Hakuna show itakayoandaliwa na clouds weusi wakakosekana...

mkuu wa bongo fleva clouds.. ni b 12.. na b12 ni mtoto wa arusha, hawezi watosa jamaa zake.. msaidizi wa b 12 ni adam mchomvu nae mtoto wa arusha.. wanajua wakiwatosa weusi wakirudi likizo makwao arusha watatengwa na jamaa wa kitaa..

so wasanii wa arusha wana nafasi sana clouds.. na weusi ndio best wasanii wa arusha.. so wanapewa chance wao sana
 
kama ni hivyo mbona Kiba na Mond hawawabebi jamaa zao wa Kigoma? au ndo tuamini maneno ya Msindi Sele?
 
kama ni hivyo mbona Kiba na Mond hawawabebi jamaa zao wa Kigoma? au ndo tuamini maneno ya Msindi Sele?
Ni kuamua kama unafanya mziki biashara au mziki harakati.
Mziki biashara, utaepuka maugomvi yasiyokuwa na maana, upige pesa yako uwekeze uendelee na maisha. Mziki harakati utaongea sana na kuponda watu, usiitwe kwenye show, uchague upande mwisho ufulie ubaki kulaumu kwamba ulibaniwa.
Mimi siyo fan wa weusi wa sasa, ila hawa jamaa uwa wanajitahidi kuwa neutral na pia comments zao. Yani hata kipindi cha uchaguzi walikataa fanya kampeni chama chochote kulinda biashara yao ya mziki
 
nimekuelewa sana mkuu
 
kama ni hivyo mbona Kiba na Mond hawawabebi jamaa zao wa Kigoma? au ndo tuamini maneno ya Msindi Sele?

diamond, kiba ni wa kigoma lakini hajakulia kigoma

b 12 na mchovu arusha ni nyumbani kwao kabisa walipokulia.. na mikoani miji ni midogo.. joh makini na b 12 wanajuana kitambo tangu enzi za mipira ya utotoni.. na marafiki wa kitaa wa joh makini ndio hao hao wa b 12..

so ile aibu ya kuwatosa ipo kubwa sana..

hao wote watoto wa arusha ile arusha ndipo wamekulia wote . dar wameletwa na harakati za maisha tu.. ila arusha ndipo watakapozikwa. hawawezi nyimana dili
 
Ahahahhahahhahah mkuu kuwa muwazi kabisa , sababu halisi sio usingizie visivyokuwepo
 
Mtetezi wa Clouds media kwenye ubora wako πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Ukiona watu wote wana mawazo yanafanana ujue kuna tatizo mkuu.
Halafu mimi siyo shabiki ya watu wanaolalamika sana bila kuchukua hatua
 
Mi sjui hata hao weusi wanaimba nini, nyimbo hazieleweki sjui wanaimba ki-lugha khaaa...comment ya ukanda na ukabila ndo inayowabeba weusi kwa kupata show pale clouds hakuna kingine kwa kweli
 
kama ni hivyo mbona Kiba na Mond hawawabebi jamaa zao wa Kigoma? au ndo tuamini maneno ya Msindi Sele?
Hujui kitu wewe nenda pale WCB kahesabau waKigoma ni wangapi??


Unajua huyo Laizer ni wa kigoma na diamond alimuokotea Burundi hana mbele wala nyuma amechoka kachakaa??? Uliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…