ni lazima maovu ya ccm yaanikwe ili watu wajue kuwa hakifai, ili wapate sababu ya kukiacha chama hiki kinachokumbatia mafisadi. Wananchi wana haki ya kujua uchafu wa ccm ili wafanye uchaguzi uliokwenda shule!
Sera za sisiem ni kutoa ahadi? kila anapopita huyu mkwere anasema nitawajengea daraja, mara ooh...nitajenga kituo cha afya.......hizo ndio sera za sisiem? THINK..........
Nina mashaka sana kama nchi yetu itakuja kuongozwa na chama cha upinzani badala ya CCM. mashaka haya yanatokana na mbinu zinazotumiwa na upinzani kwamba wakiwashambulia CCM na viongozi wake badala ya kutoa sera mbadala ndio njia bora kabisa kabisa ya kupata ushindi. Kwanza nilidhani wao watakuja na sera ya namna ya kutatua matatizo ya wananchi na utekelezaji wa sera hizo. Ni maoni yangu tu.
JINAMIZI la uchakachuaji wa matokeo ya kura za maoni pamoja na migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini jana liliipa CCM mtihani mgumu baada ya wananchi katika maeneo tofauti kumzomea mgombea na katika eneo jingine kumpa wakati mgumu mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete
Mkuu matatizo ya nchi hii ni zaidi ya CCM...hata tukibadili chama bado watu walioshika nafasi za utendaji na za maamuzi ni wale wale na mifumo ndio inafanya life kuwa tafu zaid...yawezekana CCM wamechangia kwa kiasi fulani lakini tukijitazama sisi Mmoja mmoja utakuta matatizo tunayo ndani yetu mfano Rushwa haihitaji mtu awe CCM, au kupandisha bidhaa kiholela haitokani na chama bali mtu binafsi na tamaa zake...tumefanya haya mambo kuwa utamaduni wetu...tukibadili mienendo yetu basi mifumo itabadilika na hivyo viongozi nao watabadilika na kurudi kwenye mstari...tukitazama matatizo yetu yote kuwa chanzo zhake ni CCM basi hatutayatatua kamwe coz CCM ikirudi madarakani tutakata tamaa kwa kuhisi matatizo yetu hayatapewa suluhisho wakati tuna uwezo wa kutatua baadhi ya mambo sisi wenyewe.