bro, inategemeeana na mwanamke wa aina gani uliyemwoa, msomi, mama wa nyumbani goli kipa, mfanya biashara, ana pesa au anakutegemea wewe asilimia mia moja. kamaa ni msomi au ana pesa, na wewe una pesa na ni msomi, yeye ametoka kwake akiwa na meno salasini na mbili na wewe hivyo hivyo, mmekulia familia tofauti zenye tabia tofauti, mikwaruzo haiepukiki, ni ya lazima, ila ni ule mwaka wa kwanza na wa pili tu, mkiishi zaidi ya hapo, mnasomana na kushibana hapo ndo mtaishi kwa mipaka na kuheshimiana kila mmoja kwa nafasi yake, la sivyo, huwa inaweza kutokea mapambano ya kushindania ukubwa au utoaji maamuzi ndani ya familia, labda uwe mwanaume *****.....wewe mwanaume ukiona mwanamke haleti challenge yeyote tangu umemuoa, ujue huyo mwanamke ni mbumbumbu au anaishi na wewe kwasababu ya interest fulani tu na anaogopa akikukwaruza lazima utamtema etc, lakini yule aliyekupenda na ana akili timamu, lazima atapenda kuwa huru mbele yako, hatapenda kuishi kama mtumwa ndani ya ndoa yaani atakuwa open kufanya kama alivyokuwa amezoea alipokuwa single, hapo ndopo mikwaruzo inatokea, lakini kwasababu ana akili, mkisettle mnayamaliza mapema na anakuwa mwelewa nini mipaka yake na nini mipaka yako...hapo ndo mtaishi vizuri sasa. ila hakuna ndoa isiyokuwa na mikwaruzo.
cha muhimu kujua ni kwamba, kuishi bila ndoa ni uzinzi, na ni dhambi...ila pamoja na mikwaruzo, hakuna kitu kizuri na chenye raha kama ndoa, hasa ukimwoa yule mnayeshibana na kwendana....ninyi ambao bado mko nje ya ndoa, mnazini na mnapoteza muda....na kukosa raha na mambo mengi.