Hakuna tofauti kati ya biashara na ajira



Hayo maneno yanaweza kukufumbua macho
 
 
Nafhani jamaa anazungumzia chances za kutoboa kufikia hiyo level ya Metl ni ndogo sana kuliko muajiriwa kula maisha...

Msoto wa kusimamisha biashara sio wa kitoto
 
Nitatofautiana na wewe kwenye maana ya mfanyabiashara. Naona wewe unachanganya maana ya mfanyabiashara na mifumo ya kufanyia baishara.

Mfanyabiashara, huyu ni mtu yeyote anayefanya biashara halali. Biashara ni kitendo cha mtu au watu ktk mfumo wa kibiashara waliouchagua, kuuza huduma au bidhaa kwa nia ya kupata fedha. Biashara inaweza kuwa for profit or for charitable cause. Inaweza kumilikiwa na serikali au watu binafsi.

Now...mifumo ya kufanya biashara ni ipi kwa hapa Tz?
1. Sole proprietor..huyu ni mfanyabiashra binafsi, yaani mtu mmoja anaamua kufungua business yeye kama yeye, na anaimiliki yeye mwenyewe. Eg mangi kafungua kiosk chake mtaani, au mtu kaweka kibanda cha Mpesa, Au kanunua daladala 10 kazisajili kwa jina lake zinapiga mzigo daily. In short ni biashara yoyote ile halali, ila inamilikiwa na mtu binafsi, individually.
Disadvantage ya mfumo huu wa kibiashara ni kuwa mmiliki akifa na biashara inasimama maana owner hayupo, na itakuwa sehemu ya mirathi yake itakayogawiwa kwa wanafaika wa mirathi hiyo.

Pia mfumo huu hauna kikomo cha uwajibikaji kama ilivyo kwa makampuni...lolote likitokea utashitakiwa mmiliki personally.

2. Ubia/partnership
Wabia, na watu kuanzia wawili na kuendelea ambao wameamua kushirikiana kubiashara, wakigawana faida na hasara. Wanaweza kusajili jina lao la kibiashara. Usually huwa mnatengeneza mkataba wenu wa ubia(parnership deed, ikielezea taratibu za ubia huo)
Mfumo huu pia hauno ukomo wa uwajibikaji(limited liability), mnaweza kushitakiwa wabia wote hata kama ni partner mmoja ndiye kazingua huko nje. Au mdai anaweza kumchagua partner anyeonekana ana ukwasi ndiyo akamshitaki, Na mali zenu binafsi zinaweza kutumika kufidia madeni ya ubia wenu.

Ubia unaweza kuisha pale ambapo mbia mmoja akifariki, au kwa makubaliano ya wabia wote, au kwa amri ya mahakama, au kusudio la ubia likiisha, mfano wapo wanoingia kwenye ubia kukamilisha project fulani, hiyo project ikiisha na ubia umeisha.

Kodi hulipwa na kila mbia personally kwa kila pato apatalo katika ubia huo.

3. Kampuni.
Kisheria zetu, kampuni ikishasajiliwa ni mtu kabisa(artificial person) anayemiliki mali zake, anaajiri wafanyakazi, anaweza kushitaki au kushitakiwa n.k ila nyuma ya mtu huyo, yaani kampuni wamejificha watu waitwao wanahisa.

Mfumo huu wa biashara una ukomo wa uwajibikaji, yaani limited liability. Ikiwa na maana ya kuwa mashitaka yanayoihusu kampuni yataihusu kampuni pekee na si wanahisa, mali binafsi za wanahisa hazitatumika kwenye kulipa madeni ya kampuni.

Isipokuwa mwanahisa atawajibika kwa kiwango cha hisa zake ktk kampuni ambazo alikuwa hajazilipia. Eg kama mwanahisa alikuwa na hisa 50, na amelipia 30 walipofanya kitu kiitwacho kitaalamu "call of shares", basi ikitokea kampuni inawajibika au inavunjwa basi mwanahisa huyo atalipa thamani ya hisa zake 20 tu ambazo alikuwa hajazilipia na si zaidi ya hapo.

