu Asijulikane Milele

Uamuzi wa Mahakama wa kuruhusu mashahidi wa kificho, kwa kweli ni uamuzi wa kishetani, unaolenga kudhulumu haki.

Hii ni njia ya waliombambikizia Lisu kesi ya uhaini, kuwatafuta mashahidi wa kutengenezwa.

Hakuna msema ukweli anayeweza kuogopa kujulikana. Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuleta ushahidi wa tishio la kushambuliwa kwa vile atatoa ushahidi dhidi ya Lisu. Sasa kwa nini mashahidi watoe ushahidi kwa kificho?

Waliomtengenezea Lisu kesi wamejawa na aibu ya ushetani walioufanya, ndiyo maana wanazidi kuhangaika kwa kufanya ushetani zaidi unaozidi kuwadhihirisha jinsi walivyojawa na ushenzi.

Lakini kwa hakika nawaambieni, hakuna shahidi wa kutengenezwa hata mmoja ambaye hatajulikana.

Lakini pia hao mashahidi wa kutengenezwa wajue kuwa baada ya huo ushahidi wa kutengenezwa, kamwe hawataionja amani mioyoni mwao maisha yao yote. Na waliowapa hiyo kazi, kwa kuwa wanajua CCM haitadumu madarakani kwa muda mrefu, ili wasiwe na mashaka kuwa hawa mashahidi wa kutengenezwa siku moja wataitoa hiyo siri, watawaua baada ya muda si mrefu.

Kama wana akili, wajiulize, wako wapi wale waliotumwa kumuua Imran Kombe aliyekuwa DG wa intelligence. Wajiulize, wako wapi wale waliotumwa kwenda kumuua Lisu kwa kumshambulia kwa risasi? Aliye hai si huyo mmoja tu ambaye naye yupo gerezani? Mnadhani wameuawa na nani? Si hao hao waliowatuma kwenda kufanya uharamia? Na hata hawa mashahidi wa kutengenezwa, kwa vyovyote, nao wataishia kwenye njia hiyo hiyo. Na hakika watatangulia wao kuondoka katika Ulimwengu huu kabla hata ya Lisu wanayetaka kumwua bila ya hatia yoyote.

LISU HANA HATIA, HATIA YAKE KWA SHETANI, NI KUPINGA UOVU, NA KUETETEA HAKI KWA WATU WOTE. Sina shaka, Mungu atamwinua Lisu, na kuwadhalilisha mashetani yaliyojipanga
Hata hivyo watu watajulikana tu hasa kutokana na uwezo wao mdogo wa kufikiri hivi mlikuwa mnajua kwamba watu wengi ni wavivu wa kufikiri

Binadamu ana akili sana lakini binadamu huyo huyo ni mvivu wa kufikiri

Binadamu akipata changamoto uwezo wake wa kufikiri huongezeka niishie hapo naweza nikafungua codes bure
 
Ila c n huyu huyu mbowe mlikuwa mnamsifia mpaka kumuona n mungu mdogo 😂 kwel siasa n akili

Sasa unashangaa nn hapo, watu hubadilika kwani hujui hili?!.
Mbowe turning point yake ilikuwa pale alipotoka jela!.
 
Uamuzi wa Mahakama wa kuruhusu mashahidi wa kificho, kwa kweli ni uamuzi wa kishetani, unaolenga kudhulumu haki.

Hii ni njia ya waliombambikizia Lisu kesi ya uhaini, kuwatafuta mashahidi wa kutengenezwa.

Hakuna msema ukweli anayeweza kuogopa kujulikana. Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuleta ushahidi wa tishio la kushambuliwa kwa vile atatoa ushahidi dhidi ya Lisu. Sasa kwa nini mashahidi watoe ushahidi kwa kificho?

Waliomtengenezea Lisu kesi wamejawa na aibu ya ushetani walioufanya, ndiyo maana wanazidi kuhangaika kwa kufanya ushetani zaidi unaozidi kuwadhihirisha jinsi walivyojawa na ushenzi.

Lakini kwa hakika nawaambieni, hakuna shahidi wa kutengenezwa hata mmoja ambaye hatajulikana.

Lakini pia hao mashahidi wa kutengenezwa wajue kuwa baada ya huo ushahidi wa kutengenezwa, kamwe hawataionja amani mioyoni mwao maisha yao yote. Na waliowapa hiyo kazi, kwa kuwa wanajua CCM haitadumu madarakani kwa muda mrefu, ili wasiwe na mashaka kuwa hawa mashahidi wa kutengenezwa siku moja wataitoa hiyo siri, watawaua baada ya muda si mrefu.

Kama wana akili, wajiulize, wako wapi wale waliotumwa kumuua Imran Kombe aliyekuwa DG wa intelligence. Wajiulize, wako wapi wale waliotumwa kwenda kumuua Lisu kwa kumshambulia kwa risasi? Aliye hai si huyo mmoja tu ambaye naye yupo gerezani? Mnadhani wameuawa na nani? Si hao hao waliowatuma kwenda kufanya uharamia? Na hata hawa mashahidi wa kutengenezwa, kwa vyovyote, nao wataishia kwenye njia hiyo hiyo. Na hakika watatangulia wao kuondoka katika Ulimwengu huu kabla hata ya Lisu wanayetaka kumwua bila ya hatia yoyote.

LISU HANA HATIA, HATIA YAKE KWA SHETANI, NI KUPINGA UOVU, NA KUETETEA HAKI KWA WATU WOTE. Sina shaka, Mungu atamwinua Lisu, na kuwadhalilisha mashetani yaliyojipanga
Kipi rahisi kwako kukitambua kati ya ?

Mtumiaji wa jf kwa utambulisho feki au shahidi wa jamhuri aliyefichwa ?
 
Uamuzib wa ajabu sana lengo hapa ni kitaka kumnyonga Lisu,Ila Mungu yupo atasimamia haki
 
Mashahidi wasiojulikana......hahaha.....hizi mambo zitakuja kubackfire tu

Na hao mashetani walioanzisha huu ujinga wa kuwa na mashahidi kificho, kuna siku watajutia.

Wakumbuke yaliyompata Hayati Keneth Kaunda. Aliweka sheria za hovyo kuwakomoa wapinzani. Alipoingia Chiluba, alitumia sheria alizotengneza Kaunda kumdhibiti Kaunda. Kaunda alijuta, mpaka wtu wake wakamwomba Mwalimu Mwalimu Nyerere, ndiye alieongea na Chiluba, ikawa pona yake.

Haya masheria ya ajabu kuna siku yatakuja kutumika dhidi ya Samia au Masaju au watu wa magenge yao.
 
Back
Top Bottom