Uhuru na Umoja,
Mzee Kimaro namjua vyema sana tena sana.
Alikuwa mtu muungwana na nawajua hadi wanae.
Waulize kama watanisahau ni kwa kuwa walikuwa wadogo.
Mimi sina tatizo la ghitilafu baina yetu.
Kinachonishangaza kwako na kwa wengi ni jinsi historia hii inavyowachoma.
Nadhani umesoma hapa niliyoeleza yaliyotokea mara tu baada ya uhuru katika mradi wa TANU wa kuandikia historia yake mradi ambao uliongozwa na Abdul Sykes akisaidiwa na Dr. Wilbard Klerruu.
Ikiwa umesoma utakuwa unajua kuwa wengi ndani ya TANU yenyewe walijuta kwa nini nchi ilikombolewa na hawa?
Kilichotokea ni njama za kufifilisha historia hii na wazalendo wote.
Baba yangu aliona historia yote ya TANU ikijifingua machoni pake si kwa kuwa baba yake alihusika toka enzi za African Association 1929, la hasha ni kwa kuwa waasisi wawili wa chama chenyewe Abdul na Ally Sykes walikuwa rafiki zake toka udogoni na wakimweleza kila kitu.
Lakini kwa wakati ule 1950s hakuna aliyejua kama mambo haya yatakuja kuwa makubwa kupita makamo yao.
Hii ndiyo sababu unaona mimi najua mengi katika historia ya TANU na sidhani kama kuna mtu anaweza kusimama na mie katika hili.
Muhimu kwako ni kuwa chukua tahadhari kwangu na chunga ulimi wako.
Nakuwekea hapo chini picha niliyopiga na watoto wa Abdul Sykes siku waliponionyesha Medali ya Mwenge wa Uhuru aliyotunukiwa baba yao (post humus) ambayo wao wanaamini imetokana na mimi kuandika maisha ya baba yao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kulia: Ilyas Abdulwahid Sykes, Daisy Abdulwahid Sykes, Mwandishi akiwa ameshikilia Medali ya Mwenge wa Uhuru, Misky Abdulwahid Sykes na Kleist Abdulwahid Sykes