Hakuna tena cha kuikoa Ukraine. Hata Marekani wameshajua ndio maana wanawapa misaada hewa

Hakuna tena cha kuikoa Ukraine. Hata Marekani wameshajua ndio maana wanawapa misaada hewa

Urusi anapukutishwa mdogo mdogo,

Subirini muone watu wana mahesabu ya mbali siyo ya karibu kama haya yenu ya ki ccm
Hizo hesabu za mbali zingekuwa na maana kama watu wa Ukraine hawafi maelf na maelf pia kama maeneo yangekuwa hayachukuliwi.
But Ukraine wanakufa kama kuku na maeneo yanaendelea kuchukuliwa.
 
Hizo hesabu za mbali zingekuwa na maana kama watu wa Ukraine hawafi maelf na maelf pia kama maeneo yangekuwa hayachukuliwi.
But Ukraine wanakufa kama kuku na maeneo yanaendelea kuchukuliwa.
Halafu tunatakiwa kuelewa kuwa maeneo ya Mashariki ya Ukraine ambayo yametekwa na Urusi ndio yenye uzalishaji mkubwa kwenye kilimo na viwanda. Kwa hiyo Urusi atayatumia maeneo hayo kujijenga kiuchumi.
 
Hata Urusi mwanzoni mwa vita alipata tatizo hilo la watu kukimbilia nje ya nchi kwa kuhofia kupelekwa mstari wa mbele wa vita. Viongozi wa Urusi waliling'amua hilo haraka na kuanza mikakati ya kuwaongezea maokoto na incentives nyingi wapiganaji. Zaidi, lilipotokea tukio la kuuliwa watu na kulipuliwa ukumbi wa starehe Jijini Moscow watu waliona unyama uliofanywa na walipuaji na ikawatia motisha wa kwenda kulipiza kisasi kwa kujiunga na Jeshi la nchi hiyo. Hasa kutokana na imani kuwa walipuaji walipewa fedha na Ukraine ili watekeleze shambulio lile.
Ukraine tatizo hakuna watu wa kutosha kuwavutia waingie jeshini.Wamebaki watoto wadogo na wazee kwa asilimia kubwa.
Labda waanze kutumia mamluki kutoka Afrika
 
Nilianzisha uzi kuhusu Urusi naona nimepigwa ban ya kuanzisha
Uzi😀
Hivi kuna mtu anasomaga thread zako? Maana mi najua una Id Kama mia hivi! Ukianzisha uzi unajijibu mwenyewe 😂😂
 
Tatizo kubwa linaloikabili Ukraine kwa sasa ni kukosekana kwa nguvu kazi ya kuendeleza vita. Hilo linafuatiwa na upungufu mkubwa wa silaha.

Pamoja na kuzuiwa watu wenye umri wa miaka 18-60 kutoka nje ya nchi lakini zaidi ya watu milioni 4 wamekimbia nchi kwa kuvuka mto.

Ukraine imejaribu kubadili sheria ili walioko nje warudi nchini kwa lazima wapate kusajiliwa jeshini,kwa mfano kila mwenye paspoti ya Ukraine haruhusiwi kuibadilisha kwenye balozi za nchi hiyo za nchi waliko,ni lazima warudi nchini.

Kwa kujua madhumuni ya sheria hiyo walio nje wanajibu jeruri kusema hawaoni sababu ya kurudi huko,ni bora kuchukua uraia wa nchi nyengine kuliko kurudi nchini ambako hakuna matumaini ya kushinda vita.

Hali inayoikabili Ukraine haihitaji nyongeza ya silaha wala fedha,muhimu ni askari wa kutumia hizo zana ambazo nazo kila nchi kati ya marafiki wa Ukraine ameshachangia na kukata tamaa.

Marekani imeidhinisha kiasi kikubwa cha fedha kwa Ukraine,takribani dola bilioni 62.Hata hivyo msaad huo ni wa kijanja na kiasia kwani hautotolewa papo kwa papo na wala hautoshikwa mkononi mwa Ukraine mpaka muda mrefu upite huku Urusi ikizidi kusonga mbele kuelekea Kyiv au pale watakapoamua kusimama.
Msaada iliyotoa Marekani ni mdogo kuliko iliyokwishokutolewa huko nyuma na ambayo haikuleta tija yoyote.

Msaadu uliotolewa safari hii utakuwa ni kwa awamu kwa kutoa fedha hizo kwenye makampuni ya utengenezaji silaha ya ndani ya Marekani ili watengeneze silaha zitakazofidia kurudisha silaha zilizotolewa kwenye maghala kuipatia Ukraine.

Silaha kama hizo kutoka kwenye maghala muda mwengine zinakuwa zimepitwa na wakati na zikiingia uwanja wa mapambano huwa hazifanyi kazi kisawasawa.Hilo limetokea mara nyingi kwa silaha kutoka Ujerumani na nchi nyengine za jumuiya ya NATO ambapo Ukraine imekuwa badala ya kutoa shukran kwa misaada hiyo imewatolea kashfa waliowapatia silaha hizo kwa kutangaza hadharani kuwa ni mbovu.

Ukipenda unaweza kuongeza maarifa kuhusu tatizo la Ukraine hapo chini.

‘Why should I return to fight?’ Ukrainian men living abroad say

Wale waliokuwa wanaikashfu Russia wapo wapi humu JF. Unasikia Super power anachakazwa na kanch kadogo Ukrain. Kipo wapi sasa.
 
Vita vilipoanza watu wa Ukraine vijana kwa watoto,wake kwa waume walifanya hashuo wakajipanga foleni kutaka kwenda mstari wa mbele wakapigane na mrusi.Leo imekuwa ni wa kukimbizwa na kujificha
Ngoja nije na mchoro wake utapendeza.
wanawakimbia ila kwa miaka 3 mnateka vijiji vitatu , hata kama hatuna shule ila chagueni njia za kutudanganya
 
Hizo hesabu za mbali zingekuwa na maana kama watu wa Ukraine hawafi maelf na maelf pia kama maeneo yangekuwa hayachukuliwi.
But Ukraine wanakufa kama kuku na maeneo yanaendelea kuchukuliwa.
vita ipi watu hawafi?
 
Kama ni kushindwa NATO wangenyosha mikono mapema, kitendo cha Ukraine kushindwa vita mbele ya support ya NATO kitapelekea washirika wengi wa USA kuhamia upande wa Russia, ndo maana unaona NATO bado anasapoti vita hivyo mdogo mdogo, anajua tu pumzi ya uchumi itaisha na itamchukua muda mrefu kuinunua tena kiuchumi , kwa upande wa Russia taarifa za vita hazipatikani, ila baada ya muda itakuja kusikia uchumi wa Russia umeporomoka kwa kasi ya 4G
Wakati mrusi anaombea vita isiishe, aendelee kukuza uchumi wake
 
Urusi anapukutishwa mdogo mdogo,

Subirini muone watu wana mahesabu ya mbali siyo ya karibu kama haya yenu ya ki ccm
Nyie ndiyo mlisema mrusi hana uchumi wa kupigana zaidi ya miezi mitatu naona sasa hivi mnabadirisha magoli tu
 
Nyie ndiyo mlisema mrusi hana uchumi wa kupigana zaidi ya miezi mitatu naona sasa hivi mnabadirisha magoli tu
Uchumi wa Urusi umebaki imara baada ya kukamata viwanda vyote vikubwa vya Ukraine.Ana maligahafi nyingi za chuma kutengeneza silaha mpya fursa ambayo mataifa ya NATO imeondoka.
 
Back
Top Bottom