Hakuna Taifa lenye Uhuru Kamili wa Kiserikali katika Nchi za Dunia ya Tatu

Hakuna Taifa lenye Uhuru Kamili wa Kiserikali katika Nchi za Dunia ya Tatu

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Uhuru mliopewa na Uhuru wa makaratasi tu, mkubwa akitaka jambo lake analifanya tu.

Sheria za umoja wa mataifa ni kama zipo tu kuzidhibiti Nchi za hali ya chini.

Nchi kama Marekani ina Sera zake kuwa Nchi nyingine kubwa hazitakiwi kutengeza urafiki wa karibu na nchi zilizoko katika ukanda wake. Maana yake ni kuwa nchi zote zinazopaka na Marekani hazitakiwi kukurupuka kwenye kujenga mahusiano na nchi nyingine hususani kwenye rasilimali kama mafuta, bila hisani ya Marekani.

Nchi za Uingereza, Ufaransa na nyingine za Ulaya zina sera hizo hizo kwenye Makoloni yao ya Awali hasa yale yenye rasilimali nyingi.

Urusi nayo ina sera hizo hizo katika nchi jirani hususani zile zilizokuwa kwenye Umoja wa Kisovieti kabla ya kujitenga. Nchi za Ulaya au Marekani hazitakiwi kuwa na urafiki wa karibu hasa kijeshi na nchi hizo zinazopaka na Urusi.

Maana yake ni kuwa Nchi hizi zote uwa zinashikikiwa bila zenyewe kujua na nchi zenye nguvu zaidi duniani, na endapo zitaleta ubishi basi cha mtema kuni watakiona.

Nchi nyingine ni kama Taiwan inavyopelekewa moto na China baada ya kutaka kumkaribisha Mmarekani.

Hii hipo pia kwenye Nchi za Afrika, Mfano Nigeria, Kenya hizi Mmarekani ana mkono wake moja kwa moja. Pia vilevile nchi kama Ufaransa na Uingereza zina Makoloni yao bado zimeyashikilia
 
Mataifa ni machache duniani, yaani US, China, na Russia.
 
Back
Top Bottom