Halal badr, tawaswil na visomo vilivyosomwa wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika

sasa hiy pc ya huyo mjukuu ya nn?
sawa na humu ukimaliza koment uanze kuweka picha ya makongoro o madaraka nyerere!

au kisa kavaa kanzu ya kusomea kisomo...


ULITAKA AWEKE PICHA YA PENGO NA WAZEE WA KANISA LAKO
 


HAYA FURAHIKA NA HII PICHA YA RAISI WAKO AKIPIGA MAGOTI


 

Attachments

  • upload_2017-9-21_6-20-1.jpeg
    27.9 KB · Views: 69

Wanae ni kaka kaka zangu, ingawa sasa wamebaki wawili tu. Ni kaka na dada yangu kwakua Yeye Kimaro na Baba yangu ni laka na mdogo toka nitoke. Na walikua wote Bandari ingawa Baba alikua director CMB, sijui kama walilumbuka kampuni hii?

Miaka ya ya themanini CMB directors walikua wakiendeshwa na Toyota 4x4 za nguvu mno na nadra kuona kampuni or mashirika mengine wakati huo Mabosi wa Bandari kama General Manager Joseph N Kimaro walikua wamepewa "Nissan Sendrik" Gari ndogo lakini zikitamba miaka hiyo. Nakumbuka, Jioni nilazima walinzi wa bandari lazima waje toa ulinzi kwa wakuu wa bandari, nliwaona home.

Kipindi hicho, doctor wetu alikua bwana Eden Maro, alikua hapo muhimbili, alienda masomoni Uingereza na kurudi 1991/2 na kufika nyumbani. Nilisikia alikua doctor wa Mkapa.

Anyway, nliishi maisha mazuri sana wakati wa uhai wa baba yangu na niliendelea kuishi vizuri nikiwa nyumbani kwa Baba mkubwa Joseph N Kimaro.
 

Picha hii nimeiona sio mara moja, umeipost si chini ya mara mbili ingawa sikujihusisha na mada husika bali nilipita kimya kimya.

kwanini unanionya niwe mwangalifu na wewe na nichunge ulimi wangu? ilhali sija kutusi or kukushambulia? Mada ziletwazo humu lazima zisomwe na wakati mwingine contents za mada hizo lazima zichambuliwe na watu wenye ufahamu, mimi nikiwa mmoja wao.

Kuwa na muono or maoni tofauti haimaanishi ya kua, mada husika inanichoma, la hasha! Katika Dunia hii, hutapata kukutana na mtu atakaye kubaliana na wewe kwa kila kitu, si wewe tu yeyote. Hakuna mtu atakuna na mtu atakayekubaliana nae kwa kila jambo, ni nature ya wanaadam.
 
Uhuru na Umoja,
Sasa unaandika kama muungwana.
Ahsante sana.

Tunaweza kuendelea na mjadala bila shida.
 
Kaka Mohamed Said , nini maudhui ya bandiko lako hili?, yaani unataka kutuaminisha kuwa Halal Badr inafanyakazi kweli na ni kitu cha kidini hasa na wala sio Shirk?

Nyerere na viongozi wengine wa TANU kufanyiwa hiyo Halal Badr ndio kumeifanya hiyo Halal Badr iwe shwahihi?

Binafsi sijakuelewa uanataka kusema nini?, kama ntakuelewa basi mtu wa kwanza ningependa asomewe hii kamà walivyosomewa Wakoloni basi ni Prof. Lipumba
 
Kituko,
Hapana sijasema mahali popote kuwa Halal Badr inajuzu.

Mimi kama mtafiti wa historia nimeeleza tu yale ambayo niliyoona katika utafiti wangu.

Unaweza kurudia kusoma bandiko langu kwa uelewa zaidi.

Kuna mengi na mengine nimeshuhudia kwa macho yangu utotoni yakifanyika ingawa siku hizi naona hakuna tena na nimeyaandikia mathalan kupunga mashetani.

Naingia maktaba nikipata kitu nitaweka hapa kwa faida yetu sote.
 
Uhuru na Umoja,
Sasa unaandika kama muungwana.
Ahsante sana.

Tunaweza kuendelea na mjadala bila shida.

Wewe hutaki or hupendi kupingwa kwa hoja unachotaka ni watu kukaa kimya.

Sidhani kama ni sahihi. Huku tutaichambua tu mada, kwa kina.

Hii ni nchi yetu sote na ni wajibu wakila mmoja wetu kufanya jambo litakalo leta tija kwa Taifa kadri ya uwezo wake: usalama, amani, upendo, mshikamano baina ya watanzania bila kujali itkadi zao za kisiasa ama kidini na usalama.

Ni wajubu wakila mmoja wetu, kukosoa, kukemea maovu ama waovu wenye mrengo wa kuvunja ama kuhamasisha uvunjwaji wa amani, upendo, mshikamano na usalama wa taifa letu.

Amani, upendo, mshikamano are among executive virtues this great nation has for so long been known for.

Tusiharibu haya kwa visingizio.

Mimi usinichukie, nipo humu, na nitaendelea kuwepo nikitimiza wajibu wangu kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

Zidumu fikra za Baba wa Taifa, Julius K Nyerere.
 
Uhuru n Umoja,
Mbona napingwa sana hapa JF na sijatukana mtu au kutumia lugha chafu kwa hilo?

Historia hii haina uhusiano wowote na kauli mbiu za siasa na mengineyo.

Toa hofu sina sababu ya kukuchukia ati kwa kuwa unanipinga.

Tuendelee na mjadala.
Mimi hupata faraja sana ninapoisomesha historia hii kwa watu kama nyinyi ambao hamkuwa mnaijua kabla.
 


ulisahau kulipongeza kanisa Katoliki ambalo lilikuwa likimwelekeza Nyerere nini afanye katika utawala wake
 
Historia inabaki kuwa historia na mengi ambayo mohamed anayoyaandika wengine tumehadithiwa hivyo hivyo kama yeye anavyoandika. Mimi nimekulia mtaa wa sukuma na sikukuu.Nyumba tuliyokuwa tunakaa ilikuwa inatizamana na Makao ya Yanga na kwa upande mwingine inatizamana na chuo cha sharif abdulrahman.
Ingawa nilikuwa mdogo lakini nakumbuka kuna wakati mwalimu na wazee walikuwa na vikao vyao ndani ya klabu na huko njee ili kuwa inapigwa taarab ya geresha na umati kujaa. Sisi kama watoto tulikuwa tunapenya hadi ndani na nimeshawahi kuona ikipigwa dua kali na mwalimu akiwa amekaa kati akizungukwa na wazee ambao walikuwa wanamsomea .
Ukweli utabaki hivyo hata tukiupinda namna gani utabaki tu. Ni bora tuukubali kwa sababu hakuna njia nyingine ya kukabiliana na ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…