Hakuna wa kumzidi Lunya kwa sasa

Rexwinton

Member
Joined
Mar 26, 2021
Posts
74
Reaction score
137
Tuukubali ukweli kwamba kila nabii na zama zake. Tuliona miaka ya elfu mbili mastaa kama Professor Jay, Ngwea, Fid Q, Kalapina, Juma Nature n.k, wakitawala Hip Hop huku Fid Q ndio akivaa taji.

Zama zikapita, zikaja zama za 2010, tukaona vipaji kama Roma, Stamina, Young D, Young Killer, Dogo Janja, Weusi, blah blah, huku Roma akivaa taji.

Wakavuma lakini nao wameanza kufifia, kinaibuka kizazi hiki cha kina Lunya, Rapcha na madogo wengine wengi, lakini itoshe kusema kuwa Lunya ndiyo kavaa taji la Hip Hop sasa, hilo halina ubishi. Aina yake ya kutiririka hakuna wa kumkalisha kwa sasa, hilo halina ubishi aisee!
 
Top List kwa hii Generation ni mtazamo tu.
1.FidQ [emoji146]
2.Dizasta vina[emoji238]
3.Stamina[emoji981]
4.Monicetralzone[emoji350]
5.Con boi
6.Salmin swagg
7.Young killer
8.Young Lunya
9.Country boe
10.Motral the future

SAB.
Rapcha
Marifaa
Nacha
Kontawa
Ghafla bin Vuu.
 
Mjomba yule hamna kitu anapiga tu kelele hakuna anachorap , yule media zinampromote ila mitaa inarappers wake , akirap mwanzo hadi anamaliza hauelewi alikuwa anarap nn, TUPAC IS TRUTH, kamsilize tupac anavyotembea na flow anarap ukweli wa maisha duniani , harakati na kila kitu sa rappers ndo wanatakiwa kuwa vile, kwa bongo bado FID Q ndo father na king wa hip hop mpaka atakapoondoka duniani
 
Mwanahip anatakiwa kurap ukweli na sio kurap uongo uongo ambao haupo, lunya ni rapper mwepesi sana hauwezi kumsimamisha ata na Nikki mbishi, bongo kuna rappers wanakuzwa na media houses tu lakini hakuna kitu ni kama ROSA REE tu hauwezi msimamisha na Frida Amani wala Chemical
 
Bro!Nyakati Zinabadilika Rap Game ni Sehemu ya Burudani Pia...Sio Kila Muda Uimbe Matatizo Tu...Kumbuka Hata Pac Kwenye Ngom Kama How do u Want....Me And My Girlfriend Hakuna Cha Maana Sana Alichoimba Zaidi ya Ma beef tu aliyokuwa nayo dhidi ya Masela.Acha Baadhi Ya Rappers Wa"Base" Kwenye Kuimba Reality na Wengine Waimbe Rap ya Kuburudisha Then Wasikilizaji Ndio Wataamua Wamsikilize Yupi Wamwache Yupi..By The Way Kuanzia Mamtoni Hadi Huku Uswahilini "Soft Rap" Ndio Inasikilizwa Zaidi.Angalia AudioMack Then Compare Listeners wa Nikki mbishi na Listeners wa young Lunya.. Listeners Wa Joey Baddas na Listeners Wa Lil Uzi Vert...Music is Dynamic!
 
Kifupi ni kwamba dogo anatembea na nyakati.
Ila kuna wabishi na wasioelewa kwamba bendera hupepea na beat la upepo wao wamekomaa tuu na upande mmoja.....wao wanauita "Ukweli"
Dunia ya sasa inaendeshwa kwa software,angalia movie za sasa ndo utaelewa. Na ndo maana wengi wamepotea kwa game
 
Tutajie hit song zake hata tano ili tuone Kama ana kitu

Rapcha ana hit song 1 Lisah

toa majibu
 
Lunya anajua sema style yake ni lain verse zake hazina mistar za utata kama wakina fid na killer
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…