Hali ingekuwaje endapo matumizi ya ARV yangesimamishwa?

Hali ingekuwaje endapo matumizi ya ARV yangesimamishwa?

Haya mambo sikia tu kwa wenzako omba yasikupate
 

Attachments

  • Screenshot_20250130_093810_com_whatsapp_w4b_StatusPlaybackActivity.jpg
    Screenshot_20250130_093810_com_whatsapp_w4b_StatusPlaybackActivity.jpg
    282.4 KB · Views: 2
mtwnzania bwana, ukimbana sana kwenye mada anakimbia kifo, utafikiri alishaenda peponi na kurudi
walikuwa wanasema ivoivo adi mteule D.T alipovuta shuka kwa juu ndo wakashtuka khee😳kumbe hii shuka si mali yetu tumeazima
 
Hao 1.3 wanajulikana wanatumia ARVs
Umewaza kuhusu ambao hawajapima na hawaoni dalili wapo (window stage)
Hao wanaathirika vipi na zuio la ARV wakati hawatumii? Watakaokufa si ni ambao wanazitegemea, hao 1.3?

Hapo tumeassume ukiacha tu dawa unakufa. Ila kama ukiacha dawa unaweza ukadunda, katika hao 1.3 wengi tu watadunda.
 
- JF, Insta, facebook na magazeti vyote, vingejaa picha na jumbe za Tanzia.

- Akaunti nyingi za kijamii hasa za watu maarufu kama wanamuziki wasanii wanasiasa mainfluencers zingesimama kufanya kazi.

- Baa kubwakubwa na sehemu nyingi za starehe zingefungwa maana wamiliki na baadhi ya wahudumu nguli hawajiwezi tena wamerudishwa makwao kwa uangalizi wa afya zao au wameshatangulia mbele za haki.

- Mitaa na vichochoro vingi vingejaa matenti ya wadau wakishiriki shughuli za wapendwa wao.

- Nyumba nyingi zingekuwa na walau mgonjwa mmoja mwenye ugonjwa usioeleweka.

- Nyumba nyingi zingebaki chini ya uangalizi wa watoto maana wazazi hawajiwezi au wameshatangulia mbele za haki.

- Ambulance na mahospitali yangekuwa bize kushughulikia wahanga, homa zingine zingasahaulika kwanza.

- Baadhi ya Ofisi kubwakubwa za serikali bunge mahakama na za binafsi zingefungwa kwa kupoteza watendaji wake muhimu au wahusika kuhudhuria mazishi ya mfanyakazi mwenzao.

- Humu Jf nyuzi za mambo ya mahaba zingepungua kama sio kwisha kabisa.

- Humu Jf nyuzi za kutukuza na kusifu utukufu mkuu wa muumba zinģetamalaki na kupata mashiko ya hali ya juu.

- Kungekuwa na misururu mikubwa ya costa za abiria hasa kutoka Dar kwenda mikoani zikisafirisha wapendwa wao wakiwa wagonjwa au wafu kwenda maeneo mbalimbali ya nchi.

Wakuu HIV ipo, tujilinde!
Shega tu!

Nyau de adriz
 
Kwani tayari maruweriwe yameanza kusambaa kwa sababu ya hatua ya yule mzee wa miaka 80?Au nami nimepitiwa na ndoto mchana huu?
Haahaa hamna mkuu tunahadharishana tu hapa vinginevo hakuna wa kudumu apa duniani
 
Back
Top Bottom