Halal badr, tawaswil na visomo vilivyosomwa wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
kipanya.jpg

Wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes nilikutana na matokeo manne ambayo wananchi walijikusanya na kufanya visomo au dua kujikinga na dhulma za ukoloni wa Waingereza.

Katika matukio haya manne ya kumuomba Mungu ni tukio moja tu ndilo wafanyaji kisomo walichobainisha kuwa inayosomwa ni ‘’Halal Badr’’ neno ambalo hivi sasa limekuwa maarufu midomoni mwa watu wengi baada ya kuelezwa kuwa kutasomwa Halal Badr makhsusi kufuatia jaribio la kumuua Mbunge wa Singida Mashariki, Mheshimiwa Tundu Lissu.

Nitarudi nyuma kiasi cha nuru karne na zaidi kuangalia nafasi ya visomo katika kutafuta haki. Nitaaanza kwa kueleza mazingira yaliyokuwapo wakati wa ukoloni hadi kusababisha wananchi kumgeukia Mungu na kutaka msaada wake na hivyo kusoma Halal Badr.

Nakuwekea msomaji wangu yale niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes, kitabu ambacho ndani yake nimejaribu kueleza historia ya uhuru wa na kuandika kuhusu Halal Badr ili kwa yule ambae ni mgeni katika mambo haya apate picha kamili na Tanganyika ili uweze kuona ilikuwa na kujua ni wakati gani wananchi waliamua kufanya dua iwe Halal Badr au kisomo kingine kama kinga yao dhidi ya nguvu ambayo wao waliona ni Mungu pekee ndiye angeliweza kuwapa nusra.

Labda tujiulize imekuwaje leo baada ya zaidi ya nusu karne wananchi wanarejea katika mbinu ambazo wengi wanaona kuwa kuzirejea tena katika Tanzaia huru ni kitu ambacho kidogo kinashangaza hasa kwa kuwa dini kama inavyoelezwa kuwa haina nafasi katika uendeshaji wa serikali.

Naanza kwa kukuwekea hapo chini mara yangu ya kwanza nilipokutana na huu makakati ambao kwa hakika ulikuwa mpya katika mbinu za kudai haki kwa kukueleza vuguvugu la makuli katika bandari ya Dar es Salaam pale walipoamua kupambana na dhulma za wakoloni kwa kusoma Halal Badr mwaka wa 1947:

‘’…kidogo kidogo Kleist alianza kumkabidhi Abdulwahid kazi za African Association na mara akawa msaidizi wa baba yake katika siasa za Dar es Salaam. Ilikuwa katika kutimiza haya ndipo Abdulwahid akajikuta anahusika na ule mgogoro wa makuli ulioibuka bandarini Dar es Salaam ambao ulikuwa ukichemka pole pole chini kwa chini kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa vita.

Hatimaye, Abdulwahid alihusika na harakati za siri za wafanyakazi bandarini ambao, wakiwa wamechoshwa na sheria za kazi za ukandamizaji na wakiwa wamechoka kunyonywa na makampuni ya meli, walikuwa wanapanga kuitisha mgomo.

Chama cha African Association ndicho kiliwakilisha maslahi ya wananchi wa Tanganyika na kimya kimya kiliunga mkono zile harakati za chini kwa chini za wafanyakazi katika kutafuta haki zao. Abdulwahid, kijana mdogo mwenye elimu na akiwa karibu zaidi na uongozi wa African Association kuliko Mwafrika yoyote pale mjini, alichaguliwa kuongoza harakati za tabaka la wafanyakazi zilizokuwa zinaibuka.

Haya ndiyo mambo serikali ya kikoloni ilihofia na ndiyo ilikuwa sababu ya kumfanyia khiyana asiingie Makerere. Utawala wa kikoloni ulifahamu kuwa msukumo wa Kleist na mwanae aliyeelimika ungeipa Tanganyika uongozi uliokuwa unakosekana Tanganyika na pengine hata ndani ya Al Jamitul Islamiyya.

Ili kuifanya serikali iwasikilize mahali ambapo hapakuwa na sheria za kazi, ilibidi iwekwe mikakati ambayo ingeifanya serikali iweke sheria hizo katika vitabu vyake. Kamati ndogo ya siri iliundwa na Abdulwahid akatiwa ndani ya kamati hiyo ili kuongoza mgomo uliokusudiwa.

Kazi ya kamati hiyo ilikuwa kupanga na kuratibu mikakati ya kuitisha mgomo ambao ungelisaidia katika kuondoa ile dhulma iliyokuwepo. Makuli waliitisha mkutano pembeni kidogo mwa mji, mahali palipokuwa pakijulikana kama ‘’Shamba kwa Mohamed Abeid,’’ katika bonde la Msimbazi. Sehemu hii ilichaguliwa makhususi mbali na macho ya watu ili ipatikane faragha.

Makuli walikula kiapo na kusoma, ‘’Ahilil Badr,’’ ili kujikinga na unafiki, usaliti pamoja na shari ya vizabizabina wangeokataa kugoma. Ubani ulifukizwa na Qur’an ilisomwa. Wakijikinga na kiapo hicho cha mashahidi wa vita vya Badr na huku wakichochewa na ushujaa wa mashahidi waliokufa katika katika vita vya Badr wakipigana na washirikina wa Makka wakiwa pamoja na Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake), makuli walichagua tarehe 6 Septemba, 1947 kuwa ndiyo siku ya kuanza mgomo wao.

Mapema asubuhi moja kile kilichoanza kama mipango ya siri dhidi ya makampuni ya Wazungu bandarini, kililipuka na kuwa mapambano ya dhahiri. Watu katika mitaa jirani ya alipoishi akikaa Abdulwahid walikuwa hawajatoka vitandani mwao alifanjiri moja waliposikia vishindo na makelele vimetanda mtaani.

Makuli, baadhi yao wakiwa vidari wazi, walikuwa wameizingira nyumba ya Kleist, wakipiga makelele wakimtaka Abdulwahid atoke nje. Makuli wale walipiga kwata njia nzima kutoka bandarini huku wakitoa maneno ya kupinga ukoloni na wakiimba kupandisha morali zao.

Tukio hili halikuwa na kifani. Ilikuwa ni mara ya kwanza nchini Tanganyika kwa wananchi kushuhudia katika mitaa ya Dar es Salaam uasi wa dhahiri kama huo dhidi ya serikali ya kikoloni.