Ni katika mazingira machache sana ambako wanahisa wenyewe wanaweza kushitakiwa personally, hii kitaalamu tunaita "...lifting of the veil of incorporation"

Kodi hulipwa na kampuni lenyewe likitengeneza faida, na pia gawio la wanahisa (dividend) nalo hukatwa kodi. Kampuni linaweza kurithishwa vizazi na vizazi.

Kampuni linaweza kuwa la umma, yaani public limited company, haya ni makampuni ambayo yanauza hisa kwa wananchi kwenye soko la hisa la Dar, DSE. Mfano CRDB na Vodacom. Kampuni linaweza kuwa private, yaani linamilikiwa na watu wanaoanzia wawili lakini hawazidi 50. Kampuni linaweza kuwa la charity, not for profit, limited by guarantee.

Lastly, ipo mifumo mingi ya ku earn money, unaweza kuajiriwa na wamiliki wa biashara kwenye mifumo niliyoitaja hapo juu. Unaweza kumiliki biashara kama sole proprietor, au ukaingia kwenye ubia na mtu/watu. Unaweza kumiliki kampuni ambao ni mfumo bora kabisa kuliko hiyo ya mwanzo miwili. Lakini yote kwa yote, unaweza kuwa Investor ktk makampuni yanayouza hisa.
 
Mkuu umeandika vizuri sana tena na mifano hai lukuki. Ubarikiwe.
 
Kumbuka hakuna ajira anayorithishwa mtoto ila mzazi ukiparangana ukafika kiwango fulani ukawa namtoto mjanja anaendeleza ndo unawapata akina MO leo sio kwamba alianza zero akawa alipo bali kuna mtu alianza yy akaendeleza na atarithisha je ww unarithisha nafasi ya ukurugenzi?

Au tuseme umefikia nafasi fulani bado kidogo uwe mkurugenzi je utarithisha hiyo nafasi na mtoto aanzie hapo? Tofauti ni kubwa mno mkuu tuache utani ila kama hauko interested usishawishi na wengine.
 
We jamaa kuna sehemu utakua umekopi.

Mimi mwaka 2017 kwa mara ya kwanza nilisafiri Dar kwenda Songea,baada ya kukaa siku 3 ndo nikawaona wale dagaa nyasa nikawapenda nikajaribu kuleta Dar kuuza aisee biashara ina raha ndugu yangu hapo bado mwanafunzi tu sina muda wa kutisha lakini niliweza kupata faida ya laki 150+ kwenye kila mzigo wa laki 2 na hapo niliuza kwa bei ya chini sana kuliko wengine.

Futa hayo mawazo mgando maana hata wewe ulipoajiriwa aliyekuajiri ni mfanya biashara pia.
 
Kwenye orodha ya matajiri Duniani.... hakuna tajiri mwajiriwa....ni kweli kuwa inahitaji jitihada kubwa na maarifa kujiajiri na ikakulipa....ila kama unahitaji mafanikio ya uhakika katika maisha basi kujiajiri ndio njia sahihi....kuajiriwa iwe njia ya kupitia kutafutia mitaji hasa kwa sisi tuliotoka katika familia za kimasikini....

Kwani hata mikopo ni rahisi kuipata ukiwa kwenye ajira....tatizo la ajira kipato chako anakupangia mtu mwengne tofauti na biashara faida unapanga wewe ....kuajiriwa ni utumwa wa kisasa na athari yake ni pale ajira inapokwisha wengi hurudi kwenye umasikini....hiyo mishahara mikubwa unayosema kwa mfanyabiashara mkubwa ni faida ya siku moja...

Watu kama kina azam wameajiri wakurugenzi na wanawalipa mishahara mikubwa kama hiyo...je wao wanaingiza kiasi gani?...mkinga kariakoo anaagiza kontena ya nguo za 500m na faida ni mara mbili....na mzigo anauza ndani ya mwezi mmoja au miwili.... mkuu muajiriwa ni masikini wa badae.... tutafute mitaji.
 
