Uchaguzi 2020 Hakuna tena namna ya kuizuia CHADEMA kuchukua nchi. Ila wakijirekebisha katika hili, watadumu kwenye siasa nchi kwa miaka mingi zaidi

Utaratibu wa kura za maoni CDM inabidi uangaliwe upya. Kuna majimbo huoni logic ya kuwaweka wagombea waliosimamishwa, zaidi sana ni ulafi tu na mwisho wa siku watu wa eneo husika watakiona chama kina agenda zake za siri. Watakikinai chama kwa mambo yao yakipuuzi.
 

..kamati kuu ikiwa inaingilia kura za maoni ndipo unapopatikana mwanya wa kuwaletea wananchi wagombea wa hovyo.
 
Sikupingi mkuu uko sahihi

Hoja hapa ni kwamba, kweli huyo aliyesimamishwa kwenye hilo jimbo kupambana na CCM wamezingatia nini considering the majority of voters wa jimbo husika?
 
Sikupingi mkuu uko sahihi

Hoja hapa ni kwamba, kweli huyo aliyesimamishwa kwenye hilo jimbo kupambana na CCM wamezingatia nini considering the majority of voters wa jimbo husika?

..inabidi ufunguke zaidi.

..au unamaanisha walioteuliwa huko siyo wa makabila ya maeneo hayo?

..kuna wanaounga mkono kuteua wagombea ambao ni wa kabila la jimbo husika.

..halafu wapo wengine wanasema jambo la msingi ni kuteua mkaazi wa eneo hilo, mtu ambaye anajulikana na wapigakura.

..mimi nakubaliana na wanaosema kigezo kiwe ni ukaazi, na siyo kabila. kwa mfano, ccm imekuwa ikiteua Waarabu na Wahindi na wanawashinda wenyeji wa maeneo husika.
 
There is nothing personal kwenye hii hoja, yako majimbo mengi yalipatwa na hili jambo. Kuna ukaazi na ukabila, kuangalia ukabila kama kigezo sio sahihi kwa nchi yetu. Lakini kwa kutumia kigezo cha ukaazi CDM imeamua kujijengea taswira ya kikabila kwenye baadhi ya majimbo hapa nchini, litawasumbua mbeleni.
 
Chadema haitakufa ccm itakufa muda sio mrefu lakini CDM itakuwepo kwa miaka mingi ijayo.
 
Mpaka sasa hujui kama ccm imevunjika ila wengi wao humo ndani wanaishi kwa hofu?
 

..unafahamu kwamba Prof.Safari, makamu mwenyekiti wa cdm mstaafu; Dr.Mashinji katibu mkuu; John Mnyika Naibu Katibu Mkuu; Pertobas Katambi Mwenyekiti umoja wa vijana, wote ni Wasukuma? Lakini ccm waliendeleza propaganda kwamba cdm ni chama cha kaskazini.

..Siyo kama naikataa hoja yako moja kwa moja. Kuna ukweli fulani kuhusu unachokisema.
 
Unaiamini TUME kwamba itaipa upinzani nchi ?
Kwanini wasitoe nchi?Kina Nyerere waliwalazimisha kina governor Edward Twining kuitoa nchi tena kwa maneno tu Kama wanavyofanya Chadema.Una habari Tanganyika hatujapigana Vita na mwingereza ili Kupata Uhuru?
 
Mkuu naelewa propaganda ya CCM. Ila hoja hapa ni hili swala la ukabila inadhihirishwa sasa rasmi na CDM yenyewe katika ngazi ya majimbo. CCM wakiitumia hii propaganda kwa wakati huu ambapo ipo wazi wazi kabisa huko majimboni, hakuna mtu ndani ya CDM atakayeinuka kutoa utetezi wa maan.
 

..I see your point.

..lakini hakuna chama ambacho ni immune from propaganda.
 
CCM yenye dola haivunjiki, trust me. Dola hutumika kumaliza matatizo ya chama.
 
Ole Gunnar Out! He must go. Samahani lakini
 
Hiyo ibada haimusaidii kitu Lisu alitakiwa aende na mlurheri mbowe kwa sababu yeye katoliki
 


Kwanza, hakuna chama kinachochukuwa nchi. Chama kinashinda kura na kutengeneza serkali. Kuchukuwa ni sawa na kupinduwa. Pili, mpaka sasa hakuna anayeweza kuongelea mafaninkio. Mfafanikio yatapimwa kwa ushindi wa uraisi, ubunge, na udiwani. sasa hayo mafanikio ya CHADEMA unayoyaongelea sasa hivi ni yepi? Ngonja baada ya Oktoba 28 ndiyo tutaweza kuona mafanikio ya CHADEMA, CCM, etc, Ukwel ni kuwa hata CHADEMA ispopata uraisi mafanikio yake yatapimwa na nafasi watakazopata za ubunge na udiwani. Kwa upande wangu mafanikio yatakuwepo kama CHADEMA itatetea nafasi zake za ubunge/udiwani. Kama wataweza kupata madiwani na wabunge idadi ileile au zaidi mimi najuwa wamefanikiwa. Maana kuminywa kwa uhuru wa vyama kufanya siasa kumeathiri vyama vya siasa vya upinzani kukuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…