Abdulwahid, wakati ule kijana mdogo kabisa, akichungulia kupitia dirisha la chumba chake alichokuwa amelala, alishangazwa kuona umati mkubwa wa watu nje ya nyumba yao. Aliweza kuwatambua baadhi ya wenzake katika kamati ile ya siri iliyokuwa inapanga mipango ya mgomo. Alipotoka nje kuonana nao makuli wenye hasira walimfahamisha kuwa mgomo ulikuwa umeanza na wasingerudi kazini hadi madai yao yote yamekubaliwa…’’

Kisomo kingine nilichokutana nacho wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika kilifanyika Lindi na kisomo hiki kilifanywa na Sheikh Yusuf Badi lakini kwa kauli ya mpashaji habari wangu kisomo hiki kilikuwa Tawasul na katika waliohudhuria kwa kutajiwa majina yao walikuwa Suleiman Masudi Mnonji na Bi. Sharifa bint Mzee:

Bi. Shariffa Bint Mzee

‘’Nyerere aliporudi Lindi mwaka 1959, TANU ilikuwa ina nguvu sana na ilikuwa imekumba kila mtu. Wale watumishi wa serikali wengi wao wakiwa Wakristo, walio kuwa wakiibeza TANU mwaka 1955 kwa sababu ilikuwa ikiongozwa na Waislam ëwasiokuwa na elimu,í ukweli ulikuwa umewadhihirikia na sasa walikuwa wakionyesha heshima kwa chama.

Hawakuwa na khiyari na ilibidi waonyeshe heshima kwa sababu bwana mwenyewe, yaani serikali ya kikoloni, ilikuwa na heshima kwa TANU. Serikali ilikuwa imetambua kuwa dhamiri ya watu ya kukataa kutawaliwa haiwezi tena kupuuzwa. Nyerere alikuwa amelihutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa mara mbili, mara ya pili ikiwa mwaka 1957.

Ujumbe wa TANU ulikuwa wazi, watu wa Tanganyika walikuwa tayari kujitawala. Kila siku zilivyopita ndivyo TANU ilivyopata nguvu. Rashidi Salum Mpunga, dereva wa lori, aliweza kumshawishi na akafanikiwa kumuingiza TANU mmoja wa masheikh wenye kuheshimiwa sana mjini Lindi na mshairi maarufu, Sheikh Mohamed bin Yusuf Badi.

Sheikh Badi alipoingia TANU kwa ajili ya heshima yake na kukubalika na watu, idadi kubwa ya Waislam walimfuata na kukata kadi za TANU. Nyerere alipokuja Lindi kujadili tatizo la kura tatu na uongozi wa Jimbo la Kusini, Sheikh Yusufu Badi alimpokea Nyerere na madras yake, wanafunzi wakimwimbia Nyerere kasda na kumpigia dufu.

Kuanzia hapo sasa kila mtu alijiunga na TANU. Si Mponda wala Kanisa lilikuwa na uwezo wa kupambana na TANU kwa wakati ule. Polepole lakini na kwa kwa uhakika, TANU ilingia ndani ya maeneo ya Kikristo huko Songea, Masasi, Tunduru na Newala, nyumbani kwa Yustino Mponda.

Lakini matukio mawili ya kumbukumbu kubwa yalikuwa katika safari ya pili ya Nyerere alipozuru tena Jimbo la Kusini. Kumbukumbu ya kwanza ilikuwa tawaswil aliyosomewa Nyerere na Sheikh Yusuf Badi mwenyewe pamoja na Waislam aliowachagua yeye sheikh mwenyewe maalum kwa hafla hiyo, pamoja na waliochaguliwa na masheikh wengine.’’

Kisomo kingine na hiki ndicho maarufu ni kile kilichofanywa nyumbani kwa Jumbe Tambaza Upanga ambacho Mwalimu Nyerere mwenyewe amekieleza.
Kisomo cha nne kilifanyika Mnyanjani, Tanga mwaka wa 1958 wakati TANU ilipokuwa inakabiliwa na tatizo la Kura Tatu:

‘’Siku kadhaa kabla ya kusafiri kwenda Tabora kwenye ule mkutano mkuu wa mwaka wa TANU, Nyerere na Amos Kissenge, Kaimu Katibu Mwenezi wa TANU, walisafiri kwenda Tanga kushauriana na uongozi wa Kamati Kuu ya Taifa ya TANU Tanga kuhusu matatizo yaliyoletwa na Uchaguzi wa Kura Tatu. Mkutano huu baina ya Nyerere, Kissenge na ule uongozi wa Tanga ulikuwa wa siri sana.

Tanga iliwakilishwa na Hamisi Heri, Mwalimu Kihere, Abdallah Rashid Sembe, Ngíanzi Mohamed, Mustafa Shauri na Abdallah Makatta. Nyerere alizungumza waziwazi na kwa ithibati ya moyo wake. Nyerere alikiambia kikao kile kuwa amekuja Tanga kuomba wamuunge mkono kwa sababu ilikuwa ni matakwa yake TANU lazima ishiriki katika ule uchaguzi wa kura tatu uliokuwa unakaribia hata masharti yakiwaje.

Nyerere aliuambia uongozi wa Tanga uliokuwa ukimsikiliza kwa makini kuwa alikuwa amekuja kwao kwa sababu watu wa Tanga wanajulikana kwa ufasaha wa lugha na kwa uwezo wao wa kuzungumza vizuri. Nyerere alisema angehitaji hiki kipaji adimu cha watu wa Tanga kuunga mkono msimamo wake huko Tabora.

Nyerere alitoa hoja kwamba TANU lazima iingie katika uchaguzi kwa sababu kuususia ni sawasawa na kukipa chama hasimu, UTP ushindi bila jasho kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria. TANU ingedhoofika na hivyo ingekosa sauti katika maamuzi yatakayotolewa na serikali katika siku zijazo.

Sheikh Abdallah Rashid Sembe

Kufichuka kwa msimamo wa Nyerere wa kutaka TANU iingie kaatika kura tatu kulishtua uongozi wa Tanga. Majadiliano makali yalifuata uongozi wa Tanga ukionyesha upinzani wao kwa msimamo wa Nyerere. Baada ya majadiliano ya muda mrefu Nyerere alifanikiwa kuwashawishi wote wawili, Hamisi Heri na Mwalimu Kihere ambao ndiyo walikuwa wapinzani wakubwa wa msimamo wa Nyerere na uchaguzi wa kura tatu.

Nyerere aliutahadharisha uongozi wa Tanga kuwa agenda ya kura tatu itakapokuja anatabiri kupata upinzani mkali kutoka katika majimbo. Huko Tanga kwenyewe, TANU ilikuwa ikikabiliwa na upinzani mkali kutoka UTP na serikali. Matawi kadhaa yalikuwa yamepigwa marufuku. UTP ilikuwa na nguvu Tanga kwa sababu wanachama wake wengi walikuwa wakimiliki mashamba ya mkonge katika jimbo hilo.

Kwa ajili hii chama kilikuwa kinaelemewa na mashambulizi kutoka wa wapinzani. Wakati huo Tanga ilikuwa imetoa viongozi wenye uwezo lakini wote walikuwa wamehamishiwa makao makuu mjini Dar es Salaam. Wapangaji mikakati wazuri kama Peter Mhando alikuwa amehamishiwa Dar es Salaam na kutoka hapo alipelekwa Tabora ambako si muda mrefu akafa.

