Mods tafadhali msiunganishe uzi huu na mwingine wa kuhusu PELE`
Jamani hamna wa kulinganishwa na Pele` wa Brazil. Hamna wa kumfikia Adson Arantes Dos`Nacimento(PELE).
Pele wa Brazil ndiyo mchezaji wa mpira wa miguu wa hali ya juu zaidi kuwahi kutokea duniani mpaka sasa, mimi hapa mwenye uzi wachezaji wote mahili duniani nimewaona wakicheza akiwemo king PELE`, nasema PELE` hamna wa kulingana nae, yaani huyo Maraddona hamfikii PELE` hata robo.
Kwanza nitamlinganisha PELE` na Maradona tu.
Kuna vigezo vingiiiii, naona nitawachosha tu, tatizo kuhusu wachazaji hawa nyie kizazi kipya mnaelezewa na akina Eddo Kumwembe ambao hawajui chochote wamewaona akina Rodadinno na akina Maradona tu PELE`hawajomwona zaidi ya kwenye vicrips crips, mimi nimemwona hasaaa uwanjani, na Maradona nimemwona hasaa uwanjani.
Sasa vionjo tu.

| NO | KIGEZO | PELE ` | Maradona |
| 1 | umri | Miaka 82 na zaidi | Miaka 60 |
| 2 | Sheria za mpira | PELE` alicheza wakati wa sheria za zamani, rafu, kukatwa kwa nyuma n.k | Maradona amecheza mpira wakati sheria zimeboreshwa hasa kuwalinda mastaa |
| 3 | Viwanja | Wakati wa PELE` viwanja havikuwa vizuri mfano kuwekewa nyasi za bandia na maboresho mengine | Maradona kacheza mpira wakati viwanja vimeboreshwa, nyasi za bandia na vikorombwezo vingine |
| 4 | Kunyanyua kombe dunia | King PELE` amelinyanyua mara 3, Jules Ramet cup mpaka Brazil walilitwaa moja kwa moja | Maradona amenyakua kombe la dunia mara moja tu (kombe la sasa FIFA 1974) |
| 5 | Kadi nyekundu wakati wa mashindano ya kombe la dunia | King PELE` hakuwahi kupewa kadi nyekundu wakati akicheza fainali ya kombe la dunia | Maradona alipewa kadi nyekundu mwaka 1982 fainali zaSpain |
| 6 | Kucheza fainali (mcezo wa mwisho kombe uwanjani) | King PELE` amecheza fainali 2, 1958 ma 1970 na zote alinyakua ndoo | Maradona amecheza mala moja 1986 Mexico |
| 7 | Magoli mechi za ushindani | Magoli zaidi ya 1000 King PELE`alifunga | Maradona hata 600 hakufikisha |
| 8 | Aina ya vionjo(style) | PELE` ndiye mwanzilishi wa style zote: Tik-tak,byscle kick,scissor kick,scorpion kick | Maradona style zote alizokuwa anacheza PELE` Maradona sijamwona akizicheza (wote nimewaona) |
| 9 | Kunyumbulika | King PELE` alikuwa anatumia miguu yote kulia, kushoto, mpira uje kivyovyote: mbele, nyuma,mgongoni, mabegani uje tu | Maradona alikuwa anatumia mguu mmoja wa kushoto , alikuwa anautumia vizuri sana naomba kukili kwa hilo |
| 10 | Kufunga magoli | King PELE` alikuwa anafunga kivyovyote: mashuti makali na laini, magoli ya kuplace, kichwa, faulo za kutenga, penati n.k | Maradona uwezo huo alikuwa hana,goli la kichwa pekee ni lile la mkona alilowafunga Waingereza. |
Kuna vigezo vingiiiii, naona nitawachosha tu, tatizo kuhusu wachazaji hawa nyie kizazi kipya mnaelezewa na akina Eddo Kumwembe ambao hawajui chochote wamewaona akina Rodadinno na akina Maradona tu PELE`hawajomwona zaidi ya kwenye vicrips crips, mimi nimemwona hasaaa uwanjani, na Maradona nimemwona hasaa uwanjani.
Sasa vionjo tu.
- PELE`hakucheza Ulaya kwa sababu bunge la Brazil liliamua kuwa PELE` ni nyala ya taifa kwa hiyo hauzwi, hakuna mchezaji yoyote duniani aliyefanyiwa hivyo
- PELE kule Columbia alipoenda na klabu chake cha Santos alifanyiwa rafu naye akalipiza kisasi, Refa akamtoa PELE` kwa kadi nyekundu, uwanja mzima ulipiga kelele PELE` akarudishwa uwanjani refa akatolewa nje, hakuna mchezaji yoyote aliyewahi kufanyiwa hivyo.
- 1972 Club ya Dar-es Salaam Young African chini ya uongozi wa Mbwambo na Tabu Mangala waliandaa mradi wa kumwalika PELE` na klabu yake ya Santos waje Dar kucheza mchezo wa kirafiki, Walienda Brazil wakafikia makubaliano. Yanga wakajiandaa kabisa kupokea ugeni huo na wakatengeneza kabisa na kanga ziliandikwa “ PELE NA SANTOS WAGENI WA YANGA”. Sasa wakati ulipowadia Mke wa PELE` akajifungua ikabidi Klabu ya Santos ije peke yake bila PELE` Klabu ya Yanga ikafuta mradi huo,ikaona Santos kuja bila PELE` haina maana yoyote. Wakafutilia kwa mbali mwaliko huo ila kanga zipo wakina mama wengine wanazo mpaka leo wameweka ukumbusho.