Hakuna umuhimu wa ndoa katika karne hii

Ishi sana Mkuu
 
Kwanza kabisa hujajibu hoja yangu, pili ukiwa unajadili mada kama hizi jitahidi usitumie reference ya vitabu vya dini maana si kila mtu anaamini dini, na pia kuna dini zaidi ya 1000 duniani na kila moja inaamini miungu yake na ina kanuni zake vinginevyo utaibua maswali ambayo hutaweza kuyajibu
 
Poa bac achana na kanuni ya Bible ambayo ndo yaasili na ipo wazi.

Soma biology ujue kwamba hata mwili wa mwanamke tu kiasili ni very weak ukiringanisha na mwanaume.
Soma psychology kuhusu power of interpreting things huwezi ukaringanisha hawa viumbe wawili mtuangu.

Tungekua kiasili tunaringana duniani kusingekua na pambano ya gender equality.
Eti mkiwezeshwa mnaweza.......
 
Sasa unaposema mwili wa mwanamke ni weak unamaanisha uko weak kwenye nini na kwanini hiyo weakness mmeiweka kwenye aspect ya kimaumbile tu, mtu anayeweza kubeba kiumbe tumboni miezi tisa na kuvumilia maumivu ya kukileta kiumbe hiko duniani utasemaje ni weak, na kwanini utake kumtawala binadamu mwenzio mwenye utashi kama wewe kwa kutumia sifa za kimaumbile ambazo yeye hajaumbwa nazo na hakupenda kutokuwa nazo
 
Asili ya jamii yoyote iliyo starabika ni ndoa, kwani watoto wakilelewa kwenye ndoa.Mara nyingi watoto walio lelewa kwenye ndoa huwa na tabia nzuri pamoja na nidhamu ya hali ya juu. Kinyume cha hapo single parenting mara nyingi ndio inazalisha watoto wa mitaani, kuna watoto wanatabia za hovyo, watoto wanao jihusisha na maswala ya ngono ya jinsia moja nk na sometimes watoto wanakuwa mabalozi wabaya wa ndoa.

Thamani ya ndoa ni kubwa mno kama kweli mahusiano ya uchumba yakijengwa na kwenye misingi ya upendo wa kweli, kujaliana na kila mtu kujua nafasi yake kwenye ndoa na familia na si kushindana na huku wakimtanguliza Mungu.
 
Skia Jadda: nadhani unakubali kua jukumu la mwanaume ni kumhudumia na kumlinda mwanamke, na wanawake wote mnajua hilo.
Mwanamke unatakiwa kumuheshimu sana mwanaume kwasababu mwanaume anafanya majukumu yake kwako kwaajili ya mapenzi na heshima yako tu.
Kwahiyo Jadda: muheshimu sana mmeo kwasababu yeye ndo kichwa/kiongozi/mtawala/mfalme wa familia yenu.
 
Hapa sasa ndio umekuja kwenye point mwanamke anatakiwa amtii mwanaume endapo huyo mwanaume anawajibika juu yake kwa maana kwamba anamhudumia tu na si vinginevyo, lakini masuala ya kusema eti mwanamke anatakiwa amtii mwanaume eti kwa sababu tu mwanamke ni weak na mwanaume ni strong ni uongo na utaibua maswali mengi ambayo utashindwa kuyajibu, hakuna mamlaka bila wajabu kama mwanaume hawajibiki kumhudumia mwanamke basi hastahili kupewa utii ila kama anahudumia basi utii ni haki yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…