Hakuna taifa linaloweza endelea kwa kuongeza tozo bali kwa kuchochea uzalishaji

Hakuna taifa linaloweza endelea kwa kuongeza tozo bali kwa kuchochea uzalishaji

kalonji

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2021
Posts
6,300
Reaction score
8,152
Hili jambo limetufika wote na linatuathiri sote hawa watu wamedhamiria kutufanya tuzidi kuwa masikini huku wao wakineema.

Dunia nzima Hakuna tozo kama hizi,tupeana maujuzi zaidi jinsi ya kukwepa dhuluma hizi tutumie nini sasa kufikisha pesa tutumie uber, bodaboda, parcel,mtu,konda, haingilii akili tozo za ajabu kabisa hizi,hata Magufuli asingezikubali achilia madhaifu yake zenye lengo la kuwafanya watz wazidi kuwa masikini,hali inajulikana kuna matumizi mabaya Sana ya Kodi pasipo tija kwa mlipa kodi.

Hawa watu waliokosa ubunifu awaelewi kwamba tozo hizi zinakwenda kuuwa ajira na uchumi wa wengi.Mtza anakamuliwa haswaa tozo za simu bei juu,mafuta bei juu,mbolea bei juu yaani wamelenga mle mle panapogusa maisha ya hali ya chini Ili kuwadidimiza.

Hakuna taifa linaloweza endelea kwa kuongeza tozo bali kwa kuchochea uzalishaji Ili export ikue.

Tumetoka kuisoma namba leo tunazikwa kabisa hawana huruma kabisa hawa.
 
Dawa ni kupunguza tu matumizi ili hayo makadirio yao yasitimie. Mimi kwa sasa natumia pikipiki muda wote! Bora niitwe bodaboda. Nikisafiri napanda Shambalai kudadeki!

Miamala nitafanya ile isiyokwepeka tu! Iliyobaki yote, bora nimpe mtu hela kwa mkononi.
 
twenzetu Lushoto😂
 
Njia mojawapo inayoweza kutumika, hasa kwa wale wasio na akaunti za benki, jitihidi kuwajua na kuwapata watu waaminifu wenye akaunti za benki.

Unamwambia unayetaka kumtumia, aende kwa huyo jamaa. Unaweka hela kwa huyo mwenye akaunti ya benki. Unamtumia stakabadhi uliyowekea. Yeye anampa hela uliyetaka kumtumia. Wakati wa kumlipa hela uliyemtumia, anakatwa hela ya kidogo ya usumbufu wa kwenda bank na kutolea kwenye ATM.

Hii sasa itakuwa ni biashara bubu. Hatupendi watu wakwepe kodi lakini dhuluma ikizidi, ni lazima watu watafute njia za kujikwamua ili waendelee kuishi na wafike siku ambayo mambo yatabadilika.
 
wale majiniasi wetu huu ndiyo ulikuwa muda muafaka wa kuja na ubunifu kama suluhu ya kututoa hapa kwa wanyonya damu.
Hapa tatizo sio majiniasi, tatizo ni serikali, majiniasi wameshaleta mobile money, serikali imeleta tozo.

Hata majiniasi walete nini, serikali bado italeta tozo.

Unless tuanze kufanya zile za chini ya kapeti, ambazo mwisho wa siku tutaitwa wahujumu uchumi....

Nadhani ifike kipindi sasa bungeni kusiwe na Posho kabisa..
 
Ulevi wetu wa mitandao utakuponza

Bora tulidi analogia

Ukifika nyumbani kwa mtu unatupia jiwe juu wa bati basi
 
Hapa tatizo sio majiniasi, tatizo ni serikali, majiniasi wameshaleta mobile money, serikali imeleta tozo.

Hata majiniasi walete nini, serikali bado italeta tozo.

Unless tuanze kufanya zile za chini ya kapeti, ambazo mwisho wa siku tutaitwa wahujumu uchumi....

Nadhani ifike kipindi sasa bungeni kusiwe na Posho kabisa..
uko sahihi mkuu, sema ni vile mind zetu zinatamani desperate measures on desparate situations.
 
😂😂😂mkuu unaandika kwa hisia sana.
Siku hizi tumeongezewa Burdani kutoka Dom-Lushoto,very classic mkuu
Ngoja basi nijaribu kuitumia hiyo Burdan kubebea machungwa ya pale Segera na Mkata, na yale maembe vilinge ya Msambiazi ili nikawauzie Wagogo.
 
Mwigulu ni mbaya sana!! Yaani siku hizi naonekana kama boda boda vile! Gari kitambo nimepaki tu! Yaani mimi ndiyo wa kupanda Shambalai na Vuga line kweli!!!
Mungu na amlaani kabisa anapiga bajeti utadhani watz wote wanalingana nae maisha.
Ye vocha ya laki kwa siku anamudu hali wengi sh 500 ni bajeti ya familia kwa siku.
 
Nimejaribu jana kutuma kwa bodaboda ila nilimwambia ukweli kuwa hii bahasha ina hela na slip fulani ya bank, sema roho inakuwa juu kidogo!
Hivi ni kiasi gani unaona sasa hapa nikimpa apeleke ataweza kutokomea?
Haya mambo haya!?
 
Back
Top Bottom