Mkuu matatizo ya nchi hii ni zaidi ya CCM...hata tukibadili chama bado watu walioshika nafasi za utendaji na za maamuzi ni wale wale na mifumo ndio inafanya life kuwa tafu zaid...yawezekana CCM wamechangia kwa kiasi fulani lakini tukijitazama sisi Mmoja mmoja utakuta matatizo tunayo ndani yetu mfano Rushwa haihitaji mtu awe CCM, au kupandisha bidhaa kiholela haitokani na chama bali mtu binafsi na tamaa zake...tumefanya haya mambo kuwa utamaduni wetu...tukibadili mienendo yetu basi mifumo itabadilika na hivyo viongozi nao watabadilika na kurudi kwenye mstari...tukitazama matatizo yetu yote kuwa chanzo zhake ni CCM basi hatutayatatua kamwe coz CCM ikirudi madarakani tutakata tamaa kwa kuhisi matatizo yetu hayatapewa suluhisho wakati tuna uwezo wa kutatua baadhi ya mambo sisi wenyewe.