Elias Kissenge vilevile alihamishiwa makao makuu kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa TANU baada ya Oscar Kambona aliyekuwa ameshika nafasi hiyo kwenda Uingereza kwa ajili ya masomo. Uongozi wa TANU Tanga hata baada ya kujadili mbinu waliyopanga na huku Nyerere akielekeza mikakati ambayo Mwalimu Kihere na Abdallah Rashid Sembe wataitekeleza Tabora, bado uongozi ule ulikuwa na wasiwasi wa mafanikio ya mpango huo. Kwa ajili ya wasiwasi huu, viongozi wa TANU wa Tanga walimuomba Nyerere wawe pamoja ili ifanywe tawaswil waombe msaada wa Allah awape ushindi dhidi yaa vitimbi vya Waingereza.

Maili tatu kutoka Tanga kipo kijiji cha Mnyanjani ambako kulikuwako na tawi la TANU lililokuwa na nguvu sana likiongozwa na Mmaka Omari kama mwenyekiti na Akida Boramimi bin Dai akiwa katibu. Mmaka alikuwa kijana aliyekuwa akiendesha mgahawa pale kijijini na Akida bin Dai alikuwa mwashi.

Akida aliongoza tawi la vijana wa TANU ambalo baadae lilikuja kujulikana kama Tanga Volunteer Corps (TVC). TVC ilikuwa sawasawa na Bantu Group, ambayo wakati huo ilikuwa imekwishaanzishwa huko Dar es Salaam na Tabora. Vikundi hivi mbali na kufanya shughuli za propaganda na kuhamasisha wananchi halikadhalika viliifanyia TANU ujasusi.

Nyerere na Kissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani na tawaswil ikasomwa. Waliohudhuria kisomo hicho walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana aliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimi bin Dai na Mmaka Omari. Aliyechaguliwa kusoma Quran Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh Ali Kombora…’’

Mwalimu Kihere
 
These religious acrobats get no one no where.

Kama hizi albadr ni kitu, wenye dini yao Waarabu wasingekua wanabinuliwa binuliwa na Waamerika kila kukicha.

Usije na stories za hurricanes.
Uhuru na Umoja,
Tatizo la historia ya uhuru wa Tanganyika imewaghadhibisha wengi na
naona wewe ni mmojawapo.

Wala hapakuwa na ''gymnastics,'' zozote wakati mimi nilipokuwa natafiti
na mwishowe kuandika kitabu cha Abdul Sykes.

Wala mimi si wa kwanza mathalan kukuta katika utafiti visomo kutumika
kama moja ya njia za kupambana na ukoloni.

''Utenzi wa Kutamalaki kwa Wadachi Mrima,'' ulioandikwa na Hemed
Abdallah bin Said el Buhry
kuhusu vita ya watu wa pwani dhidi ya
Wajerumani katika mwaka wa 1888 - 1889, katika utenzi huo visomo
vimeelezwa.

Huu ulikuwa wakati Bushiri bin Salim alipokuwa akipambana na
Wajerumani.

BUSHIRI%2BBIN%2BSALIM%2BAL%2BHARITH.jpg

Bushiri bin Salim

Halikadhalika ukimsoma Iliffe katika, ''A History of Dockworkers of
Dar es Salaam,'' katika Tanzania Notes and Records, 71 (1970) uk.
130 kaeleza kuhusu hivi visomo vilivyofanyika 1947 wakati wa harakati
za mgomo wa makuli kati ya 1947 - 1950.

El Buhry na Iliffe hawakuwa katika ''circus,'' yoyote bali walikuwa
wao wanaeleza na kuandika kile walichokikuta katika utafiti wao.

Labda nikufahamishe kuwa haya yote ya hivi visomo vinakwenda na
Uislam na hili ndilo lililokuchoma wewe na mfano wa wewe kwa kuwa
hampendi kusoma juhudi za Waislam katika historia ya uhuru wa
Tanganyika.

Lakini tutafanya nini na hii ndiyo historia ya Tanganyika?
Kukataa kuwa kuwa haya hayakuwapo ni muhali mkubwa sana.

Kwa kuhitimisha ningependa kukueleza kuwa wala haya usomayo
katika historia ya uhuru wa Tanganyika hayana uhusiano wowote
hata kwa mbali na siasa za Waarabu.

Nakusihi utustahamilie tunapoandika historia za wazee wetu.
Wakuja na ''hurricane,'' si Mohamed Said.

Get to know him.
Yeye Mohamed Said huja na tufani khasa.

fVtkpNYqneFXjfgR_qeK1G3qX1DsjldVxNWteKWlbgFkoSmND0nVpfRMOEfBJ2sWefYxot74mdcAjZ5isZEDybdUqpPVG15tpoTh3-nAaglZpoRmM8AHWGXZiD1KrUqew4FeZK9fgAifQGAciUVe_PiUSqtdS0eu5nELmnJGmPVW8L2OGM29mVq5CreK7fYf2mo1IzPGdQlsHNK5pAKC0Dsq1ailKyhIAQ68vWgsFbeWH7sznh5fCT6RGLm0AtCJh0O3CK-fQ6HSPRKfkLDbVLJA409UkWDrNd1wt_7_YQ0HM2Z8jxfpFyH1dI4Ga2WeFlWMZkhyKYMMzFb_TSG1eZZRrbgPWoYoB6ysSixbj-N_yrC2KmvF9rJT_v4AkqTpU_JnoTm2ec0IJ3Z9Po5-yVvVdExKZ1KTsKKf87yaxoXoZSiX5cshiqNBoxRoKzEl4prrlUldy9rJxkOos7E7chXvL1JAshPYLe0IJSD8SnvxNc0Oq5qvXZI004UQnX0g71piNphrY1j0cT8WLi-6kXiRAWEmlvgJVa1AkJNZQ5twMEFK5zRptkbjJ-_aDWZp8kh0SoVfo3A_KwlMSIXY-XqlFI8vjmiymcxVhtW7aek=w420-h629-no

Marehemu Sheikh Zukheri El Bukhry kitukuu cha Hemed
Abdallah bin Said el Bukhry
 
El Buhry na Iliffe hawakuwa katika ''circus,'' yoyote bali waikuwa
wao wanaeleza na kuandika kile walichokikuta katika utafiti wao.

Labda nikufahamishe kuwa haya yote ya hivi visomo vinakwenda na
Uislamna hili ndilo lililokuchoma wewe na mfano wa wewe kwa kuwa
hampendi kusoma juhudu za Waislam katika historia ya uhuru wa
Tanganyika.