Asante sana kwa kumwelewesha huyu jamaa. Naomba nijazie kwa mifanyo kwenye haya ya pili na ya tatu.

Haya ya 1: ni kweli kabisa ukiona mfanyakazi analipwa pesa nzuri ujue mwenye biashara anachukua kikubwa.

Niliwahi kufanyia kazi kampuni x ambayo mtu wa juu alikuwa analipwa 20m na marupurupu. Kwa mwezi tulikuwa tunaingiza 2-3 b. Jamaa wakishatoa kodi mishahara na pesa za uendeshaji walikuwa wanabakisha faida ya 700m mpaka 1b

Aya ya 2:
Nikweli kiwango cha ukuaji wa mshahara ni tofauti na ukuaji wa biashara. Biashara ina nafasi kubwa.

Hiyo kampuni x niliyoizungumzia hapo juu mtaji wake ulikuwa 100b mwenye kampuni akaamua kuiuza na ikanunuliwa kwa 400b.

Baada ya kuuzwa tulibaki na mishahara yetu ile ile lakini mwenye biashara akapata faida mara dufu. Kumbuka hapo amepata billion 300 nje ya zile milioni 700 alizokuwa akipata kwa miaka 4 toka alipoanza biashara hiyo.
 
Duh sio mchezo Milion Mia 700 kwamwaka?

Kujiajiri raha sana hasa ukiwa namtaji. Sisi wenye biashara ndogondogo namitaji yetu haba vipato vyetu ukivichunguza vinalingana namishahara yawalimu, manesi, namaaskari.

Ila sisi tunawigo mpana wakutanua vipato vyetu, kwamfano mwezi wakwanza nampango wakuongeza biashara nyingine ishaifanyia mahesabu nakatika hiyo biashara nikikosa sana nikitoa gharama zauendeshaji basi sitakosa laki 2 na50 kwamwezi, huo nimfano wangu mimi ambaye mtaji wangu nimdogo kwahiyo mpaka hapo nitakuwa nimeongeza kipato chalaki 2 na50.

Je niwaajiri wangapi wanaweza kuwaongezea mshahara wafanyakazi wao kiasi chalaki 2 kwamwezi?
 
Sio kwa miaka hiyo walikuwa wanapata kila mwezi. Yaani kwa miaka ni milioni 700 x miezi 12.

Kwa kweli kama unaweza kujiajiri bora ufanye hivyo.

Nyongeza ya mishahara huwa nibkila Baada ya contract kuisha kwa upande wa private sector na kiasi kinachoongezwa so zaidi ya asilimia 10 ya mishahara wako.
 
WADAU HEBU TUELEWANE VIZURI

1. Kuajiriwa na kujiajiri wote wawili mnakuwa mnatafuta JOB; tofauti yenu ni "Degree of freedom", wa pili anaweza akachelewa kazini hata nusu saa kama hana attittude nzuri na asifanywe chochote na yeyote. Ila wa kwanza avute hata dakika 5 tu, atakiona cha moto, atafanywa mbaya, mara warning letter, mara kikao na H.R e.t.c

2. Mfanya biashara " mkubwa" kama mo** yuko tofauti kabisa. Kumbuka kuwa anafanya kitu kilekile kama cha aliyejiajiri but he is SMART.
-Hana job
-Kodi halipi kizembe (anajua kukwepa kodi).
-Hatumii pesa zake jamani; nimewasoma baadhi ya wadau hapo juu wamekazana "mpaka uwe na mtaji mkubwa, mara hela nyingi n.k" it doesn't work like that; watu hawa ni smart wanatumia hela zenu hizo mnazoziita 'ndogo'. Anazikusanya huko huko unakopeleka, bank au Pension funds i don't care na wanampa anazifanyia anachotaka kwa promise ya 'small percent'
-Hatumii nguvu zake au talent yake; anategemea usomeshe mtoto wako au ndugu yako apate hiyo masters au P.h.d, halafu yeye ainunue kwako kwa kuwa wewe mwenzangu na mie hujui jinsi ya kuitumia.

