Nilitegemea majibu hayo ya chuki toka kwako, ingawa ulijaribu kuficha muhemuko, nashukuru umejiweka wazi.
Lakini wenye mawazo ya "kabila" hiyo ni wale wanufaika wa kifo chake pekee.
Rudia tena kufanya utafiti wako mitaani uone kama raia wa Tanzania wana msimamo gani kifikra kwa sasa na namna wanavyougulia maumivu ya ugumu wa maisha kwa sasa.
Hayo ya kusema "Satanic icon" ni chuki tu tulishazoea kusikia haters wakiropokwa hayo kila siku.
Na ujue kwamba hakuna binadamu anayeweza kumjaji binadamu mwingine kwa matendo yake isipokuwa Mungu mwenyezi pekee.
Sisi waja ni kama nyani anayecheka tupu la mwenzake wakati anachokicheka kwa mwenzakw, kwake mwenyewe kimekaa vibaya sana.
Pia "umenikoti" vibaya namna nilivyoeleza kwamba kuwakumbuka wafu kwa matendo yao mema na kuyachukulia kama somo kwao siyo kosa.
Sijajadili wadhambi wala watakatifu mie.