Lakini tutafanya nini na hii ndiyo historia ya Tanganyika?
Kukataa kuwa kuwa haya hayakuwapo ni muhali mkubwa sana.

Kwa kuhitimisha ningependa kukueleza kuwa wala haya usomayo
katika historia ya uhuru wa Tanganyika hayana uhusiano wowote
hata kwa mbali na siasa za Waarabu.

Nakusihi utustahamilie tunapoandika historia za wazee wetu.

fVtkpNYqneFXjfgR_qeK1G3qX1DsjldVxNWteKWlbgFkoSmND0nVpfRMOEfBJ2sWefYxot74mdcAjZ5isZEDybdUqpPVG15tpoTh3-nAaglZpoRmM8AHWGXZiD1KrUqew4FeZK9fgAifQGAciUVe_PiUSqtdS0eu5nELmnJGmPVW8L2OGM29mVq5CreK7fYf2mo1IzPGdQlsHNK5pAKC0Dsq1ailKyhIAQ68vWgsFbeWH7sznh5fCT6RGLm0AtCJh0O3CK-fQ6HSPRKfkLDbVLJA409UkWDrNd1wt_7_YQ0HM2Z8jxfpFyH1dI4Ga2WeFlWMZkhyKYMMzFb_TSG1eZZRrbgPWoYoB6ysSixbj-N_yrC2KmvF9rJT_v4AkqTpU_JnoTm2ec0IJ3Z9Po5-yVvVdExKZ1KTsKKf87yaxoXoZSiX5cshiqNBoxRoKzEl4prrlUldy9rJxkOos7E7chXvL1JAshPYLe0IJSD8SnvxNc0Oq5qvXZI004UQnX0g71piNphrY1j0cT8WLi-6kXiRAWEmlvgJVa1AkJNZQ5twMEFK5zRptkbjJ-_aDWZp8kh0SoVfo3A_KwlMSIXY-XqlFI8vjmiymcxVhtW7aek=w420-h629-no

Marehemu Sheikh Zukheri El Bukhry kitukuu cha Hemed
Abdallah bin Said el Bukhry

Mohamed Said

Mimi sina habari na historia ya nani kafanya nini. Uhuru wa Tanzania/Tanganyika haukupatikana kwa vita.

Pili, mimi sichomwi na chochote juu ya mijadala yako ya kidini zaidi ya kuona ya kua wewe ni Adui mkubwa wa Amani, Mshikamano na Usalama wa Tanzania na Watanzania ukiwemo wewe.

Najua wajua ya kuwa Watu wenye akili timamu, hawajisaidii sebuleni am vyumba vya kulala; wenye akili timamu huenda Malwatoni aka Msalani.

Mimi niliandika inshu za Abadr baada ya kuona ni kwa muda sasa inshu hii imeshika hatam baada ya Wasioitakia mema inchi hii kama wewe kutaka kumuua Lisu ili ionekane ni Serikali yetu pendwa inayosomamia haki za wanyonge na yenye nia ya dhati kuleta maendeleo kwa Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa ama uhuru wetu wa kuabudu.

Nimeongea swala la Albadr na Waaarabu sio kwakua wanauhusiano wowote na uhuru na Tanganyika [kama unavyependa kuandika ila mimi naiita nchi yangu pendwa Tanzania] bali ni juu ya prejudicial beliefs wengi walizo nazo juu ya imani zetu za kidini.

Ndio maana nilitoa mfano wa Nguvu ya Albadr na Vita visivyoisha kati ya Waraabu na Waamerika na manyanyaso ya Taifa la Palestina--kama albadr inafanya kazi ilitakiwa ianze huko, inshaalah.

HITIMISHO

No matter how intellect you may be or claim to be, the matter of fact is, no one in this world has intrinsic aptitude to perceive anyone’s mind by introspection. For this reason, I humbly beseech you to desist from arbitrary presupposition(s) [“historia ya uhuru wa Tanganyika imewaghadhibisha wengi nanaona wewe ni mmojawapo]

Mimi sio mtu wa ghadhab wala sighadhibishwi na maandishi ambayo kwa kiasi kikubwa ni private opinion(s) za mtu na wote tuna uhuru wa kufanya hivyo.
 
Ungekuwa huchomwi na historia hii usingekuja na lugha hii uliyokujanayo.

Hii nchi ni yetu sote na mimi natembea kifua mbele kwa sababu babu yangu Salum Abdallah ni mmoja wa wazalendo waliopambana na ukoloni kwa hali na mali na ukipenda nitakuwekea hapa historia yake toka 1947 hadi uhuru ulipopatikana.

Hayo mengine wala sina haja ya kukujibu.
 
Asante mzee Saidi kwa utafiti mzito . Historia haifutiki hata vitabu vilivyonukuu vikichomwa moto au kuandikwa upya kuziba baadhi ya matukio - itajitokeza tu na baadhi ya watu wanakufa kwa kihoro ukweli ukijitokeza.
 
Kama ulivyosema nchi hii ni yetu sote na na kila mtu anatembea kifua mbele.

Inshu wewe kutembea kifua mbele kwa kua eti babu yako alikua karaani TANU haina mshiko or kutaka kuaminisha umma umuhimu wa babu yako kwenye nchi hii ni kupoteza wakati.

Nchi hii, watu wengi wameifanyia makubwa na hawatambi wala kujitembeza.

Tuna Baba zetu, ndugu, jamaa na marafiki waliofia uwanja wa mapambano kwaajili ya Taifa hili.

Hizi ngonjera hazina tija kwa Taifa hili ambalo linaandika historia mpya ya ukombozi na uhuru wa kweli dhidi ya vita ya UMASIKINI, MARADHI NA UJINGA.

Hizo nyingine ni Ngonjera or Mazungumzo baada ya habari.
 
Babu yangu Salum Abdallah hakuwa karani wa TANU.

Soma hapo chini umjue ni bandiko niliweka hapa kumjibu Nanren:
Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu Salum Abdallah.

Hakuwekwa kwa ajili ya dini.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955 Kasanga
Tumbo
akiwa katibu.

TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.

Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.

Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh Kenya.

Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya wanajeshi
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.

Kuwekwa kwao ndani ilikuwa Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.

Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu Mwalimu Nyerere kwa
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa
wakisikilizwa na wananchi.

Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962 Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.

Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.

Nyerere hakufurahishwa na yeye.

Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na
kilimo cha tumbuku Urambo.

Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.

Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.

Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.

Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.

Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.

Uhuru na Umoja,
Sasa nasubiri kusoma hayo makubwa ya watu wako ambayo ni makubwa kupita
aliyofanya babu yangu unaemkejeli.

Ikiwa historia hii katika kitabu cha Abdul Sykes ni ngonjera hiyo ngonjera itakuwa
nini?
 
