Hakuna tena ndoa za "vijana" now days


kuna sababu gani ya kuoa kama kila kitu unachokihitaji kwenye ndoa unakipata kabala ya kuoa????? u want 2 leave out of stress... stop marrying now!
 

Unajua watu tunafanya vitu kwa mazoea bila kutafakari. Pia tunachanganya mambo. Kuna uchumba na ndoa. Uchumba ni wakati ambapo watu wawili wana negotiate, na kufanya mazungumzo ili wakikubaliana waingie kwenye ndoa. Mazungumzo hayo hu usisha wazazi wa pande zote na ndugu wengine. Kumbuka hapa wanandoa watarajiwa wanakuwa hawajakutana kimwili. Mfumo huu ulikuwepo zamani, leo hii hili halifanyiki. Badala yake watu wanaingia kwenye ndoa bila kupitia uchumba. Mnapoanza kufanya ngono, tayari unakua umeingia kwenye ndoa. Ninachopinga ni mtazamo kuwa ndoa huanza baada ya kwenda kanisani, msikitini au kwa mkuu wa wilaya. Kwa tafasiri hiyo ndoa siku hizi huanza mapema zaidi.
 
kuna sababu gani ya kuoa kama kila kitu unachokihitaji kwenye ndoa unakipata kabala ya kuoa????? u want 2 leave out of stress... stop marrying now!
Je hili unalosema lina uhusiano wowote na kushuka kwa maadili kunakosemwa?
 
Mkuu unachokisema wewe nadhani ndio moja ya sababu kwanini watu wanachelewa kufunga ndoa au kanisani au msikitini or whatever....
Lakini kwanini basi hiyo negotiation ichukue muda mrefu hivyo hadi ku involve kujamiiana? je vijana wa sasa hawataki "kuuziwa mbuzi kwenye gunia" hadi wawe "matomaso"
 
ina ukweli huu, mie nilifunga ndoa baada ya miaka mitano ya kufahamiana, namjua ananijua, mikikimikiki tunaihimili vyema...... Ila wanandoa wakumbuke kumtanguliza Mungu kwenye ndoa yao ndipo watakapofanikiwa....
 
ina ukweli huu, mie nilifunga ndoa baada ya miaka mitano ya kufahamiana, namjua ananijua, mikikimikiki tunaihimili vyema...... Ila wanandoa wakumbuke kumtanguliza Mungu kwenye ndoa yao ndipo watakapofanikiwa....
Ushauri mzuri...........
Lakini najiuliza mwaka wa kwanza wapili mimba, wanne,watano nakuendelea...... muda wote huo huwa mnaongea nini kuhusu kufunga ndoa? au mnakwenda kimya kimya?
 
ABC Report Why Successfull Black Women Find It So Hard To get Married - YouTube
Tatizo la dada zetu wamekua wakijaribu kuishi maisha ya western ambayo haya owani na maisha halisi ya Mtazania wa kawaida nitatowa mfano unamkuta sister amesoma vizuri amebahatika kazi nzuri inapokuja kuwa na mpenzi hilo ndio tatizo wanamambo mengi ndani ya akili zao pia wanasahau kuwa Tanzania kuna wanawke wengi tena wazuri sana sana ,inapokuja kwa mwanamume nitafauti you can be 49 na utaowa msichana 25 kwa mwamke hilo halipo .
 

Inategemea definition yako ya "ndoa" ni ipi. Kwa wengine kukaa kinyumba ni "common law marriage" tayari na inatambulika hata kisheria.

Kwa hiyo, kwa definition ya "common law marriage" hawa wanaokaa pamoja kwa miaka kadhaa, pengine na kuzaa watoto, walishaoana tayari wenyewe, hicho kinachofuatia unachoita "ndoa" ni sherehe tu.

Tunatakiwa kuangalia kwa undani maana ya ndoa, sio kuangalia superficialities kama sherehe / oficial ceremonies na kuziita ceremonies hizi "ndoa".

Mtu anaweza kuwa na sherehe ya ndoa bila ya kuwa na ndoa, na kuwa na ndoa bila ya kuwa na sherehe ya ndoa.

Inawezekana this is not so much that ndoa zinapungua, bali mtazamo wetu kuhusu ndoa unabadilika. Badala ya watu kuwa na courtship, watu wengi wanaamua kukaa pamoja kwanza (common law marriage) na hata kuzaa kabla ya kufanya formal marriage ceremony.

Wwengine wanairuka kabisa formal marriage ceremony. Mtu anapigwa intro tu kwenye familia. These are changing times.
 
