Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Katika watu wajinga, nafikiri wanaoamini habari za kichawi wanaongoza. Nimekuja kugundua kuwa mambo mengi yanayoaminika kutokana na uchawi, yanaaminika hivyo sababu ya watu kuwa wajinga. Nitoe mifano.
1. Kuna mtu alikuwa anapata kinyesi cheusi. sasa sababu ya ujinga akawa anaamini amerogwa. Lakini kumbe kile kinyesi cheusi ni dalili ya vidonda vya tumbo, na ule weusi ni madini chuma kutoka kwenye damu inayomvuja tumboni.
2. Mtu mwingine akasema wazungu nao wachawi sana. kuna kijiji watu walikuwa wanakufa kwa radi. Mzungu akaja akasimamisha kamnara tu radi ikaacha kuua watu.
3. Wengi wanaamini vichaa wanaotembea barabarani wamerogwa. Lakini vichaa karibu vyote vinatokana na vichocheo kuyumba au kujeruhiwa kwa ubongo.
4. Watu wanaamini bundi wanatumiwa na wachawi sababu wanatembea usiku. Lakini tunajua uwezo wa bundi kuona usiku ndiyo unamuwezesha kufanya mawindo yake usiku.
5. Watu kwa ujinga wa kushindwa kupiga hesabu za mapato na matumizi, na kuweza kutunza pesa wanasingizia chuma ulete.
6. Magonjwa mengi hapo zamani yalidhaniwa kuwa yanatokana na kurogwa. Lakini sababu zake hasa zimekuja kufahamika. ujinga ndiyo ulifanya watu waamini kuna kurogwa. Kuna mchezaji amefariki juzi mguu unaoza yeye anasema ametupiwa jini.
7. Kanuni za kilimo zinajulikana lakini unakuta kuna watu wanaamini mtu anaweza kuroga apate mazao mengi, au akakuroga usipate mazao ya kutosha.
8.Madini yanapopatikana na jinsi ya kuyachimba huwa inafahamika, l;akini watu huwa wanaamini yanapatikana kwa uchawi.
9. Mara kuna uchawi wa kuleta mvua na hali habari ya ujio wa mvua na kutokuja zinajulikana.
10. Wengine wanaamini uchawi unaweza kukusaidia kwenye uvuvi.
11. wengine wanasema kuna wachawi huwa wanaingilia watu kingono!!1!
Kiufupi, wajinga wakishindwa kuelewa kitu wanasingizia uchawi. Hakuna kitu kinafunua ujinga wa mtu kama imani yake juu ya habari za kichawi. Jinsi ilivyo kali ndivyo ujinga wake ulivyo mkali zaidi.