Asante mzee Saidi kwa utafiti mzito . Historia haifutiki hata vitabu vilivyonukuu vikichomwa moto au kuandikwa upya kuziba baadhi ya matukio - itajitokeza tu na baadhi ya watu wanakufa kwa kihoro ukweli ukijitokeza.
Percival,
Si hulka yangu kumjibu mtu kwa ukali.
Huyu kwa kuwa kaja na kibri, kejeli na jeuri kisha kujifanya yeye ni Charles Dickens nimeona nimwonyeshe ili siku nyingine aje na adabu zake kamili.
 
Mimi wanijua vyema na si mara ya kwanza tunagongana mitazamo kwenye mada zako humu.

Si mara ya kwanza, ya pili, ya tatu wala ya nne kutofautiana na mara nyingi.

Na sijawahi badilika, ni kule tu kwenye uzi wa Lt Gen John Walden na Uzi wa Sir Andy Chande.

Mimi nilikua namsoma Andy Chande nikiwa mtoto sana kwenye Diaries za Bandari, kama Chairman wa board of directors, madirectors wa kipindi hicho kama: Janguo, Cholobi.

Cholobi ni jina nalokumbuka miaka hiyo ila Janguo siwezi sahau kwakua alikua mkuu wa kazi wa baba mlezi wangu: General Manager wa Bandari: Joseph N Kimaro, kipindi wewe wafanya kazi Bandari, Masoko chini ya Dr Ramadhan Dau.

Baba mzazi alikua Director hapo hapo Bandari, AMI, CMB.

So yapo maeneo tunaweza twaelewana na yapo hatuwezi enda sawa.
 
kipanya.jpg

Wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes nilikutana na matokeo manne ambayo wananchi walijikusanya na kufanya visomo au dua kujikinga na dhulma za ukoloni wa Waingereza.

Katika matukio haya manne ya kumuomba Mungu ni tukio moja tu ndilo wafanyaji kisomo walichobainisha kuwa inayosomwa ni ‘’Halal Badr’’ neno ambalo hivi sasa limekuwa maarufu midomoni mwa watu wengi baada ya kuelezwa kuwa kutasomwa Halal Badr makhsusi kufuatia jaribio la kumuua Mbunge wa Singida Mashariki, Mheshimiwa Tundu Lissu.

Nitarudi nyuma kiasi cha nuru karne na zaidi kuangalia nafasi ya visomo katika kutafuta haki. Nitaaanza kwa kueleza mazingira yaliyokuwapo wakati wa ukoloni hadi kusababisha wananchi kumgeukia Mungu na kutaka msaada wake na hivyo kusoma Halal Badr.

Nakuwekea msomaji wangu yale niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes, kitabu ambacho ndani yake nimejaribu kueleza historia ya uhuru wa na kuandika kuhusu Halal Badr ili kwa yule ambae ni mgeni katika mambo haya apate picha kamili na Tanganyika ili uweze kuona ilikuwa na kujua ni wakati gani wananchi waliamua kufanya dua iwe Halal Badr au kisomo kingine kama kinga yao dhidi ya nguvu ambayo wao waliona ni Mungu pekee ndiye angeliweza kuwapa nusra.

Labda tujiulize imekuwaje leo baada ya zaidi ya nusu karne wananchi wanarejea katika mbinu ambazo wengi wanaona kuwa kuzirejea tena katika Tanzaia huru ni kitu ambacho kidogo kinashangaza hasa kwa kuwa dini kama inavyoelezwa kuwa haina nafasi katika uendeshaji wa serikali.

Naanza kwa kukuwekea hapo chini mara yangu ya kwanza nilipokutana na huu makakati ambao kwa hakika ulikuwa mpya katika mbinu za kudai haki kwa kukueleza vuguvugu la makuli katika bandari ya Dar es Salaam pale walipoamua kupambana na dhulma za wakoloni kwa kusoma Halal Badr mwaka wa 1947:

‘’…kidogo kidogo Kleist alianza kumkabidhi Abdulwahid kazi za African Association na mara akawa msaidizi wa baba yake katika siasa za Dar es Salaam. Ilikuwa katika kutimiza haya ndipo Abdulwahid akajikuta anahusika na ule mgogoro wa makuli ulioibuka bandarini Dar es Salaam ambao ulikuwa ukichemka pole pole chini kwa chini kwa muda mrefu tangu kumalizika kwa vita.

Hatimaye, Abdulwahid alihusika na harakati za siri za wafanyakazi bandarini ambao, wakiwa wamechoshwa na sheria za kazi za ukandamizaji na wakiwa wamechoka kunyonywa na makampuni ya meli, walikuwa wanapanga kuitisha mgomo.

Chama cha African Association ndicho kiliwakilisha maslahi ya wananchi wa Tanganyika na kimya kimya kiliunga mkono zile harakati za chini kwa chini za wafanyakazi katika kutafuta haki zao. Abdulwahid, kijana mdogo mwenye elimu na akiwa karibu zaidi na uongozi wa African Association kuliko Mwafrika yoyote pale mjini, alichaguliwa kuongoza harakati za tabaka la wafanyakazi zilizokuwa zinaibuka.

Haya ndiyo mambo serikali ya kikoloni ilihofia na ndiyo ilikuwa sababu ya kumfanyia khiyana asiingie Makerere. Utawala wa kikoloni ulifahamu kuwa msukumo wa Kleist na mwanae aliyeelimika ungeipa Tanganyika uongozi uliokuwa unakosekana Tanganyika na pengine hata ndani ya Al Jamitul Islamiyya.

Ili kuifanya serikali iwasikilize mahali ambapo hapakuwa na sheria za kazi, ilibidi iwekwe mikakati ambayo ingeifanya serikali iweke sheria hizo katika vitabu vyake. Kamati ndogo ya siri iliundwa na Abdulwahid akatiwa ndani ya kamati hiyo ili kuongoza mgomo uliokusudiwa.

Kazi ya kamati hiyo ilikuwa kupanga na kuratibu mikakati ya kuitisha mgomo ambao ungelisaidia katika kuondoa ile dhulma iliyokuwepo. Makuli waliitisha mkutano pembeni kidogo mwa mji, mahali palipokuwa pakijulikana kama ‘’Shamba kwa Mohamed Abeid,’’ katika bonde la Msimbazi. Sehemu hii ilichaguliwa makhususi mbali na macho ya watu ili ipatikane faragha.

Makuli walikula kiapo na kusoma, ‘’Ahilil Badr,’’ ili kujikinga na unafiki, usaliti pamoja na shari ya vizabizabina wangeokataa kugoma. Ubani ulifukizwa na Qur’an ilisomwa. Wakijikinga na kiapo hicho cha mashahidi wa vita vya Badr na huku wakichochewa na ushujaa wa mashahidi waliokufa katika katika vita vya Badr wakipigana na washirikina wa Makka wakiwa pamoja na Mtume Muhammad (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake), makuli walichagua tarehe 6 Septemba, 1947 kuwa ndiyo siku ya kuanza mgomo wao.

