Uchaguzi 2020 Hakuna tena namna ya kuizuia CHADEMA kuchukua nchi. Ila wakijirekebisha katika hili, watadumu kwenye siasa nchi kwa miaka mingi zaidi

Uchaguzi 2020 Hakuna tena namna ya kuizuia CHADEMA kuchukua nchi. Ila wakijirekebisha katika hili, watadumu kwenye siasa nchi kwa miaka mingi zaidi

mbugabire

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2012
Posts
261
Reaction score
87
Wasalaam wanaJF,

Leo ni siku ya Jumapili, naamini watu wengi mko katika mapumziko ya wiki. Huu ni muda muafaka katika wiki ambao tunaweza kuutumia kujadili mambo ya kisiasa yaliyotokea na yanayotokea nchini kwetu katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Mosi, kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu CHADEMA imefikia maturity stage katika siasa za Tanzania, kimeanza kuingia katika saturation stage kwa speed ya hali ya juu (mafanikio makubwa kwa chama cha siasa). Hiki chama kinazidi kuwa kama IMANI kwa watu wazima na hata watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa kupiga kura. Hili ni tishio kwa chama tawala kwakuwa kizazi kimoja mbele CHADEMA itakuwa na mtaji mkubwa sana wa supporters wanaokulia katika harakati zake za kipindi hiki.

Jambo la muhimu leo ni kuwajulisha viongozi na watu wote wenye mtazamo wa mbali wanaopenda sera za chama hiki umuhimu wakuweka utaifa mbele katika maeneo yote ya nchi yetu.

Kuna majimbo ya mfano ambayo CHADEMA wameweka wagombea yenye tafsiri ya kwamba chama kina wenyewe na hakina nia ya dhati kuwaongoza watanzania kwa miaka mingi ijayo. Majimbo hayo ya mfano ni NGORONGORO, MONDULI na MOROGORO MJINI.

Hakika leo watanzania watawaunga mkono kwasababu tu wanataka kuitoa CCM madarakani, hivyo hawana budi kuyafumbia macho hichi mnacho kifanya kwenye majimbo ya watu wengine.

Ila mkae mkijua ya kwamba msipo ondoa hii tabia chafu na ya kilafi katika chama, mkaamua kutoheshimu maeneo yote kwamba yana watu wenye uwezo na ustadi wa kujiongoza wenyewe basi mjiandae na vita itakayokuwa mbele yenu baada ya kuiondoa CCM madarakani.

Narudia, CHADEMA isipoacha tabia hii chafu na ya kilafi, it will have no longevity in Tanzanian politics.

Jumapili njema.
 
Mambo mengine ni magumu kwasababu ya culture na mazoea ya Watanzania .Hivi vyama vinatokana na Watu
 
Unaiamini TUME kwamba itaipa upinzani nchi ?

Anyway Struggle is the Duty...., hata kama mtu unajua matokeo hauna budi kuendelea kupambania Haki, Usawa na kile unachokiamini...., Death ya CCM itatokea pale tu CCM itakapovunjika vunjika..., bila ya hivyo hakuna level playing field.....
 
Ila mkae mkijua ya kwamba msipo ondoa hii tabia chafu na ya kilafi katika chama, mkaamua kutoheshimu maeneo yote kwamba yana watu wenye uwezo na ustadi wa kujiongoza wenyewe basi mjiandae na vita itakayokuwa mbele yenu baada ya uchaguzi.
Funguka mkuu hapa ni jamiiforums usiwe na uwoga.

Kwenye chama chetu CHAUMA tunamheshimu kila mtu na tunathimini uwezo wake. Karibu Sana ujiunge nasi.
 
Nimefumguka vya kutosha mkuu, majimbo yana wenyewe na sio pipi kwamba wanajigawia wanavyotaka

Hilo kwa chadema huwa hawajali. Wakifikia muafaka utasikia Jimbo fulani apewe ACT kirahisi kabisa.

Njoo chauma huku bado tunatafuta wagombea
 
Hiyo saccos, imeanza kuzama kamanda. Tegemea mpasuko mkubwa, baada ya uchaguzi huu. Lissu hawezi kaa chini ya Mbowe, kila kitu kiwe cha Mbowe huku chama kikidhalilika. Akijaribu kumendea ile keki ya mwenyekiti, Mbowe atamfurusha mchana kweupe. Mbowe bonge la dikteta mule saccos, wote hamkohoi kule ila mkitoka nje hilo povu mtoalo hakina mfano. Kajipangeni upya 2040..
 
Unaiamini TUME kwamba itaipa upinzani nchi ?

Anyway Struggle is the Duty...., hata kama mtu unajua matokeo hauna budi kuendelea kupambania Haki, Usawa na kile unachokiamini...., Death ya CCM itatokea pale tu CCM itakapovunjika vunjika..., bila ya hivyo hakuna level playing field.....
Kifo cha CCM kipo hapa 👇
5842DDE3-884C-402C-96D4-FF468473F069.jpeg
 
Unaiamini TUME kwamba itaipa upinzani nchi ?

Anyway Struggle is the Duty...., hata kama mtu unajua matokeo hauna budi kuendelea kupambania Haki, Usawa na kile unachokiamini...., Death ya CCM itatokea pale tu CCM itakapovunjika vunjika..., bila ya hivyo hakuna level playing field.....
Wananchi ndo wanaamua. Kazi ya tume ni kutangaza tuu
 
Nimefumguka vya kutosha mkuu, majimbo yana wenyewe na sio pipi kwamba wanajigawia wanavyotaka

..kwa uelewa wangu Uteuzi wa wagombea ubunge wa CDM umefuata kura za maoni toka majimboni kwa asilimia 99%.

..Ni jimbo moja tu la Segerea ndiyo kamati kuu ya CDM haijamteua mshindi wa kwanza ktk kura za maoni.

..Jiungeni na CDM mjenge chama, mjulikane na muaminike na wenzenu, na chama kitawateua kwa nafasi za uwakilishi.

NB:

..kwa jimbo la Monduli hivi mumeridhika na Fred Lowassa?

..Mmeridhika na jinsi Fred alivyopwaya jukwaani, na asivyoweza kujieleza?
 
Unadhani huyo mgombea wa CDM wa sasa ataweza kumshinda Fred Lowassa? CDM mmewapa wanaMonduli chaguo la dhihaka kwao hivyo hawana budi kumchagua Fred
 
Kwa sasa uchaguzi ni kati ya chadema na ccm.wengine wasindikizaji tu..
 
Unadhani huyo mgombea wa CDM wa sasa ataweza kumshinda Fred Lowassa? CDM mmewapa wanaMonduli chaguo la dhihaka kwao hivyo hawana budi kumchagua Fred

..Inabidi uwalaumu wana-cdm wa jimbo la monduli.

..kamati kuu imepitisha mgombea waliyeletewa na wanachama walioko monduli.

NB:

..Fred hawezi hata kuomba kura. Hawezi kabisa.

..waziri mkuu alikwenda kumuombea kura na alifedheheshwa sana performance ya Fred jukwaani.

..sasa kama Fred anaweza kushinda kwa uombaji kura niliouona basi kuna tatizo kubwa huko Monduli.

..msikilize Fred Lowassa hapa.

Back
Top Bottom