Niende kwenye mada moja kwa moja!!.
Nimekuwa moja ya wahanga wa hili Tatizo kwa muda mrefu sana
Kati ya watu wanaosoma kwa mateso makubwa sana ni watu wenye ulemavu, kuanzia shule za msingi mpaka sekondari, hii inatokana na miundo mbinu mingi kuwa tofauti na Hali zetu watu wenye ulemavu.
Wakati mtu mwenye ulemavu anapambna akiamini kuwa yeye hawez kulima, kutembeza mitumba, Wala kufanya kazi ngumu za ujenzi akitegemea akili yake tu ya darasani angalau impe mwanga wa maisha.
Baada ya ajira huyu mtu mwenye ulemavu anaanza kuzunguka na baiskeli yake au magongo yake kweny interview mbalimbali, wakati mwingine hufanyika mikoani, au kwenye majengo yasiyo na lift.
Wengi wanaishia kukata tamaa sana.
Kuna sehemu niliwahi kataliwa kabisa kisa mimi ni mlemavu kwamba siwezi kufanya hio kazi kwasababu nitakuwa naenda sana hospitali, yaani trip kazini trip hospitali. Wanahisi labda sisi ni wagonjwa fulani hivi,
Inaumiza sana sana, naongea kwa niaba Yao sana.
Wengi walioajiriwa ni sababu za kisiasa, ili ionekane hawabaguliwi hasa kwenye sekta zinazohusiana na walemavu ndio huko wamejazwa!
Nina watu nawajua ni walemavu, wanapitia kipindi kigumu sana lakini wakiwa na elimu Yao kichwani! Yaani huu unyanyapaa huwezi ona kwa jicho la kawaida! Ni dhamira za watu.
Kitanda usicholalia huwezi jua kunguni wake!! We feel pain sana sana
Natimiza mwaka wa saba(7) tangu nimalize digrii yangu ya usimamizi wa fedha..
Serikali haitujali tena, zaidi ya kutulazimisha tukope pesa tuu.
Wadau wapo kimaslahi na kisiasa zaidi wapate attention wakati wanatoa misaada.
Hata vyama vya walemavu sasa hawana la kusema baada ya kulamba sukari
Sisi tukimbilie wapi zaidi yenu wadau wa hapa JF, tusaidieni kupaza sauti sisi walemavu tuliopambana kusoma kwa bidii, tunatamani kubeba tofali angalau tupate mkate wa kila siku lakini Hali zetu hazituruhusu.
Tuliamini katika elimu nayo imetusaliti, nchi imetutenga, tuna hari mbaya sana