Mapema asubuhi moja kile kilichoanza kama mipango ya siri dhidi ya makampuni ya Wazungu bandarini, kililipuka na kuwa mapambano ya dhahiri. Watu katika mitaa jirani ya alipoishi akikaa Abdulwahid walikuwa hawajatoka vitandani mwao alifanjiri moja waliposikia vishindo na makelele vimetanda mtaani.

Makuli, baadhi yao wakiwa vidari wazi, walikuwa wameizingira nyumba ya Kleist, wakipiga makelele wakimtaka Abdulwahid atoke nje. Makuli wale walipiga kwata njia nzima kutoka bandarini huku wakitoa maneno ya kupinga ukoloni na wakiimba kupandisha morali zao.

Tukio hili halikuwa na kifani. Ilikuwa ni mara ya kwanza nchini Tanganyika kwa wananchi kushuhudia katika mitaa ya Dar es Salaam uasi wa dhahiri kama huo dhidi ya serikali ya kikoloni.

Abdulwahid, wakati ule kijana mdogo kabisa, akichungulia kupitia dirisha la chumba chake alichokuwa amelala, alishangazwa kuona umati mkubwa wa watu nje ya nyumba yao. Aliweza kuwatambua baadhi ya wenzake katika kamati ile ya siri iliyokuwa inapanga mipango ya mgomo. Alipotoka nje kuonana nao makuli wenye hasira walimfahamisha kuwa mgomo ulikuwa umeanza na wasingerudi kazini hadi madai yao yote yamekubaliwa…’’

Kisomo kingine nilichokutana nacho wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika kilifanyika Lindi na kisomo hiki kilifanywa na Sheikh Yusuf Badi lakini kwa kauli ya mpashaji habari wangu kisomo hiki kilikuwa Tawasul na katika waliohudhuria kwa kutajiwa majina yao walikuwa Suleiman Masudi Mnonji na Bi. Sharifa bint Mzee:

Bi. Shariffa Bint Mzee

‘’Nyerere aliporudi Lindi mwaka 1959, TANU ilikuwa ina nguvu sana na ilikuwa imekumba kila mtu. Wale watumishi wa serikali wengi wao wakiwa Wakristo, walio kuwa wakiibeza TANU mwaka 1955 kwa sababu ilikuwa ikiongozwa na Waislam ëwasiokuwa na elimu,í ukweli ulikuwa umewadhihirikia na sasa walikuwa wakionyesha heshima kwa chama.

Hawakuwa na khiyari na ilibidi waonyeshe heshima kwa sababu bwana mwenyewe, yaani serikali ya kikoloni, ilikuwa na heshima kwa TANU. Serikali ilikuwa imetambua kuwa dhamiri ya watu ya kukataa kutawaliwa haiwezi tena kupuuzwa. Nyerere alikuwa amelihutubia Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa mara mbili, mara ya pili ikiwa mwaka 1957.

Ujumbe wa TANU ulikuwa wazi, watu wa Tanganyika walikuwa tayari kujitawala. Kila siku zilivyopita ndivyo TANU ilivyopata nguvu. Rashidi Salum Mpunga, dereva wa lori, aliweza kumshawishi na akafanikiwa kumuingiza TANU mmoja wa masheikh wenye kuheshimiwa sana mjini Lindi na mshairi maarufu, Sheikh Mohamed bin Yusuf Badi.

Sheikh Badi alipoingia TANU kwa ajili ya heshima yake na kukubalika na watu, idadi kubwa ya Waislam walimfuata na kukata kadi za TANU. Nyerere alipokuja Lindi kujadili tatizo la kura tatu na uongozi wa Jimbo la Kusini, Sheikh Yusufu Badi alimpokea Nyerere na madras yake, wanafunzi wakimwimbia Nyerere kasda na kumpigia dufu.

Kuanzia hapo sasa kila mtu alijiunga na TANU. Si Mponda wala Kanisa lilikuwa na uwezo wa kupambana na TANU kwa wakati ule. Polepole lakini na kwa kwa uhakika, TANU ilingia ndani ya maeneo ya Kikristo huko Songea, Masasi, Tunduru na Newala, nyumbani kwa Yustino Mponda.

Lakini matukio mawili ya kumbukumbu kubwa yalikuwa katika safari ya pili ya Nyerere alipozuru tena Jimbo la Kusini. Kumbukumbu ya kwanza ilikuwa tawaswil aliyosomewa Nyerere na Sheikh Yusuf Badi mwenyewe pamoja na Waislam aliowachagua yeye sheikh mwenyewe maalum kwa hafla hiyo, pamoja na waliochaguliwa na masheikh wengine.’’

Kisomo kingine na hiki ndicho maarufu ni kile kilichofanywa nyumbani kwa Jumbe Tambaza Upanga ambacho Mwalimu Nyerere mwenyewe amekieleza.
Kisomo cha nne kilifanyika Mnyanjani, Tanga mwaka wa 1958 wakati TANU ilipokuwa inakabiliwa na tatizo la Kura Tatu:

‘’Siku kadhaa kabla ya kusafiri kwenda Tabora kwenye ule mkutano mkuu wa mwaka wa TANU, Nyerere na Amos Kissenge, Kaimu Katibu Mwenezi wa TANU, walisafiri kwenda Tanga kushauriana na uongozi wa Kamati Kuu ya Taifa ya TANU Tanga kuhusu matatizo yaliyoletwa na Uchaguzi wa Kura Tatu. Mkutano huu baina ya Nyerere, Kissenge na ule uongozi wa Tanga ulikuwa wa siri sana.

Tanga iliwakilishwa na Hamisi Heri, Mwalimu Kihere, Abdallah Rashid Sembe, Ngíanzi Mohamed, Mustafa Shauri na Abdallah Makatta. Nyerere alizungumza waziwazi na kwa ithibati ya moyo wake. Nyerere alikiambia kikao kile kuwa amekuja Tanga kuomba wamuunge mkono kwa sababu ilikuwa ni matakwa yake TANU lazima ishiriki katika ule uchaguzi wa kura tatu uliokuwa unakaribia hata masharti yakiwaje.

Nyerere aliuambia uongozi wa Tanga uliokuwa ukimsikiliza kwa makini kuwa alikuwa amekuja kwao kwa sababu watu wa Tanga wanajulikana kwa ufasaha wa lugha na kwa uwezo wao wa kuzungumza vizuri. Nyerere alisema angehitaji hiki kipaji adimu cha watu wa Tanga kuunga mkono msimamo wake huko Tabora.

Nyerere alitoa hoja kwamba TANU lazima iingie katika uchaguzi kwa sababu kuususia ni sawasawa na kukipa chama hasimu, UTP ushindi bila jasho kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria. TANU ingedhoofika na hivyo ingekosa sauti katika maamuzi yatakayotolewa na serikali katika siku zijazo.