Watu wanachagua sana na wanaangalia vigezo vingi kabla hawajao/kuolewa.
 
mkuu natambua sana unayoyasema yapo, lakini in general bongo ndoa ambazo watu wanapenda kujivunia ni zile rasmi za akanisani, shekh au mkuu wa wilaya
Mimi naangalia zaidi hizi ndoa "rasmi" kwanini zamani haikuwa hivi sana? yaani sasa hivi watu wanokimbilia uzeeni ndio utawakuta kwenye kumbi mbalimbali za sherehe za harusi kama maharusi
 

Ndoa ikishatambulika na wawili na kisheria ni "rasmi" tayari. Huna haki ya kusema walioamua kukaa katika "common law marriage" hawana ndoa rasmi. Hii ni stigma inayotokana na tradition tu na inafaa kuachwa.

Na kuna watu kibao wanajivunia kuwa katika "common law marriage", kwao wanaona kwamba kuamua wao wenyewe kuwa pamoja bila ya kufungwa na kanisa au serikali kunaonyesha kwamba wametaka kuwa pamoja kikweli na hawajalazimika kuwa hivyo kwa sababu ya tradition.

Kwa hiyo there is a case to be made here kwamba wale unaosema hawana sababu kubwa sana za kujivunia "ndoa" zao (common law marriage) actually ndio wenye sababu kubwa sana ya kujivunia ndoa zao. Hawajamchangisha mtu mchango wa harusi na kufanya harusi ya gharama na hivyo kuhofia kuwa disappoint watu wakiachana, lakini hawaamui kuachana.

Kiujumla, watu wanaangalia traditions nyingi wanakuta ziko overrated. Kwa mfano ndoa, kitu ambacho kimsingi ni makubaliano ya watu wawili, imeenda kufanywa kuwa a pompous circus yenye migharama ya ajabu na spectacle ya kushangaza. Kuna wengine wanaona bughudha hii ya nini wakati mambo ni ya wawili? Ndiyo maana unaona common law marriage zinazidi.

Zamani harusi watu wakipika wenyewe, kinamama kuchambua mchele etc. Siku hizi mpaka matarumbeta, catering services sijui, suti za Savile Row na habari za kushindana misafara. Wengine wanaona hatuwezi haya, bora tufanye kivyetuvyetu.

Kwangu mie bora mapenzi. Kati ya ndoa unazoziita "rasmi" kuna nyingi tu zina matatizo mengi na kati ya hizo unazoziona si "rasmi" kuna nyingi tu za mapenzi ya kweli.

Tukiacha ubaguzi wa ndoa "rasmi" na zisizo "rasmi" tukatambua zote kama ndoa, na kuelekeza juhudi kwenye kuongeza mapenzi ya kweli, tutakuwa tunafanya la maana zaidi.

Na hesabu zetu za ndoa pengine hazitaona mabadiliko uliyoyaona.
 
Utafiti wako sio mzuri kabisa,watu waliooa kati ya miaka 20-25 ukiangalia wengi wamesaidiwa na wazazi wao na kweli kijana wa miaka 20 si atakua anasoma?? Unaanza shule miaka 7 form one miaka 14,form five 18,mwaka wa kwanza miaka 20 mpaka unamaliza chuo una miaka 24 mpaka 28(kwa kozi ya miaka 3 mpaka 7) kupata kazi miaka 29 kujipanga mwaka m1 30 sasa ukiooa na miaka 20 unamaanisha unaooa wkt upo sekondari?? Au Zamani unayozungumzia vijana walikua hawaendi shule? Umri mzuri kuooa kwa sasa kuanzia 28--35 ni reasonable kuooa!!
 

Labda zamani watu walikuwa wanaishia darasa la saba na kuoa, siku hizi wanasoma zaidi. Na hata wasiposoma maisha magumu inabidi kuwe na kipindi cha kujiandaa kama ulivyosema.

Haya nayo yanaweza kuchangia.
 
ina ukweli huu, mie nilifunga ndoa baada ya miaka mitano ya kufahamiana, namjua ananijua, mikikimikiki tunaihimili vyema...... Ila wanandoa wakumbuke kumtanguliza Mungu kwenye ndoa yao ndipo watakapofanikiwa....

mlipeana ile kitu kabla ya kwenda kanisani.? Au na nyie mliuziana mbuzi kwenye gunia?
 

Umedadavua vizuri. Actualy stigma hii inawaathiri sana kina dada. Wengine hata hukosa haki zao, eti kisa hawakufunga ndoa inauma sana.
 

Ujana wa JK katika siasa unahusikaje na Ujana katika Ndoa?
 
Naungana na wewe mtoa mada hii usiful sread yako na mie nimeshaona kwa asilimia 80 kama sio 90
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…