Kwanza tuanzie hapa nini maana ya UGAIDI?
Imeelezewa vizuri katika kifungu cha 4 cha sheria ya Ugaidi Soma hapa
4.-(1) Mtu yeyote aliye ndani au nje ya Jamhuri ya Muungano anayefanya kitendo cha kigaidi anatenda kosa.
(2) Mtu anatenda kitendo cha kigaidi ikiwa kitendo hicho au kushindwa kutenda kunafanywa kwa lengo la-
(a) kutisha sana au kusababisha hofu miongoni mwa wananchi au sehemu ya wananchi;
(b) kutisha sana au kuishinikiza Serikali au shirika la kimataifa kufanya au kuacha kufanya kitendo chochote; au
(c) kudhoofisha au kutetemesha kwa kiwango kikubwa taasisi za kidini, kisiasa, kikatiba, kiuchumi au kijamii za nchi au za shirika la kimataifa.
(3) Neno "kitendo cha kigaidi" linamaanisha, kitendo au tishio la kuchukua hatua au kushindwa kuchukua hatua ambacho kinahusisha:
(a) shambulio dhidi ya uhai wa mtu ambalo linaweza kusababisha kifo au madhara makubwa ya mwili;
(b) utekaji nyara wa mtu;
(c) uharibifu mkubwa wa mali;
(d) hatari kubwa kwa afya au usalama wa umma au sehemu ya umma;
(e) matumizi ya silaha za moto au vilipuzi;
(f) kuachilia katika mazingira au sehemu yoyote yake au kusambaza au kuwaweka wazi wananchi au sehemu yake kwa-
(i) dutu yoyote hatari, yenye mionzi au yenye madhara;
(ii) kemikali yenye sumu; au
(iii) vijidudu au wakala mwingine wa kibayolojia au sumu;
(g) kutatiza mfumo wowote wa kompyuta au utoaji wa huduma zinazohusiana moja kwa moja na miundombinu ya mawasiliano, huduma za benki au fedha, huduma za umma, usafirishaji au miundombinu mingine muhimu; au
(h) kutatiza utoaji wa huduma muhimu za dharura kama vile polisi, ulinzi wa raia au huduma za matibabu.
(4) Kitendo ambacho-
(a) kinatatiza huduma tu; na
(b) kimefanywa kwa kutekeleza maandamano, mhadhara au mgomo wa kazi,
hakita chukuliwa kuwa ni kitendo cha kigaidi kwa maana ya kifungu hiki, mradi tu kitendo hicho hakikusudiwi kuleta madhara yoyote yaliyotajwa chini ya kifungu kidogo cha (2).