Hakuna tena Mahubiri ya habari njema, kuacha dhambi, msisitizo ni matoleo

Kwani RC hawana mahubiri ya sadaka huku kwetu padri ametangaza hataki kuona mtu anatoa chini ya elfu moja hataki chenji kwenye sadaka.
 
Kwani RC hawana mahubiri ya sadaka huku kwetu padri ametangaza hataki kuona mtu anatoa chini ya elfu moja hataki chenji kwenye sadaka.
Kwani RC hawana mahubiri ya sadaka huku kwetu padri ametangaza hataki kuona mtu anatoa chini ya elfu moja hataki chenji kwenye sadaka.
🤣🤣. Ndio Maana nasema siku hizi Makanisani Msisitizo ni SADAKA.
Zamani Msisitizo ilikuwa ni Habari ya Matendo Mema, Kuacha dhambi na kumuabudu Mungu.
 
Toa sadaka mleta mada.
Mbona kuhonga unahonga au kula unakula daily?
Kama hutaki kutoa sadaka basi acha sio kuja kumwaga shombo huku mambo ya kiimani yanaenda kiimani.
 
🤣🤣. Ndio Maana nasema siku hizi Makanisani Msisitizo ni SADAKA.
Zamani Msisitizo ilikuwa ni Habari ya Matendo Mema, Kuacha dhambi na kumuabudu Mungu.
Zamani zipi unazozisema wewe?
Toa sadaka vyote umepewa bure na mwisho wa siku utaviacha hapahapa duniani.
Kiburi na jeuri ya nini?
 
Sadaka ilikuwa zamani tulipoambiwa pesa si msingi wa maendeleo. Sasa hivi pesa ni msingi maedeleo ni matokeo
 
Padri wako nae kapotoka uhusiano wa Mungu na mwanadamu hauwi kwa sala tu bali kwa Matendo mema na kufuata amri zake. Sala hata mganga wa kienyeji ana sali.

Kutoa sadaka kwa wahitaji hata wauaji na wazinzi wanatoa..

Kufunga hata walevi na waasherati wanafunga.

Kinacho matter ni MATENDO yako ndio yataamua mahusiano yako na Mungu
 
Basi wewe uwe padri wangu
 
KIDOGO NAWASIFU RC angalau
Kanisa lote la yesu Kristo limo katika majaribu hata huko Kuna computer kwa ajiri ya kukusanya mapato ole wako ukosekane kwenye hiyo mashine ukristo wako unatiliwa mashaka upendo kusaidia yatima na wajane kuwahurumia wasiokua na kipato SIYO Tena kua ni injiri ni Mambo yaliyopitwa na wakati hayana tija kwa kanisa la .com ni kujenga majengo taasisi na sherehe za kupongeza wandamizi kujenga roho zilizo potea kuhamasisha kupenda majirani nk ni kupoteza muda ukengeufu huu ulifanyika ulaya leo majengo makubwa yamekosa waumini walipo gundua yanayohubiriwa yanalenga kitu hayana faida kwa maisha ya peponi hayamuandai kuingia mbinguni wakapotezea
 
Umesema ukweli Mtupu

Hawana huruma na roho za watu

Sasahivi wanachohubiri na kusisitiza ni MATOLEO TU

Hasa Radio SAFINA Arusha Ndio umekuwa mradi wa kibiashara wanauza mpaka maji, vitambaa eti na Kalamu za Israel.

Hahahaa.... Amakweli wajinga ndio waliwao
 
Umekwisha hubiria wangapi mpaka sasa? Unalalama tu huna cha kufanya. We kahubiri achana na wengine. Kila mtu atatoa hesabu siku ile kivyake.

Maadamu hakuna aliyelazimishwa, na wao ni watu wazima, na hizo pesa hukuwasaidia kuzitafuta, kelele za nini?
 
Rudini ukatoliki ndio dhehebu pekee la Yesu Kristo. hayo mengine ni ubatili na tamaa ya madaraka na fedha.
 
Matayo 24 Kwa maana watatokea makristo na manabii wa uongo
Umetaja verse ya maandiko wakati huko huko kwenye hizo upon faith now mahubiri ni 10mins 50mins ni michango.

Na wanakwambia tutabanana hivyo hivyo lazima utoe vinginevyo mambo hayaendi!.
 
Ukishaona roho ya fedha imeingia Kanisani ujue hapo Roho wa Mungu hayuko!Kanisa linakuwa limebaki ni sawa na pango la Wanyanganyi tu.
 
Mwamposa anaombea watu kwa mafungu ya hela utaskia wenye elfu hamsini wapite mbele, baadae wenye elfu30 mwendo ni huohuo mpaka kufikia wenye elf5 tena anaitamka kiunyonge japo wanaojitokeza ni wengi

Sasa hv vidada ambavyo ndio humuita mwamposa na kumwambia huku kuna muijiza .... Yupo wap ehhhh yani ni siasa tupu vingine vidangaji tu

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
 
Rudini ukatoliki ndio dhehebu pekee la Yesu Kristo. hayo mengine ni ubatili na tamaa ya madaraka na fedha.
Sina hakika yote makanisa ni yale yale, Kama iliumbwa kwa mfano wa MUNGU una utambuzi kasikilize injili.,ndicho kilicho kupeleka kanisani ,mengine waachie!!
 
Naichukia hii safina hatari. Inakula pesa wajinga kupitiliza akiwemo bibi angu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…