Hali hii inanitokea hadi imekuwa kero kwangu!

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,074
Nashindwa kuelewa ni muonekano unachangia ama nini.

Yaani nikienda kwenye duka la mshikaji yeyote tukiwa tunapiga story za hapa na pale akija mteja kununua kitu akihitaji punguzo anamuacha mwenye duka ananikomalia mimi nipunguzie kwa kudhani mimi ndio mwenye duka.

Hali hii inatokea hata nikipewa lifti, watu wanadhani mwenye gani ni dereva wangu, yaani nimekuwa naonekana boss kila sehemu napoenda wakati mimi muuza simu tena used tu. Kwa vile sipendi sifa hali imekuwa kero kubwa sana kwangu.
 
Kuna jamaa alilalamika hapa kwamba NIDA wame muandikia kitambulisho cha utaifa F, wakati jinsia yake ni M.
Sasa alipo omba ushauri nikamuuliza kwamba, wakati anaenda kujiandikisha NIDA alikuwa amevaaje..??

Sasa nawewe nakushauri, jichunguze mkuu maana kuna mambo mengine hata washkaji zako wa karibu ni ngumu kuku ambia ukweli....

Ahsante,
Naamini utakuwa umenielewa kiutu uzima.
 
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…