kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,846
- 20,319
Vyombo vya dola vya Uganda vyamuachia huru Bobi Wine; waliouawa katika ghasia wapindukia 60+SAUTI
Nov 20, 2020 14:27 UTC
PAKUA
Kiongozi wa chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP) ambaye pia na mgombea urais nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu kwa jina la Bobi Wine ameachiwa huru kwa dhamana na mahakama moja ya nchi hiyo. Hii ni baada ya kushtadi maandamano ya ghasia yaliyopelekea makumi ya watu kuuawa kufuatia kukamatwa kwa mwanasiasa huyo chipukizi.
Wine alipandishwa kizimbani leo Ijumaa, na kushtakiwa kwa kosa la kukiuka sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi Uganda (EC) kwa ajili ya kufanya kampeni wakati huu wa maambukizo ya virusi vya corona.
Bobi Wine alikamatwa juzi Jumatano na polisi ya nchi hiyo, kwa kosa la kujaza wafuasi zaidi ya 200 katika mkutano wake wa kampeni, kinyume na kanuni za Tume ya Uchaguzi.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 38 amechiwa huru kwa dhamana na anatazamiwa kurejeshwa mahakamani Disemba 18 mwaka huu 2020.
Watu wasiopungua 68 wanaripotiwa kuuawa katika maandamano ya fujo yaliyoshuhudiwa katika mji mkuu Kampala tokea juzi baada ya kutiwa mbaroni Bobi Wine.
[https://media]Rais Museveni anayeiongoza Uganda tokea mwaka 1986
Waandamanaji walimiminika katika barabara na mitaa ya Kampala, baada ya polisi kumkamata mgombea huyo wa urais akiwa katika mkutano wa kampeni. Mbali na kuuawa, mamia ya waandamanaji wengine wamejeruhiwa huku wengine miongoni mwao wakitiwa mbaroni.
Wine ambaye kwa sasa ni mbunge wa Kyadondo anatazamiwa kuchuana vikali na Rais Yoweri Museveni (76) ambaye yuko madarakani tokea mwaka 1986, katika uchaguzi wa rais wa mapema mwaka ujao 2021.
Soma zaidi[emoji1313]
parstoday.com

Kiongozi wa chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP) ambaye pia na mgombea urais nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu kwa jina la Bobi Win...