Hali ingekuwaje kama Mahakama zetu nazo zingekuwa kama Bunge la Makinda?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hivi mdau mwenzangu umewahi kujiuliza swali hili?

Katika mihimili mitatu ya Dola,mahakama ndio mhimili pekee unaotenda haki kwa wapinzani.Mahakama zetu zingekuwa zinafanya kazi kama Bunge kwa kuilonda serikali hakika upinzani leo ungekuwa unasuasua kwa kiasi kikubwa.Mifano ni mingi kuanzia kesi za wabunge,mfano kesi ya mh.Lema na sasa hii ya Lwakatare.

Mwisho, nashauri taasisi zinazohusika na haki za binadamu,utawala bora pamoja na vyama vyote vya upinzani viungane kuitisha maandamano ya kupongeza mhimili huu wa dola kwa kutenda haki na pengine kulaani mwenendo wa bunge la Makinda.

Kama maandamano ni tatizo basi hata watoe salamu za pongezi kwenye vyombo vya habari kama TV na magazeti.
 
Yaani nako kuwe na watu ambao hawajui maana ya IMPOTENCY?
 
Ohhhh, tumuombe Mungu tusifike huko. Yaani Makinda kabaka demokrasia bungeni.
 
ingekuwa hatari sana,,,, kwani Mwenendo wa BUnge letu katika kujadili hoja ni sawa kabisa na Jamii Forums, yaani hoja yeyote ya Chadema lazima itapingwa na CCm kwa wingi wao na humu JF hoja yeyote ya CCM lazima itapingwa kwa wingi wa Chadema humu. Yaani ukiangalia hata lugha zinaotumika humu ni copy +pest toka bungeni, Ni vigumu sana kwa hoja za Wa- Tanzania kwa faida ya Tanzania kujadiliwa bila kulazimishwa kuwa na upande hata ikibidi kwa matusi!! Sasa pale mahakamani sijui pangekuwaje ati.....? anyway nahisi ndio Watanznaia tulivyo so huo ni utamaduni wetu...au?
 

Aah! Muarobaini Mchungu! Unataka kusema kuwa na JF nayo imefikia hivi?
 
Aah! Muarobaini Mchungu! Unataka kusema kuwa na JF nayo imefikia hivi?
View attachment 92877

haahahaa kwa picha hiyo nini hakimo humu? Chakaza ni ukweli tupu nilichokiongea hapo juu, japo katika kipindi kifupi nimeona inaelekea kupata 'balance fulani hivi in terms of ''mipasho'' yaani CCM nao wamezama kujibu hoja humu ndani which is good kwetu sie tusiowaumini wa vyama hivi. I wish itafikia siku hoja zikajadiliwa na nguvu ya hoja ikachukua nafasi, mipasho ikatoweka.. manake nahisi watu humu ndio watakaokuwa wabunge ama ni wabunge so labada watalibadili bunge letu wakipata nafasi..Then!!!
 
Msimlaumu wakat wa wanawake kuwa viongoz bado,amelazmishwa,na ccm
 
Nimekupata mkuu wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…