Hali ngumu ya maisha ya nyumbani ndo ilisababisha mwanafunzi kutaka kuacha shule

Hali ngumu ya maisha ya nyumbani ndo ilisababisha mwanafunzi kutaka kuacha shule

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Baada ya kufuatilia tukio zima la mwanafunzi wa darasa la sita kuchapwa na mwalimu wake hadi kuumia mkono, huko mkoani kilimanjaro nimegundua mambo kadhaa toka kwenye familia yake

Familia anayotoka ni duni sana ,mama yake anafanya vibarua vya kufua kwa watu japo sio mara zote hupata kibarua, baba yake nae hana kazi maalumu. Na wazazi wote hawana hata simu ya mkononi.

Nguo za shuleni zimechakaa na ambayo akivaa ikiwa na ubora basi wanafunzi waliomaliza la 7 ndo wamempatia na mara nyingi nguo hizo zinakuwa kubwa kwake.

Ukosefu wa chakula nyumbani pia na hali duni umemfanya kukosa uchangamfu shuleni na hata kufeli darasa la 4.
yebo yebo anazovaa kwenda nazo shule ni chakavu .


Mtoto huyo anaeleza ya kuwa hata chai nyumbani hawanywi na chakula wakati mwingine hakipikwi hivyo huenda hivyo hvyo shuleni.

Baba wa mtoto huyo alienda hadi ofisini kwa mtendaji wa kata kuripoti tukio la mwanae kupigwa na mwalimu hadi kuumizwa mkono lakini kutokana na kwamba ni familia maskini mtendaji alimjibu akae kimya na hakumpa ushirikiano wowote.



Binti huyo alikaa nyumbani kwa muda wa wiki tatu akijiuguza na pia akawa na hofu ya kuendelea na shule.

Itaendelea. . . .
 
Mtendaji anamlinda mwajiriwa mwenzake.Mungu aisaidie hiyo familia.
 
Back
Top Bottom