Hali hii inanikuta mimi au watu wote?

Django unchained

Senior Member
Joined
Sep 3, 2015
Posts
102
Reaction score
158
Habari ...

Nimejenga nyumba nimeimaliza kiasi cha kuweza kuhamia, ila nasumbuliwa na hali ya uvivu sana kwenye kuhamia...wakat mwanzoni nilikua na mzuka wa kujenga na kumaliza ..nakutamani kuhamia.

Nimekua mvivu na mzito kuliko.
 
Uwende na mchungaji mwaminifu mkaifanyie maombi, waswahili huwa wanasotea.

Muda mwingine wanaloga ushindwe hata kuimaliza, wapo watu wanatelekeza nyumba ambazo hazijaisha sio kwamba wameishiwa fedha za kumalizia ujenzi.

Wanakuwa wamefungwa. Wanasahaulishwa kwa uchawi.
Mkafanye ibada ya maombi hapo nyumbani,utapata wepesi.
 
HAAAAH....
Unaishi kwenye karne ya giza....
 
Mara nyingi hii inatokea after kupanga kwa muda mrefu.

Unakuta nyumba uliopanga imerembwa hatari, mara taa za kwenye gypsum, heater ya maji ya kuoga, vigae, hangin shelves jikoni, makorokoro kibao. So wana wakija ghetto unakuta wanabaki kukusifia kua umepanga nyumba kali. Akili inazubaa maana unatamani watu wakukute hapo pazuri.

So ukifkiria kwenda kuhamia nyumba sijui maji bado, mara madirisha hawajamalizia alluminium, sijui fence hamna unaanza kuona uvivu.

Pia wapenzi tunaokua nao wanachangia, maana unakuta kadem kako hakataki kwenda kuteseka huko nje ya mji kanataka kaendelee kuosha jicho town kwenye nyumba za kupanga so kanakushawishi uone kua nyumba bado haijakamilika.

Mkuu, kama n pepo kemea kabisa. Beba vitu vyako hamia kwenye mji wako. Hakuna baba mwenye gari lakini kuna baba mwenye nyumba.
 
Habari ...

Nimejenga nyumba nimeimaliza kiasi cha kuweza kuhamia, ila nasumbuliwa na hali ya uvivu sana kwenye kuhamia...wakat mwanzoni nilikua na mzuka wa kujenga na kumaliza ..nakutamani kuhamia.

Nimekua mvivu na mzito kuliko.
Ipige bei au uikodishe
 
Hii ni pointi kubwa sana
 
Endelea tu na huo uvivu ni jambo jema,tena hiyo Nyumba iuze kabisa ili uendeleze uvivu wako na kutokuhama kabisa hapo ulipo.
Unaweza kusema ni mas-hara .. .
Dah sjui ni ni kimenkumba
Au labda ni sawa na mpishi anaepika chakula ila mwisho hua hana hamu nacho..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…