Hali mbaya ya bei za vyakula nchini, kwanini mawaziri husika wasijipime katika hili kama wanatosha au laa!

Hali mbaya ya bei za vyakula nchini, kwanini mawaziri husika wasijipime katika hili kama wanatosha au laa!

MR.NOMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
339
Reaction score
505
Wakuu kwema!

Hali ya bei za vyakula inatishia kwelikweli, mawaziri husika hawaoneshi jitihada zikaeleweka na bei zikashuka kwanini wasijipime na wakaamua kutupisha na Ili tupate watu wanaoweza kudhibiti Hali hii.

1. Mchele 3000-4000/-
2. Maharage zaidi ya 3500/-
3. Unga zaidi ya 2000/-
4. Nk.

Kama mahindi, mpunga, maharage na hivyo vingine vyote vinalimwa hapa nchini, kwanini tulishindwa kudhibiti usafirishaji wa bidhaa hizi nje tangu mapema na Sasa wananchi wanateseka? Kwa hili inatakiwa mawaziri husika wajitathmini.
 
Mkuu mvua zinanyesha nenda shamba ukalime then uje ukifiche chakula chako usimuuzie mtu ujilie tu.
 
Mbona wakuu mnajibu kwa hasira Sana. Nini tatizo au ndio njaa Kali na nyie?au nyie ndio mnanufaika na huu mfumuko wa bei za vyakula.
 
Mpuuzi sana Wewe kwanza umelima au unaharisha tu hapa. Yaani watu wakulimie wewe ule rahisi.
Huna akili kabisa. Funga domo kalime ndegelesiii
Unadhani ntakujibu kwa matusi kama ulivyonitukana. Walaah! Sina uhakika na uwezo wako wa kufikiria na hivyo nakushauri uendelee kutukana tu watu popote pale, ipo siku utavuna ulichopanda mkuu. Thanks
 
Kuna njia rahisi ya kupima unachokifikiria

Fanya tu kufikiria mara mbili,
1. Mara ya kwanza fikiria kama ulivyofikiria kama mnunuzi na mlaji anayeuziwa mazao bei 'ghali'. Na ndiyo tayari umeshafikiria. Done
2. Mara ya pili fikiria kama wewe ndo mkulima aliyezalisha mazao hayo kwa gharama, muda na pembejeo na bado akahifadhi ili yamsaidie leo anataka kuuza kwa bei 'nzuri'.

3. Nyongeza; ukikamilisha kufikiria mara hizo mbili jaribu kuongeza na levo moja zaidi. Fikiria mara ya tatu kama serikali ambayo inapaswa kutetea matakwa ya wote hao wawili bila kuonea wala kupendelea upande. Halafu ndio utupatie jibu tufanye nini!?

Maelezo zaidi kuhusu ufikiri yapate katika video
 
Back
Top Bottom