Wasalaam wanaJF,
Leo ni siku ya Jumapili, naamini watu wengi mko katika mapumziko ya wiki. Huu ni muda muafaka katika wiki ambao tunaweza kuutumia kujadili mambo ya kisiasa yaliyotokea na yanayotokea nchini kwetu katika kipindi hiki cha uchaguzi.
Mosi, kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu CHADEMA imefikia maturity stage katika siasa za Tanzania, kimeanza kuingia katika saturation stage kwa speed ya hali ya juu (mafanikio makubwa kwa chama cha siasa). Hiki chama kinazidi kuwa kama IMANI kwa watu wazima na hata watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa kupiga kura. Hili ni tishio kwa chama tawala kwakuwa kizazi kimoja mbele CHADEMA itakuwa na mtaji mkubwa sana wa supporters wanaokulia katika harakati zake za kipindi hiki.
Jambo la muhimu leo ni kuwajulisha viongozi na watu wote wenye mtazamo wa mbali wanaopenda sera za chama hiki umuhimu wakuweka utaifa mbele katika maeneo yote ya nchi yetu.
Kuna majimbo ya mfano ambayo CHADEMA wameweka wagombea yenye tafsiri ya kwamba chama kina wenyewe na hakina nia ya dhati kuwaongoza watanzania kwa miaka mingi ijayo. Majimbo hayo ya mfano ni NGORONGORO, MONDULI na MOROGORO MJINI.
Hakika leo watanzania watawaunga mkono kwasababu tu wanataka kuitoa CCM madarakani, hivyo hawana budi kuyafumbia macho hichi mnacho kifanya kwenye majimbo ya watu wengine.
Ila mkae mkijua ya kwamba msipo ondoa hii tabia chafu na ya kilafi katika chama, mkaamua kutoheshimu maeneo yote kwamba yana watu wenye uwezo na ustadi wa kujiongoza wenyewe basi mjiandae na vita itakayokuwa mbele yenu baada ya kuiondoa CCM madarakani.
Narudia, CHADEMA isipoacha tabia hii chafu na ya kilafi, it will have no longevity in Tanzanian politics.
Jumapili njema.