Hakuna ubaya wowote kwa Saudi Arabia kupewa uendelezaji bandari ya Bagamoyo, endapo tu, kama mikataba itakuwa ya wazi na yenye tija!

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Uwazi wa mikataba kwa umma, ndipo kilio kilipo, tuingie mikataba safi, ya vipindi vifupi kadri iwezekanavyo, mamlaka zetu kama tra ziweze kufanya kazi yake kwa uhuru, gawio letu lisiwe chini ya 30% govt gain up!

Huku 70% ikitumika kulipia ujenzi na gharama za wabia, nathubutu kusema hakuna ubaya wowote, isipokuwa tutajiongezea mapato yetu kwa Trilion kadhaa!

N. B, viongozi wetu waache woga, wasonge mbele tuzidishe mapato yetu ya ndani hatimaye tuweze kujitegemea na kuwa stable country!

-Tuongeze mapato ya kiushuru kwa taifa ukizingatia Tanzania yetu walipa kodi ni wachache sana, na wanaolalama wengi wao si walipa kodi, bali kupiga tu kelele! / vyanzo hivi vya kodi vya lazima ndio njia nzuri zaidi ya kuongeza mapato!
 
Tatizo Tanzania Kuna Wenyenchi ambao ndio hutawala (nje ya utawala wa Kidemokrasia) na Kuna wananchi ambao ndio huishi na kutawaliwa humo (kama tenants tu), hawapaswi kujua ya wenye nchi au landlords wao.
Kama siko sahihi, nieleweshwe ushirikishwaji wa wananchi ukoje kwenye issue kubwa zinazopaswa kuwaondolea shaka kwa elimu shirikishi.
 
Hoja hii ya Saudia kujenga na kumiliki Bandar Bwagamoyo lina maswali mengi na labda tulio wengi hatujajua undani.
Lakini ndio haya mambo ya Bwana Kafulila ya PPP.
Kafulila mara nyingi amekuwa akinadi na akijigamba kwamba BADALA ya serikali kutumia pesa zake hadimu kufanya miradi,wawekezaji wanafanya miradi hiyo na baadae huduma inatozwa kiasi fulani na watumiaji.
Pia kodi na ushuru wa serikali unazidi kuongezeka kupitia PPP.

Sasa reality ndio hizo Saudia atazamisha mabilioni kwa mabilioni ya dola kujenga miundo mbinu ya kisasa,nasikia hata Bandari ya Durban na Singapore zitakuwa cha mtoto.
Lakini ile njia ya kufanya biashara kwa nchi za Kongo,Uganda,Rwanda,Burudi,Zambia hadi Angola kutoka mashariki ya Afrika hadi magharibi ya Africa Bandari ya Bwagamoyo ndio Timizo.

Kazi ya msingi ya bandari ni kupakia na kupakua mizigo kutoka/kuingiza kwenye meli.
Kichocheo ni miundo mbinu yenye ubora na wepesi wakuhudumia meli na shehena nyingi kwa MUDA MCHACHE.
Bila kusahau nguvu kazi yenye tija na sheria rafiki,ushuru wenye mashiko.
 
Bado Tunao wataalamu wa sheria wazuri tu, mfano sioni ubaya mkataba safi ukatengenezwa na professor, Palamagamba kabudi mbobevu huyu sina mashaka naye!
Huu ndiyo wakati sahihi, na muda sahihi, lakini mikataba nayo iwe sahihi.
 
Nipe Geopolitical situation zinazofanya tusipanue Tanga au Mtwara. Na pia tuambia why that strategy tusichukue sie wenyewe hata kwa ku issue bond. Na kama wataalamu tutawaajiri ?. Nipe business case inayopelekea tubinafusishe or sale.
 
Suala la kubinafsisha au kuuza halipo katika project iliyopo, elewa kwanza hapo, hapa ni PPP agreement, Bagamoyo ni uso unaotazama bahari vizuri zaidi, hakuna ubaya wa kuwa na multiples harbours, stadiums, and etc!
 
Bring business case. Kuwa by 2030 tunahitaji bandari , na kuipata yahitajika kiasi flani. We can raise kiasi hiki within. Uenedheshaji utafanywa na nani na kwa nini?. Je tuna resources or tunataka kupata nini
 
Suala la kubinafsisha au kuuza halipo katika project iliyopo, elewa kwanza hapo, hapa ni PPP agreement, Bagamoyo ni uso unaotazama bahari vizuri zaidi, hakuna ubaya wa kuwa na multiples harbours, stadiums, and etc!
If it's ppp, fine means ukiweka Bond ina maana wale matajiri kkoo wataacha kununu v8 watanunua bond for investment. Why mnawakosesha umuliki wananchi umilili ba sovereignty. Je ni haraka yahitajika?. Why baby you give him a luganga project to build a smelter for iron ore?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…