Hakutatokea tena msanii mkali, mwenye kipaji kama 20%

beatboi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
561
Reaction score
1,356
hakutatokea tena msanii mkali, mwenye kipaji cha kueleweka na watu wa lika zote kama 20%...
kipindi hicho anatoka ili msanii ukubarike ni lazima ubane pua au uwe na sauti ya kumtoa nyoka pangoni, ilikuwa ngumu kupenya mbele ya wababe wa melody kipindi hicho kama wakina mb dog, z anto,matonya nk.
mchizi alipasua katikati na sauti yake ya mkwaluzo na kuvunja na kuweka record ya kuchukua tuzo za kili 5 bila kuwa na makandokando yoyote yale sababu hadi wapinzani walikubali jamaa alistahili, baada ya hapo tuzo zikawa zimepoteza mvuto na kufa kabisa kwani walianza kupeana kiholela...
mungu amfanyie wepesi ndugu yetu arudi kwenye muziki kwani pengo lake lipo wazi...
 

Attachments

  • 20_naficha_h264_48632.mp4
    6.6 MB
Mziki biashara siku hizi😂😂... uyo bange zilimpeleka matopeni uko
 
Wewe unawajua wasanii. Kwangu pia huyu ndo msanii bora wa Bongofleva wa muda wote kwa utunzi na kughani. Mashairi yake yalieleweka kwa dhumuni la kuelimisha, kuburudisha, kuonya na kuelekeza jamii. 20per bila bangi hana mshindani.
 
Kipaji cha album moja
 
Mama Neema..[emoji22][emoji22][emoji22] 20%
 
Dawa aina ya bange ni hatari sana ukiitumie bila kufata mashart hasa ya lishe! Huyu jamaa angekuwepo muzikini tungekuwa na miziki ya kusikiliza na wakwe zetu na watoto wetu bila tahadhar!
 
Moja ya mstari bora kabisa "rahisisha mahitaji yako, ongeza kipato chako.......".
 
Mziki biashara siku hizi😂😂... uyo bange zilimpeleka matopeni uko
kwa kipindi kile wasanii wengi bongo walikuwa hwajui target yao wengi walilizika na umaarufu tuh, na pesa wakawa wanapiga wachache
 
Wewe unawajua wasanii. Kwangu pia huyu ndo msanii bora wa Bongofleva wa muda wote kwa utunzi na kughani. Mashairi yake yalieleweka kwa dhumuni la kuelimisha, kuburudisha, kuonya na kuelekeza jamii. 20per bila bangi hana mshindani.
wengi wanaofanya mziki wa kijamii zaidi huwa hawajui biashara ya Mziki, wengi hufurahia kuona ujumbe wao umefika kwa hadhira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…