A
Anonymous
Guest
Kwema!
Mimi ni mwananchi na mkulima kutoka Wilaya ya Urambo, Mkoa wa Tabora. Tunaomba sauti yetu isikike kuhusu mgogoro mkubwa unaoendelea katika biashara ya tumbaku msimu huu. Hali ni mbaya sana, na wakulima wengi wanateseka.
1. Makampuni yanawakandamiza wakulima
Makampuni kama MKWAWA LTD na GTI LTD yanatoa bei wanazotaka bila kuzingatia ubora wa tumbaku wala kufuata viwango sahihi vya grading. Kwenye masoko, baadhi ya wawakilishi wao wamekuwa wakisema, "Mwaka huu tunawanyoosha wakulima." Kauli na vitendo hivi vimewaumiza sana wakulima wa Urambo, ambao wengi wao sasa wanalia kwa hasara kubwa.
2. Rushwa na upendeleo katika mauzo
Kuna tuhuma kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wanapokea rushwa na kuwapa nafasi ya kuuza watu wasiokuwa wanachama, huku wakulima halali waliopokea pembejeo na kufuata taratibu zote wakiachwa kusubiri bila majibu. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba vyama vingi tayari vimemaliza makisio ya vilo vya tumbaku, ilhali wakulima wengi bado hawajauza na tumbaku zao zimejaa maghala.
3. Uongozi wa wilaya umeshindwa kusimamia haki za wakulima
Pamoja na maagizo yanayotolewa na Mkuu wa Wilaya, watendaji wanaopaswa kusimamia maslahi ya wakulima wanadaiwa kushirikiana na baadhi ya makampuni, jambo linalowaacha wakulima wakipata hasara kubwa na kukosa haki zao.
Tunawauliza viongozi wetu: Je, wakulima watalipaje madeni? Watawalipaje wafanyakazi wa mashambani? Familia zao zitaishije wakati tumbaku ndiyo tegemeo kuu la uchumi wa Wilaya ya Urambo?
Tunamuomba Waziri Mkuu, Waziri wa Kilimo na viongozi wengine wa Serikali msikie kilio chetu na mchukue hatua za haraka.
Zao la tumbaku linachangia kwa kiasi kikubwa mapato ya Wilaya ya Urambo na uchumi wa Taifa. Ni muhimu wakulima walindwe na wapate haki yao.
Tunaomba mtupazie sauti. Wakulima wa Urambo tunalia.

Tunaiomba Serikali ichukue hatua
- Waziri wa Kilimo afike Urambo kujionea hali halisi badala ya kutegemea taarifa za mezani.
- Mkuu wa Mkoa wa Tabora asimame kutetea wakulima kama anavyosimamia masuala mengine ya maendeleo na usalama.
- Serikali ichunguze tuhuma za upangaji wa bei, grading isiyo ya haki, pamoja na vitendo vya rushwa vinavyoathiri mauzo ya tumbaku.