Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,599
- 26,263
Sikuwa na nia ya kukujibu lakini ningeacha kuku-quote usingeona post yangu. Nakiri sikufahamu lakini siogopi kukuita MUONGO na MZANDIKI.
Uko sahahi kuhusu bei za vyakula na bidhaa za mafuta. Ziko chini kwa sababu ya ukaribu na vyanzo vikuu vya mafuta. Kwa ujumla bei za hapa ziko chini kwa sababu nchi haina mfumo imara wa kulipa kodi. Bidhaa nyingi zinaingizwa kimagendo. Sehemu yoyote yenye bidhaa za magendo - bei ziko chini. Hii ndio nchi inayoongoza kwa kuingiza bidhaa feki kutoka kwa watengenezaji wa bidhaa za hovyo kutoka nchi ambazo sitazitaja hapa!!
Uongo na uzandiki wako uko katika maeneo haya - barabara na umeme. Na kuwa Somalia inaendelea kuliko Tanzania. Nchi isiyokuwa na maji inazalishaje umeme? Wa mafuta au nyuklia? Au umesikia kampuni ya Beco kutoka uturuki yenye majenereta ndio ukadhani ni issue kubwa?? Nchi hii imejaa wazalishaji wa umeme wa jenereta zinazohudumia mtaa mmoja au miwili na mnamlipa mwenye jenereta!! Nchi hii haina barabara za lami kuunganisha states. Njia kuu ya usafirishaji ni kwa njia ya anga. Na kama unasafirisha kwa barabara kwenda mikoani kwenye barabara za vumbi lazima ufanye kipindi cha kiangazi kwa tena kwa kuwalipa alshabab. Hii ni nchi ambayo haina barabara zinazounganisha nchi jirani.
Waambie wasomaji kuwa njia pekee ya mtu kuingia Somalia ni kwa anga tu. Hakuna reli, barabara wala meli kwenda popote nje ya Somalia.
Hospitali. Asilimia 99 ya hospitali ni binafsi. Ndio unalinganisha na Tanzania?? Serikali haina uwezo hata wa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake - inawezaje kuwa na hospitali zinazofanya kazi!! Huwezi kusikia maji ya bomba hapa. Chimba kisima chako.
Ninachukulia post yako kama ni maoni ya mtu anayefika sehemu akawa na dhana zisizokuwa na msingi! Akaondoka na impressions zisizokuwa na facts nyuma yake.
Declaration of interests: Nimeishi nchi hii miaka 11 sasa. Nimeishi hata huko kwenye states, sio Mogadishu tu. Na uliyosema hapa ni uongo mtupu!!
Mkuu umetema madini.
Kuna kundi la watu sijui kwa kukusa exposure wanachukulia kila kitu cha TZ poa. TZ sio bora ila sasa kufananisha na nchi kama Somalia ni kukosa akili kwa kiwango cha lami.
Sikutaka kujibishana na mleta mada ila a quick google search ingeonyesha karibu yote aliyoongea ni uongo.
Somalia nchi yenye GDP ya 4B USD inazidiwa uchumi na DSM tu let alone TZ nzima.
Hali ya usalama ni factor kubwa sana otherwise wasomali wasingekua wanajazana kwenye nchi za watu wengine leo. Mtu hawezi kimbia kwake kama kumeendelea it's just common sense ndo maana huoni waafrika kusini nchi zingine Afrika ila waafrika wengine kila siku wanakimbilia SA.
Nchi ambayo imepata first ATM 2014 tu ndo ya kufananisha na TZ? Mleta mada mada aseme tu hana exposure ndo maana kazuzuka na Somalia ila mara 100 Kigoma kuliko huko.
Mogadishu gets first cash machine - CNN
People in Mogadishu can now take out U.S. dollars thanks to a new ATM machine, which is the city's first.