Hali ishaanza kuwa mbaya hapa Geneva, Corona anataka kuletea balaa

Parabora

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2019
Posts
1,504
Reaction score
2,221
Hapa katika nchi ya Switzerland hali haikuwa ya kutisha, lakini tangu wiki hii ianze mambo yamebadilika Corona anasambaa kwa kasi, mpaka leo kwa takwimu za serikali tayari kuna caases 4002 nchi nzima waliothibitika na ugonjwa huu na watu 982 ambao ni wa maambukizi mapya, watu waliokufa mpaka leo hii ni 45 akiwemo Mwafrika mmoja raia wa Zimbabwe, na vifo vipya mpaka muda huu vimeongezeka kufikia 18.

Uzuri ni kwamba kwa wote waliobaki hakuna mgonjwa aliye serious, wote wana unafuu na wengi karibu asilimia 96 wanatarajiwa kuruhusiwa kurudi makwao.

Kuna mitaa tayari mamlaka za serikali haziruhusu watu kutoka nje ya nyumba yako kwa mujibu wa tangazo la jana kwenye television. Maafisa usalama na watu wa afya wametapakaa kila kona ya mitaa hiyo wanapulizia madaa, maahitaji ya nyumbani yote wanaagiza online na yule anayekuletea huwezi kumuona, yeye anafika nje ya mlango wako anaku-notify kuwa amefika anaacha mzigo anaondoka.

Migahawa yote na hotel kubwa na ndogo za hapa Geneva kama Mövenpick Hotel & Casino, InterContinental, Ari Resort Apartments, Hotel Beau Rivage na nyinginezo zina vipimo maalum vya korona ambavyo vinaweza kumtambua mgonjwa ndani ya masaa 24 tu baada ya maambukizi, japo serikali ya huku imejipanga sana lakini usaambaji wa huu ugonjwa ni mithili ya zimwi.

Huko nyumbani Tanzania naona watu wanaleta mzaha na huu ugonjwa, ukianza kuchanganya mtatafutana, ukweli mtatafutana. Tuombe tu Mungu atuepushe maana hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Mpaka ninavoandika hapa nimechungulia kwa taarifa za Africa vifo vya ugonjwa huu vimefika 16.

Misri 6
Algeria 6
Morocco 2
Bukinafaso 1
Sudan 1

Mungu Ibariki Africa. Mungu ibariki Tanzania na watu wake, waepushie hili janga.
 
Huku tuankutana na video za wanaojiita masupa star wakichukulia poa...na waengine wajitenga na kukaa ndani ya mahoteli. Wengine wanadiriki kufanya mpaka press conference kuuelezea uma juu ya maambukizi yao. Takwimu halisi huku hakuna.

oVAAAAA
 
Imeisha hiyoo,kama hapa bongo kuna vurugu na jam ya kila aina full misongamano lkn mpaka sasa hakuna hata aliekufa inamaana kwa bongo hapa huyu mdudu kashindwa. Naamini ugonjwa upo hapa Bongo tena kwa watu weengi sema umebuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa taarifa, nimatumaini yangu kwa sasa hauna mpango wa kurudi Tanzania, usije kutuletea virusi kama tulivyoletewa na baadhi ya watanzania wenzetu wazalendo kama isabella na wenzake
 
Ahsante kwa taarifa, nimatumaini yangu kwa sasa hauna mpango wa kurudi Tanzania, usije kutuletea virusi kama tulivyoletewa na baadhi ya watanzania wazalendo kama isabella na wenzake
Mkuu mipaka haijafungwa na naweza kurudi tu, lakini sio mgonjwa mimi mkuu labda niupate kwenye ndege
 
Wakuu hili joto la Dar mmeliona? Kama kweli kirusi hakikai kwenye mikoa ya joto basi sehemu kubwa tumenusurika kwa sehemu flani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiniambia wana nafuu wanatarajia kuruhusiwa kurudi makwao unamaanishaje? Kwamba 1.Wamepona? 2. Hawana virus tena? Au 3. Wanavyo bado?. 4. Huko hawatawaambukiza wengine?. 5. Havitawarudia na kuanza kuwaambukiza wengine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu kwa mjibu wa serikali asilimia kubwa ni kama wamepona.
watawekwa chini ya uangalizi kwa mda sehemu maalum.
kwa huku serikali iko makini japo hili gonjwa ni kama zimwi lakini mamlaka za serikali zinafnya kazi zake kisawasawa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…