Sheikh Abdallah Rashid Sembe

Kufichuka kwa msimamo wa Nyerere wa kutaka TANU iingie kaatika kura tatu kulishtua uongozi wa Tanga. Majadiliano makali yalifuata uongozi wa Tanga ukionyesha upinzani wao kwa msimamo wa Nyerere. Baada ya majadiliano ya muda mrefu Nyerere alifanikiwa kuwashawishi wote wawili, Hamisi Heri na Mwalimu Kihere ambao ndiyo walikuwa wapinzani wakubwa wa msimamo wa Nyerere na uchaguzi wa kura tatu.

Nyerere aliutahadharisha uongozi wa Tanga kuwa agenda ya kura tatu itakapokuja anatabiri kupata upinzani mkali kutoka katika majimbo. Huko Tanga kwenyewe, TANU ilikuwa ikikabiliwa na upinzani mkali kutoka UTP na serikali. Matawi kadhaa yalikuwa yamepigwa marufuku. UTP ilikuwa na nguvu Tanga kwa sababu wanachama wake wengi walikuwa wakimiliki mashamba ya mkonge katika jimbo hilo.

Kwa ajili hii chama kilikuwa kinaelemewa na mashambulizi kutoka wa wapinzani. Wakati huo Tanga ilikuwa imetoa viongozi wenye uwezo lakini wote walikuwa wamehamishiwa makao makuu mjini Dar es Salaam. Wapangaji mikakati wazuri kama Peter Mhando alikuwa amehamishiwa Dar es Salaam na kutoka hapo alipelekwa Tabora ambako si muda mrefu akafa.

Elias Kissenge vilevile alihamishiwa makao makuu kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa TANU baada ya Oscar Kambona aliyekuwa ameshika nafasi hiyo kwenda Uingereza kwa ajili ya masomo. Uongozi wa TANU Tanga hata baada ya kujadili mbinu waliyopanga na huku Nyerere akielekeza mikakati ambayo Mwalimu Kihere na Abdallah Rashid Sembe wataitekeleza Tabora, bado uongozi ule ulikuwa na wasiwasi wa mafanikio ya mpango huo. Kwa ajili ya wasiwasi huu, viongozi wa TANU wa Tanga walimuomba Nyerere wawe pamoja ili ifanywe tawaswil waombe msaada wa Allah awape ushindi dhidi yaa vitimbi vya Waingereza.

Maili tatu kutoka Tanga kipo kijiji cha Mnyanjani ambako kulikuwako na tawi la TANU lililokuwa na nguvu sana likiongozwa na Mmaka Omari kama mwenyekiti na Akida Boramimi bin Dai akiwa katibu. Mmaka alikuwa kijana aliyekuwa akiendesha mgahawa pale kijijini na Akida bin Dai alikuwa mwashi.

Akida aliongoza tawi la vijana wa TANU ambalo baadae lilikuja kujulikana kama Tanga Volunteer Corps (TVC). TVC ilikuwa sawasawa na Bantu Group, ambayo wakati huo ilikuwa imekwishaanzishwa huko Dar es Salaam na Tabora. Vikundi hivi mbali na kufanya shughuli za propaganda na kuhamasisha wananchi halikadhalika viliifanyia TANU ujasusi.

Nyerere na Kissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani na tawaswil ikasomwa. Waliohudhuria kisomo hicho walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana aliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimi bin Dai na Mmaka Omari. Aliyechaguliwa kusoma Quran Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh Ali Kombora…’’

Mwalimu Kihere
unaweka mapicha tu ya watu na 'vibagarashia' vilivyotoboka
weka ushahid wa maandishi wacha hizo ngano zako,unakuja kuleta stor za kusimuliwa hadith njoo ...uongo njoo

sasa kama kisomo dawa nyerere asingeenda uno babu zako wangesoma tu wazungu waondoke

toka uhuru mpaka sasa, ulivyozaliwa mpaka leo povu linakutoka serikali inawaonea kasome kisono kitatue matatizo yenu!
 
Uhuru na Umoja,
Tatizo la historia ya uhuru wa Tanganyika imewaghadhibisha wengi na
naona wewe ni mmojawapo.

Wala hapakuwa na ''gymnastics,'' zozote wakati mimi nilipokuwa natafiti
na mwishowe kuandika kitabu cha Abdul Sykes.

Wala mimi si wa kwanza mathalan kukuta katika utafiti visomo kutumika
kama moja ya njia za kupambana na ukoloni.

''Utenzi wa Kutamalaki kwa Wadachi Mrima,'' ulioandikwa na Hemed
Abdallah bin Said el Buhry
kuhusu vita ya watu wa pwani dhidi ya
Wajerumani katika mwaka wa 1888 - 1889, katika utenzi huo visomo
vimeelezwa.

Huu ulikuwa wakati Bushiri bin Salim alipokuwa akipambana na
Wajerumani.

BUSHIRI%2BBIN%2BSALIM%2BAL%2BHARITH.jpg

Bushiri bin Salim

Halikadhalika ukimsoma Iliffe katika, ''A History of Dockworkers of
Dar es Salaam,'' katika Tanzania Notes and Records, 71 (1970) uk.
130 kaeleza kuhusu hivi visomo vilivyofanyika 1947 wakati wa harakati
za mgomo wa makuli kati ya 1947 - 1950.

El Buhry na Iliffe hawakuwa katika ''circus,'' yoyote bali walikuwa
wao wanaeleza na kuandika kile walichokikuta katika utafiti wao.

Labda nikufahamishe kuwa haya yote ya hivi visomo vinakwenda na
Uislam na hili ndilo lililokuchoma wewe na mfano wa wewe kwa kuwa
hampendi kusoma juhudu za Waislam katika historia ya uhuru wa
Tanganyika.

Lakini tutafanya nini na hii ndiyo historia ya Tanganyika?
Kukataa kuwa kuwa haya hayakuwapo ni muhali mkubwa sana.

Kwa kuhitimisha ningependa kukueleza kuwa wala haya usomayo
katika historia ya uhuru wa Tanganyika hayana uhusiano wowote
hata kwa mbali na siasa za Waarabu.

Nakusihi utustahamilie tunapoandika historia za wazee wetu.
Wakuja na ''hurricane,'' si Mohamed Said.

