PostGE2025 Hali ikiendelea hivi, hata vyombo vya usalama vitachoka kumlindia ugali wake

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
25,968
Reaction score
36,044
Haya mambo yakiendelea angalau mara tano ,sita , nawakikishieni hata vyombo vya usalama vitachoka kumlinda.

Leo watu wameandaa maandamano hewa jamaa wamejaa kwenye mfumo , wamepoteza pesa kizembe na wameishia kujichosha.

Hata hivyo vyombo vya usalama wanachoka kuzurula na hayo magari, siku kuu kama ya leo wengine walipanga kwenye viti virefu wapate moja moto moja baridi.

Ila sasa raia wamekaa ndani ambao ndio hao hao wanaotegemewa kuwauzia askari mahitaji muhimu ikiwemo vyakula (maana sidhani kama huwa wanapewa vyakula viwasogeze sogeze na wao) .

Wengine ndio hivyo wazee wa moja moto moja baridi, na pombe za nyumbani hazinogi, wanakosa mahali pa kwenda kuenjoy na michepuko yao kisa kulinda ugali wa mtu fudenge.


Wengine wanakosa mpaka muda wa kukaa na familia zao kwa amani kisa kulinda ugali wa mtu fudenge (japo huwa wanasema wamekula kiapo cha utiifu) 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wakati wa utoto wangu nilitamani sana kujiunga na hiyo kazi, lakini mizimu yangu iligoma kabisa leo ndio naona umuhimu wake na faida yake kwangu.
 
Walee jamaa wa jezi ya Yanga nj wa dakika za jioni superaSub wakichoka Mapolisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…