BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Nimekuta Wanafunzi na shule nzima ya Msingi Kamama iliyopo Wilayani hapo ina changamoto nyingi ambazo kiukweli inasikitisha sana mzingira yaliyopo shuleni hapo.
Baadhi ya changamoto zinazowakabili Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kamama ni mazingira mabovu ya Vyoo na hata vilivyopo mazingira sio rafiki kabisa kabisa.
Hali hiyo inasababisha baadhi ya Wanafunzi kujisaidia porini kulingana na hali ilivyo, kitu kinachoumiza zaidi kuhusu mabinti pindi wanapo kuwa katika siku zao, wanapata wakati mgumu wakati wa kujistili hali hiyo wakiwa Shuleni.
Hali ya muonekano wa vyumba hivyo kiukweli sio wa wakati tulio nao, hali hizi zilikuwa kabla ya uhuru enzi za kukalia matofali ndio muonekano wa madarasa hayo.
Japokuwa madawati yapo ila vyumba hivyo sio rafiki kwa Mwanafunzi kupata elimu.
Kipindi cha kiangazi vumbi ni lao, masika mvua na tope ni jambo la kawaida kulingana na hali ilivyo.
Pia soma:
~ Baada ya picha za vyoo vya Shule ya Kamama (Uyui - Tabora) kuziweka hapa JF, nimeona wanajenga vyoo vipya
~ Miundombinu ya Shule ya Msingi Kamama yaboreshwa, Vyoo na madarasa vyajengwa