Get to know him.
Yeye Mohamed Said huja na tufani khasa.

fVtkpNYqneFXjfgR_qeK1G3qX1DsjldVxNWteKWlbgFkoSmND0nVpfRMOEfBJ2sWefYxot74mdcAjZ5isZEDybdUqpPVG15tpoTh3-nAaglZpoRmM8AHWGXZiD1KrUqew4FeZK9fgAifQGAciUVe_PiUSqtdS0eu5nELmnJGmPVW8L2OGM29mVq5CreK7fYf2mo1IzPGdQlsHNK5pAKC0Dsq1ailKyhIAQ68vWgsFbeWH7sznh5fCT6RGLm0AtCJh0O3CK-fQ6HSPRKfkLDbVLJA409UkWDrNd1wt_7_YQ0HM2Z8jxfpFyH1dI4Ga2WeFlWMZkhyKYMMzFb_TSG1eZZRrbgPWoYoB6ysSixbj-N_yrC2KmvF9rJT_v4AkqTpU_JnoTm2ec0IJ3Z9Po5-yVvVdExKZ1KTsKKf87yaxoXoZSiX5cshiqNBoxRoKzEl4prrlUldy9rJxkOos7E7chXvL1JAshPYLe0IJSD8SnvxNc0Oq5qvXZI004UQnX0g71piNphrY1j0cT8WLi-6kXiRAWEmlvgJVa1AkJNZQ5twMEFK5zRptkbjJ-_aDWZp8kh0SoVfo3A_KwlMSIXY-XqlFI8vjmiymcxVhtW7aek=w420-h629-no

Marehemu Sheikh Zukheri El Bukhry kitukuu cha Hemed
Abdallah bin Said el Bukhry
sasa hiy pc ya huyo mjukuu ya nn?
sawa na humu ukimaliza koment uanze kuweka picha ya makongoro o madaraka nyerere!

au kisa kavaa kanzu ya kusomea kisomo...
 
Mimi wanijua vyema na si mara ya kwanza tunagongana mitazamo kwenye mada zako humu.

Si mara ya kwanza, ya pili, ya tatu wala ya nne kutofautiana na mara nyingi.

Na sijawahi badilika, ni kule tu kwenye uzi wa Lt Gen John Walden na Uzi wa Sir Andy Chande.

Mimi nilikua namsoma Andy Chande nikiwa mtoto sana kwenye Diaries za Bandari, kama Chairman wa board of directors, madirectors wa kipindi hicho kama: Janguo, Cholobi.

Cholobi ni jina nalokumbuka miaka hiyo ila Janguo siwezi sahau kwakua alikua mkuu wa kazi wa baba mlezi wangu: General Manager wa Bandari: Joseph N Kimaro, kipindi wewe wafanya kazi Bandari, Masoko chini ya Dr Ramadhan Dau.

Baba mzazi alikua Director hapo hapo Bandari, AMI, CMB.

So yapo maeneo tunaweza twaelewana na yapo hatuwezi enda sawa.
Uhuru na Umoja,
Mzee Kimaro namjua vyema sana tena sana.

Alikuwa mtu muungwana na nawajua hadi wanae.

Waulize kama watanisahau ni kwa kuwa walikuwa wadogo.

Mimi sina tatizo la ghitilafu baina yetu.
Kinachonishangaza kwako na kwa wengi ni jinsi historia hii inavyowachoma.

Nadhani umesoma hapa niliyoeleza yaliyotokea mara tu baada ya uhuru katika mradi wa TANU wa kuandikia historia yake mradi ambao uliongozwa na Abdul Sykes akisaidiwa na Dr. Wilbard Klerruu.

Ikiwa umesoma utakuwa unajua kuwa wengi ndani ya TANU yenyewe walijuta kwa nini nchi ilikombolewa na hawa?

Kilichotokea ni njama za kufifilisha historia hii na wazalendo wote.

Baba yangu aliona historia yote ya TANU ikijifingua machoni pake si kwa kuwa baba yake alihusika toka enzi za African Association 1929, la hasha ni kwa kuwa waasisi wawili wa chama chenyewe Abdul na Ally Sykes walikuwa rafiki zake toka udogoni na wakimweleza kila kitu.

Lakini kwa wakati ule 1950s hakuna aliyejua kama mambo haya yatakuja kuwa makubwa kupita makamo yao.

Hii ndiyo sababu unaona mimi najua mengi katika historia ya TANU na sidhani kama kuna mtu anaweza kusimama na mie katika hili.

Muhimu kwako ni kuwa chukua tahadhari kwangu na chunga ulimi wako.

Nakuwekea hapo chini picha niliyopiga na watoto wa Abdul Sykes siku waliponionyesha Medali ya Mwenge wa Uhuru aliyotunukiwa baba yao (post humus) ambayo wao wanaamini imetokana na mimi kuandika maisha ya baba yao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

20170429_185254.jpg

Kulia: Ilyas Abdulwahid Sykes, Daisy Abdulwahid Sykes, Mwandishi akiwa ameshikilia Medali ya Mwenge wa Uhuru, Misky Abdulwahid Sykes na Kleist Abdulwahid Sykes
 
unaweka mapicha tu ya watu na 'vibagarashia' vilivyotoboka
weka ushahid wa maandishi wacha hizo ngano zako,unakuja kuleta stor za kusimuliwa hadith njoo ...uongo njoo

sasa kama kisomo dawa nyerere asingeenda uno babu zako wangesoma tu wazungu waondoke

toka uhuru mpaka sasa, ulivyozaliwa mpaka leo povu linakutoka serikali inawaonea kasome kisono kitatue matatizo yenu!
Mtanganyika...
Umeghadhibika na unakuja na matusi.

Katika hali kama hii inakuwa shida kukujibu maana hauko katika hali ya
utulivu.

Mimi nitakusubiri hadi pale chembelecho, ''povu,'' litakapokutulia.

Ila kitu kimoja mimi siandiki ngano na laiti ningekuwa naandika upuuzi
hakuna angaenisikiliza.

Angalia hapo chini:
  1. PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
  2. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
  3. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006
  4. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
  5. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
  6. Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
  7. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
  8. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
  9. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  10. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  11. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  12. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  13. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  14. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  15. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  16. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
  17. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
  18. 14. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.
  19. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
  20. Awards: Several Awards.
  21. Visiting Scholar: (2011)
  22. University of Iowa, Iowa City, USA
  23. Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
  24. Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
  25. OTHER COUNTRIES VISITED
  26. Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 
sasa hiy pc ya huyo mjukuu ya nn?
sawa na humu ukimaliza koment uanze kuweka picha ya makongoro o madaraka nyerere!

au kisa kavaa kanzu ya kusomea kisomo...
Mtanganyika...
Picha inazungumza maneno elfu moja.

Nimeweka picha ya Sheikh Zukheri El Bukhri nia ni kuonyesha kuwa
nafahamiana vyema na ukoo huu na nimejifunza mengi kutoka kwao.

Napenda nikufahamishe kitu kingine kuwa ukoo huu umetoa watu wenye
akili sana hadi hii leo kuanzia ujuzi katika elimu ya dini hadi computer
science na utunzi wa mashairi.
 
Back
Top Bottom