3. Mwekezaji a.k.a "Investor" this guy ndo Smart kupitiliza, we unahangaika unakuza kibiashara chako, na unahisi ni muda wa kukipeleka DSE; Jamaa ndo anakuja;
- Anaangalia una perform kiasi gani kwenye biashara zako annual returns
-Anakadiria future yako itakuwaje; halafu ananunua sehemu ya biashara yako kwa njia ya hisa.
-Sehemu inayobakia anakuachia wewe, uendeshe, usimamie mara mfanyakazi kazingua, mara T.R.A n.k yeye kakunja nne anasubiria R.O.I
 
Hao wafanya biashara wote ni investor pia Note.
 
The funny thing hata dunia ya kwanza waajiriwa wapo,wanaojiajiri pia wapo.
Kikubwa ni kuangalia tu unataka nini,kwa uzoefu wangu mdogo was nchi ya Tanzania mazingira ya kujiajiri na kutoboa ni magumu mno.

Yaani ukifanya survey ya mtumishi wa mwisho kwa mshahara serikalini maisha yake ni mazuri mara 10 ya wafanyabiashara/wajasiriamali wengi.

I.e.wajasiriamali wengi wa Tanzania ambao wesema wamejiajiri wanapata tu hela ya kula,yaani mitaji yao ni chini ya milioni 1.

kitu ambacho mtu aliyeajiriwa anaweza kukifanya muda wowote.
*hali ya umasikini wa wajasiriamali wadogo ni kubwa mno,kuliko wa watumishi wa serikali wanaopata ujira/mshahara mdogo*,ingawa wenye pesa nyingi ni wajasiriamali.

Watu wanazungumzia Uhuru..........mfanya biashara ambaye anapata laki 5 kwa mwezi,wengi wanafanya kazi zaidi ya masaa 12 hawana weekend hawana sikuu.
Wakati mwalimu wa aina hiyo anafanya kazi masaa 8 siku 5,ana weekend,ana sikukuu,......akitoka kazini ana boda boda.
Anaonesha video.

Mwisho kibongo bongo wengi wamekua wajasiriamali baada ya kufeli shule na kukosa kuajiriwa na si kama wanapasssion na biashara.

Kikubwa ni kuchagua unapoona unafaa,ukiajiriwa humrithishi mwanao ajira,ila hata ukijiajiri millioni 50(pesa ambayo zaidi ya 50% ya wafanyabiashara wa bongo ndio mitaji yao ama chini ya hapo),huwezi warithisha watoto wako 3 na mke wako, nao waje kua na hizo.

Kikubwa uangalie tu unapoona unafaa........mwajiriwa anayelipwa milioni 2 kwa mwezi ni ngumu umshawishi akalime matikiti maji akitegemea apate millioni 50,kwa hesabu za makaratasi wakati anaona mjini yanauzwa 500,tena wanayoyauza anaenda kazini anawaona anarudi anawaona.............
 
Umetazama masuala kama kujipangia muda, mapumziko, scaling ya mapato, kumnyenyekea mtu, n.k?
 
Sawa kiongozi , ila ujue faida ya investments sio ya kirahisi kama ulivyoisema , Hasa zile hisa za equity ambazo zinampa muwekezaji umiliki wa moja kwa moja wa rasilimali za uzalishaji.jahazi likienda mrama anakua wa mwisho kulipwa ka ma kitabaki chchte.

Hisa nyingine kama bond zinalipa fixed amount kwa mda flani na huwa ni kiasi kidg mnoo , mpk uwekeze fedha nyingi sna ndo utapata malipo ya maana. So sio simple kma unavyoiweka.
 
Umetazama masuala kama kujipangia muda, mapumziko, scaling ya mapato, kumnyenyekea mtu, n.k?
Mkuu mwajiriwa anaetafuta sympathy kwa boss wake ni yule ambaye uwezo wake wa kutenda kazi ni mdogo.mchapakazi na mtaalam katika fani yake kamwe hawezi kujipendekeza kwa boss.huwa kuna mitual respect kati yake na boss maana boss akizingua tu kuna waajiri wengine wengi wanamuhitaji.
 
I love this
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…