Hakuna Udini kwenye Katiba Inayopendekezwa-Mangula

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,536
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara, Philip Mangula amesema kuwa viongozi wa dini wasiwapotoshe wananchi kuhusiana na kuwapo kwa masuala ya dini katika katiba pendekezwa wala Kipengele kinachotaja masuala ya dini na mahakama ya Kadhi.

Akizungumza na wanafunzi wa sekondari, chuo na walimu katika shule ya Hagafilo Mkoani Njombe wakati akitoa elimu ya katiba pendekezwa, amesema kuwa ameisoma katiba yote na hajaona kipengele kinacho zungumzia masuala ya udini wala mahakama ya kadhi.

Lakini hata hivyo viongozi wa dini wanapinga muswada wa mahakama ya kadhi kupitishwa bungeni na kuwa sheria.
Amesema kuwa alikuwa katika kanisa moja anako Sali mchungaji wake alisema kuwa waumini wasiipigie kura katiba pendekezwa kwa kuwa ina masuala ya Mahakama ya Kadhi alipo muuliza ni katika kipengele gani kinacho zungumzia mahakama hiyo mchungaji huyo hata kipengele hicho alisema hakifahamu.

Amesema kuwa katiba hiyo haina kipengele hata kimoja kinachozungumzia dini yoyote na kuna kipengele kinacho zungumzia utawala wa sheria na kuwapo kwa mahakama huruAmesema kuwa katika katiba pendekezwa kuna misingi ya utawala bora na umiliki wa ardhi na kuwa ardhi hiyo inatunza na kuwa ni mali ya mtanzania wa kizazi cha sasa na cha baadaye.

Katika hatua nyingine Mangula ameungana na kauli ya kiongozi katoriki Muadhama Kadinali Policarp Pengo kuhusiana na kuwaruhusu wananchi kuchukua maamuzi yao wenyewe juu ya kupiga kura ya ndio au hapana.
Amesema kuwa wananchi wakiisoma katiba wao wenyewe wakaielewa kama kuna mapungufu watayaona waikatae wao wenyewe na wanaosema isipigiwe kura wawe na hoja kwanini isipigiwe kura na sio wanasema hivyo bila kuwa na hoja sahihi
 
Katiba hainyeshi udini ndiyo, lakini ujanja wa kutumia udini ili ipite nadhani ndicho kinacholalamikiwa na baadhi ya viongozi wa dini.
 
Mangula kamsikia kiongozi wa kanisa akiwadanganya na akiwashawishi wakristo waikatae katiba pendekezwa kwa sababu ina kipengele cha mahakama ya kadhi, ww unasema unatumika ujanja wa kidini kupitisha katiba mbona unapindisha ukweli mkuu, hebu tubie huo ujanja wa kidini unatumika.
 
Huyu mzee kafirisika tu

huyu mzee mzalendo sana sio sawa na yule bebari wa tengeru anamiliki heka 800, wataki waliomzunguuka hawana mashamba wala sehemu za kufugia, matokeo yake wakulima na wafugaji wakigombana yeye anailam serikali, aibu kwake
 
Anafanya politics tulizozizoea za ccm za kasema uongo tu
 
Mangula kamsikia kiongozi wa kanisa akiwadanganya na akiwashawishi wakristo waikatae katiba pendekezwa kwa sababu ina kipengele cha mahakama ya kadhi, ww unasema unatumika ujanja wa kidini kupitisha katiba mbona unapindisha ukweli mkuu, hebu tubie huo ujanja wa kidini unatumika.

Mkuu, nadhani nao viongozi wa dini wamegawanyika - wengine wanasema huo ujanja na wengine ni kweli wanadai kwenye Katiba kuna mahakama ya kadhi au walichanganya na ile sheria iliyokuwa imeletwa bungeni nini!
 
Katiba hainyeshi udini ndiyo, lakini ujanja wa kutumia udini ili ipite nadhani ndicho kinacholalamikiwa na baadhi ya viongozi wa dini.

Za kuambiwa changanya na zako,kura utapiga mwenyewe wala huyo kiongozi wa dini hautamuona akikusimamia!
 
Sure mkuu, sijawahi kupiga kura kwa kuambiwa. I always use my freedom at least 100 per cent.
Kwanza kura ni siri ya mtu, mtu anayepita kutangaza tangaza kura yake tunamuona mshamba na kama mtoto aliyetimiza umri wa miaka 18 juzi juzi tu
 
Sijui kama maoni haya ni relevant kwa quote uliyotumia.
 
Hakuna suala la kama hilo labda hiyo agenda uianzishe wewe!

Hujaelewa mantiki ya mchango wangu. Sikusema ninachodhani mimi, bali nilichangia wanachokidhania baadhi ya viongozi wa dini maana hoja yenyewe ilihusu hao viongozi wa dini. Jaribu kuelewa hoja inayoletwa siyo kuchangia tu kabla ya kuelewa.
 
Back
Top Bottom