Elections 2010 Hali halisi vituoni siku ya kupiga kura

hivi hawa waandishi wa habari wa kitanzania wana matatizo gani?wamesoma wapi?mbona wanauliza maswali ya kipuuzi ?

nimeangalia live footage kupitia Star TV waandishi wanamuuliza kikwete maswali, wengine wanamuuliza umempigia kura nani?wengine ooh uliwahi kuwateua wapinzani wawe wabunge kwa nini kwenye serikali ijayo usiwateue wawe mawaziri?kikwete alichukizwa na swali hili akamjibu muda huu watu wanazungumzia uchaguzi kwanini aulizwe maswala ya serikali?mbona matokeo bado?wakawa wanarudiarudia kuuliza maswali yasiyo na kichwa wala miguu mpaka kachukia
 
Star tv wapo live muda huu Kijiji cha Gongali(ni) huko Karatu wanamsubiri dr slaa aje apige kura kisha wamhoji

mlio majumbani angalieni mahojiano haya
 
Nawaomba wagombea wapite vituoni kuwakagua na kuwakumbusha mawakala wajibu wao wa kuthibitisha utambulisho wa wapiga kura.
 
Mimi nimepiga kura Salasala A. Mambo ni shwari japo mawakala wa vyama sikuona wakifanya uhakiki wowote isipokuwa 1 ambaye alikuwa anaweka tiki tu katika daftari.
Baada ya hapo nikaenda sokoni kununua mahitaji. Nilipowauliza vijana wanaouza bucha kama wameshapiga kura wakanijibu, "Kura ya nini? Kikwete haondosheki hadi kipindi chake cha miaka 10 kipite!". Nikauliza kama wanatambua nguvu ya kura zao katika kuleta mabadiliko katika nchi, wakadai, "Haturidhiki kabisa na maisha haya, lakini nani atakayefanya mambo tofauti? Hata mwingine atakaeingia ni yale yale tu..."
Nimesikitika sana.
 

Tuwaambia hawana weledi, wananuna..
 
Kuna jamaa mgombea udiwani kupitia CCM hapa Sinza alitaka kujipenyesha aingie kwenye kituo kwa 'wadhifa ' wake watu wamemkomalia likatokea zongo polisi wakamtuliza nitawapandishia video clip mara tu nitakapomaliza kupiga kura na kurudi home


Kazi yako nzuri sana!Endelea kutuhabarisha
 
mimi nimepiga kura yangu ktk kituo cha bunge hapa dar.. mambo niu shwari lakini nawasiwasi na wasimamizi kwa kua kata hii inaujanjaujanja mwingi sana.. tafdhali waheshimiwa mnaomsimamia mgombea wa ilala pale kuna vijana wa ifm kama wa4 wanawafuata watu na kuwataka wapige ccm,, kwa kifupi wanapiga kampeni.. tafadhali naomba muwafuatilie nampite vituo vyote jamani
 
Tayari nimepiga kura yangu kwakweli safari hii uchaguzi unatia hamasa sana kwenye kituo cha Muhimbil hali ni shawri ila watu wa Nec wako slow sana,Habari iliyo juu ni CHADEMA time for chage jamani ndio hii
 

Chadema hamuishi visingizio na shaka.Ikiwa mumeshindwa kuwajuwa mawakala wenu mpaka hapo.Mukishindwa isitafutwe sababu.Si kwamba mutaibiwa kura bali chama hakiko makini kama vyenzao vya CCM na CUF.
Hata mukishinda nchi itayumba sana na uongozi wenu.
 
mkuu natumai umeshapiga kura yako... hivyo basi nakutakia majibu mema....
 
Hali ya vurugu imeripotiwa huko Mwanza pamoja na Musoma
 
Mimi na familia yangu tumepiga kura leo mapema sana, hali ilikuwa ni nzuri tu pale kituoni-sinza. vijana kwa wazee wamejitokeza kwa wingi sana japo ni wazi vijana wamejitokeza kwa wingi zaidi na on my way back home nilisimamishwa na kijana mmoja akitaka ajue kama nimeshapiga kura, kwakweli inatia moyo sana. Nimeongea na mama 70yrs now amenithibitishia kuwa amepiga kura ya "mabadiliko". Ni raha iliyoje.
 

Kajifunze kiswahili kwanza...........then come back with ur crap.....
 
SOKET: Watendee haki wan JF kwa kuwaeleza kwa undani juu ya matukio hayo. Na elezea kama ni ya kisiasa, kiukoo, au kifamilia.
 
Toa taarifa zenye maana ili tuelewe unachotaka kutueleza. Tupe na picha au chaanzo cha habari
 
The biggest fear CCM had was the turn out of the youth. The YOUTH ARE CHADEMAs ASSETS and our campaign manager Prof Baregu cautioned CCM that if all registered youth go to the polling station on the election dad (D-Day), then CCM will be VOTED OUT!! It is turning out to be exactly that!!! Mind you the YOUTH CONSTITUTE ABOUT HALF OF THE VOTERS TODAY !!!!!!

GO THE YOUTH GO!!! GO FOR CHANGE !!!

!!!!GOD BLESS CHADEMA, GOD BLESS TANZANIA!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…