Hakuna utofauti wa wanaume wa Dar na wengine

Principal Focus

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2013
Posts
925
Reaction score
550
Habari wana jf!

Kwanza kabisa napenda niweke wazi mimi si mkazi wa dar ila kusoma tu ndo kulinifanya nifike dar bila hivyo ningebaki porini kwwtu kama kungekuwa na chuo kinafundisha yale niliyokwenda somea.

Hili bifu na wanaume wa dar na mikoani naona ni declare kabisa mimi sifungamani na upande wowote, nina marafiki mikoa mbalimbali na dar pia nina marafiki. So sitaki nitajwe kwenye hili bifu ambalo sijui mqanzo wake.

Ukweli ni kuwa sisi wanaume wa mkoani tukisikia dar mioyo yetu inafurahi sana maana kwa watz wote dar ni mji ambao wengi hutamani kufika kusafisha macho. Ni kama vile mtu umtoe Afrika kwenda Amerika ni kitu ambacho atafurahi sana maana ni moja ya miji mizuri, vivyo hivyo na kwa watz tukiambiwa kwenda dar tunafurahi sana maana kule ndo kila kitu kipo.

Nimeona mijadala mingi tu mara sijui wanakula vipande viwili vya mkate, mara uji na dagaa mchele(nimewamiss sana nyie), kiukweli hizi hoja hazina mashiko mara eti sijui nguvu za kiume n.k hii mijadala imekuwa ikiendeshwa kwa mihemko na wivu pamoja na chuki kama ukikutanisha ccm na chadema.

Kiukweli dar mjini kila moja analake sema wingi wa media na ukuaji wa teknojia na utandawazi ndio hutokea kama sample ya kutolea mfano ila pengine wa mikoani wanatatizo kubwa kuliko wa dar. Kila mmoja na siri yake hivyo mwanaume atabaki kuwa mwanaume, ukisema wanalelewa a.k.a mario hata mikoani wapo, ukitafuta mashoga hata mikoani wapo pia ukitafuta wenye ukosefu wa nguvu za kiume hata mikoani wapo.
Tena kukaa dar kipindi cha anko magu ni uanaume haswa na wingi wa maarifa hivyo kumnyoshea mtu kidole na kusema wewe ni bora kuliko mwingine werevu watajua wewe ndio unatatizo.


Mwisho mwanaume atabaki kuwa mwanaume hata awe ametokea dar huwezi mbadili maana ndivyo alivyo. Chuki yako usipandikize kwa mwingine.
 
NAONA UNAWATETEA WENZAKO MKUU

HAHAHA LAKINI UJUE HUU NI UTANI TU SIO KWAMBA NI ISHU SERIOUS SANA HADI KUCHUKIANA
 
Utofauti upo mkuu, tena mkubwa tu
 
Kwanza wanaume wa dar tumetokea mikoani...sijui hawa wanaoitwa wanaume wa dar ni wazalamo au maana sisi wengne tupo huku kisa kutafuta maisha ila tumekulia mikoani...kama ni kulima tunajua na shida zote za mikoani tunajua...sasa nini maana ya wanaume wa dar??
 
Embu waambie ndugu GuDume sijui na watamwita nani sasa
 
WanabadilikA kivip
Mkuu umesema hoja yangu haina maana kabla hujanisikiliza, halafu unaniuliza tena, kwa kifupi mtu yoyote anayeishi jijini ni tofauti na mtu anayeishi kijijini, hivyo mtu anayeishi Dar na anayeishi mkoani hawawezi kufanana, kwa sababu changamoto zao zinatofautiana
 
Haya mkuu. Hata dar kuna vijiji pia
 
mimi nimezaliwa na kukulia dar ila si mzaramo na mechi zangu na mademu sijawah kufungwa wakijitahidi sana nimewapiga bao chache.
Ndo najiuliza sasa hao wanaoponda wanaume wa dar... Sijui wewe watakuita nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…