Kuelekea tarehe 29.10.2025 itakuwa ni birthday ya mwamba yule anaye sadikika kuwa alufanyiwa figisu Morogoro na wana mtandao kisha kukatisha uhai wake.
Jamii baada ya kutonywa na yule kijana mjanja wa shule ya uongozi wananchi wameapa kutoshiriki haramu tarehe tajwa ,siku hiyo wengi itakuwa ni maandamano na kwenda kuhiji kule alipo lala mwanamageuzi Watanzania ,aliyesema kitu kwa kutenda na siyo hadaa kama za huyo anayezunguka mikoani.
Tetesi zilizopo makada wa chama kile wanataka kufichua makucha yao zikibaki siku mbili kabla ya kwenda kwenye box la kura za kumkataa kuwa hafai kuwa kwenye kiti kile alichokalia.
No reform no election nayo imeshika kasi kwa vijana wa GEN Z kila kona wanalalamika kuhusu awamu hii.
Naona zimebaki siku 26 mtu asulubiwe msalabani na umma.
Watawala mliambiwa mapema mkawa na kibuli hivyo vyombo mnavyoviamini kuwalinda haviko tayari kufanya uharifu hakuna aliyetayari kutoa amri zisizo halali kwa kulinda aliyekataliwa.
Jion njema.
Si uwaseme tu waziwazi, mkuu 'RWANDES', kwani kuna kitu gani cha kuficha wakati kila mtu anaffahamika. Unainyima nguvu mada yako kwa kuandika kama ulivyofanya.
Hao wanaosubiri kuonyesha makucha siku mbili kabla ya Oktoba, waambie watakuwa wamechelewa mno!
Hao ndio wakai huu wanatakiwa wawe mstari wa mbele kumlilia mtu wao aliyekatizwa ndoto zake.
Hata sijui huko kumebaki na akina nani tena, maanake tunawaona akina Bashite; Kalamaganda na wengi wengine wakati huu ndio wanaoimba nyimbo zote za Samia.
Hivi Kalemani aliishia wapi, hasikiki teamna enzi hizi.
Mwisho, nikusihi sana mkuu'Rwandes'; kawaeleze hao watu wa Magufuli, kama kweli wapo, kwamba kama wanartaka na wao wahesabiwe kwenye ukombozi wa nchi hii; ni lazima watoke sasa hivi, na kazi zao zionekane na waTanzania kwamba kweli wanapigania nchi hii.
Nini kinawazuia wasianze leo; kama siyo unafiki ule ule ulioennea ndani ya CCM wasitambuliwe kuwa ni wapinzani, huku wakitegeshea kama Samia atabakia madarakani kwa nguvu.